Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Kwa Jinsi Mlivyoniogopesha Sasa Naandika Huku Miguu Yangu Nimeipandisha Mezani Na Nilikuwa Nina Mpango Wa Kwenda Kuoga Lakini Nimeusitisha Kidoooooooooooooogo Hadi Nijipange Upya Tena.

Huyu nyoka anapanda juu ya dari bila kugusa ukuta...sasa wewe unasema meza??
 
hawa wadudu nawaogopa mno nikimwona hata kwenye picha nasisimka mwili mzima
 
Nilikuwa na safari ya kwenda Msata kutafuta madini na siendi tena. Nimeambiwa haya majoka yamejaa huko

Jipange tu.
Mbali na Chatu, Nyoka yyt haui mtu kwa kumvizia. Hufanya hivyo km self defense.
Kaa mbali na vichaka na kukaa chini ya miti.
Epuka kutembea peke yako na mara zote tembea na Jiwe la sumu ya Nyoka kamba na Wembe mpya just incase ukigongwa na nyoka hii itaokoa maisha yako.

Hizi ni techniques tulizikuta kwa wenyeji huko porini na zinatumika mpaka leo.

Mkuu unataka kitajirika Fasta?😂
 
Ikitokea amekugonga nini cha kufanya kudhibiti kutokana na nature ya sumu yake inayosambaa haraka?
inatakiwa kutulia, ukitembeatembea au kukimbia sumu husambaa haraka. inatakiwa kijitahidi kumtambua nyoka, maana kila nyoka ana antivenom yake. kufunga kamba kuzuia damu kusambaa. kama unajiwe la nyoka unaweza kutumia. mtu anaweza kukunyonya damu/sumu na mdomo.
 
Kuna video moja niliiona,alizinguliwa na mongoose mmoja mpaka akaliwa,ila anachokifanya mongoose ni kumvizia na kumdaka shingoni,mongoose ni mjanja sana kukwepa strikes za koboko kwasababu zikimpata zinaweza kumdhuru.
 
Unishindi mimi hata wale wanaokula panya nikisikia kaingia ndani nahamia guest house mpaka nihakikishiwe kauwawa na nyumba lazima ifanyiwe fumigation ya maana.

Du noma sana aisee
 
Ana uwezo wa kuuwa watu 12 kwa sekunde chache tu, sio nyoka hata wa kumuota huyo ni balaa na very aggressive akikuona lazima akukimbize na ana speed sana, nilimuona akifukuza panya kwenye matuta yeye alikuwa anapita juu ya matuta imagine that

Ashiiiii.......basi nitaanza kumuogopa.
mie nilijua akija nitampiga hata kwa ndala au ufagio
 

Mkuu hilo jiwe la sumu ya nyoka ndio nini tena, ufafanuzi kidogo.
 
Mkuu hilo jiwe la sumu ya nyoka ndio nini tena, ufafanuzi kidogo.

Sisi tuliolelewa vijijini ndivyo tunavyoliita lkn kwa lugha za Kikoloni hilo jiwe lina majina mengi tu.
Baadhi ni Haya.
Serpent Stone,
Snake-stone,
Viper’s Stone,
Pierre Noire,
Schlangenstein,
Piedra Negra,
Slangensteen au Belgian Stone.

Haya mawe mweusi Yanatumika Dunia nzima kwa kazi hio ya kuvuta sumu ya Nyoka Kutoka mwilini mwa Binaadamu.

Ukiumwa na Nyoka Au Nge au Wale Centipede sisi tunawaita TANDU na Km uko mbali Na Hospitali Basi Unachanja Kidogo na wembe pale ulipoumwa Unaweka hilo Jiwe la Nyoka Linaanza Kufyonza sumu tartiiibu, wakati huo wewe unatembea kwa upole kuelekea Hospitali.

Lile jiwe linakuwa limenasa Kwenye Nyama (pale kwenye jeraha) km Sumaku.
Likimaliza hio Sumu Linadondoka Lenyewe!
Halafu kwetu Usukumani Hayo Mawe Ni Bure tu. Yamejaa kila kona.
Hapo Dar Yanauzwa Kipande km Shs 4000 hivi pale Shimoni kariakoo kwenye maduka ya Dawa ya wazanzibari au waarabu.

Ni jiwe la asili zawadi kutoka kwa Mungu mtukufu. Kwa wale tu wenye imani.
 

Please!!! Kumuua black mamba kunahitajika muwe angalau watatu. Kwa jinsi stori yako ulivyoitoa na kwa kuwa tukio hili lilitokea nyakati za usiku, ndipo mambo yanakuwa magumu zaidi. Hii stori yako iongeze nyama ili tuwexe kukuamini, kwa sasa ilivyo umebugi, kajipange!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…