Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

huyo nyoka ni balaa, kamwe hang'ati mguuni, ila kichwani tena kisogoni ndo anapenda ili ufe haraka

Acheni hadithi za vijiweni....koboko anang'ata sehemu yeyote ile katika mwili wa binadamu na huishi popote si juu ya miti tu hata mapangoni na vichakani. Acheni ujinga wa hadithi za vijiweni kuna watu wamesoma humu.
 
Na mbwembwe zake zote koboko hana ujanja kwa bundi. Ndiyo sababu usiku hatembei.

Koboko anapenda sana kuwinda usiku na anakula sana watoto wa bundi kasoro bundi mwenyewe kwani mkubwa mno. Soma undani wa koboko ama tazama documentaries zake ujifunze, usilete hadithi za vilabuni.
 
Hivi kati ya black mamba na Greena mamba nani hatar zaidi?
Nakumbuka kipind flan nilitembelea mbuga ya mikumi sehem moja inaitwa Genesis nilipata kuoana viumbe mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyoka lakn niliambiwa Green mamba ni nyoka mpole na hana kawaida ya kung'ata hovyo ila ndio nyoka mwenye sumu kuliko nyoka wote.

Niliambiwa Green mamba huwa anaogopwa na nyoka wengne kwan hata kama akijichanganya na nyoka wengne anaweza kuwazuru wote na wakafa.

Unasemaje juu ya hili Dola Iddy

Aina za mamba, huyo wa kijani ana sumu kali.
 
Attachments

  • 1451199789684.jpg
    1451199789684.jpg
    7.5 KB · Views: 402
Last edited by a moderator:
Hivi kati ya black mamba na Greena mamba nani hatar zaidi?
Nakumbuka kipind flan nilitembelea mbuga ya mikumi sehem moja inaitwa Genesis nilipata kuoana viumbe mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyoka lakn niliambiwa Green mamba ni nyoka mpole na hana kawaida ya kung'ata hovyo ila ndio nyoka mwenye sumu kuliko nyoka wote.

Niliambiwa Green mamba huwa anaogopwa na nyoka wengne kwan hata kama akijichanganya na nyoka wengne anaweza kuwazuru wote na wakafa.

Unasemaje juu ya hili Dola Iddy

True to some extent, ila characteristics za green mamba ni kweli uwa mpole na asumbui watu hovyo. Anaweza kujibana kwenye tawi akikuangalia tu ila ukimguza ama akihisi yuko hatarini atakugonga ikiwa uko karibu naye. Wao kwa huku kwetu Afrika hupenda kuishi sana kwenye miembe haswa wakati huu wa mavuno. Sumu yake na ya koboko ni sawa na wala hazina tofauti kwani zote hushambulia mishipa ya fahamu na kukusambaratisha si chini ya dakika 7 kama hujapata matibu ya awali. All the mambas have the same type of poison which is neurotoxic!
 
koboko na black mamba ni vitu viwili tofauti. Black mamba ashambulii hivyo kama mleta mada alivyo tuambia. koboko yes, anashambulia hivyo.
 
Safi mkuu inaonekana una knowledge fulani, ila nimejifunza kitu kwamba kutofahamu ukweli wa hatari za wanyama pia ilichangia sisi tulioishi vijijini kuwa na ujasiri fulani ninasema hivyo kwasababu kuna ujasiri fulani siku za nyuma nilikuwa nao kuhusu hawa wadudu lakini sasa siwezi kabisa kadri ninavyokuwa ninajua tulikuwa tunacheza na hatari wacha Mungu aitwe Mungu
Maelezo mazuri kiasi lakini ingefaa utuambie unayatoa wapi maelezo hayo ili tujue kama yanatokana na uzoefu au siyo ili tuweze kujua thamani yake. Mie ni mmojawapo niliyechunga ng'ombe wakati wa udogo wangu na nilikutana mara nyingi na nyoka huyo. Kwa uzoefu wangu nyoka huyo ni wa aina nyingi; wengine wafupi na wengine warefu lakini wote ni machachari. Rangi yake ni ya kijivu zaidi lakini alama yake kubwa ni huo mdomo mweusi. Maelezo nilikuwa nikipata kwa wazazi wangu kabla sijafungulia ng'ombe kwenda porini yalikuwa: nikikutana na simba au koboko (huyu naye ndiye simba wa nyoka) anashambulia ng'ombe niwaache ng'ombe nirudi nyumbani niwaeleze wakubwa. Hii ilikuwa ina maana nikikutana na dharura nyingine nishughulikie kadri nitakavyoona inafaa. Na kweli nikikutana na wengine kama nyoka mweusi, cobra, pamoja na makeke yake hakunitisha; akipanua mdomo nilikuwa namtupia jiwe la manati na likimpata kwenye domo alilopanua nyoka anakuwa hoi. Black mamba yuko sehemu nyngi mno hapa Tanzania. Anapenda sehemu yenye mvua ya kadri, isizidi inchi 40 za mvua kwa mwaka au sehemu kavu yenye mito au visima vya maji. Kwa hiyo Iringa kavu ya Ilula, Ismani, Pawaga, Idodi; Dodoma, Singida, Tabora, Chunya ni halali yao. Game Park ya Ruaha wako wengi.
Black mamba ni nyoka anayehodhi eneo lake, (territorial snake) hivyo husiamamia mkia na kuchunguza mgeni nayeingia kwenye eneo lake; anaishi zaidi ya miaka 12. Pia bila shaka mnajua nyoka wote hawasikii. Macho, harufu na mtikisiko wa ardhi ndiyo kinga yao.
 
Nilimuona anakimbizwa na Nyegere kama vile kibaka, mtini anae, ardhini anaye, kwenye mawe anaye, mpaka akamdaka na kumtafuna kikatili !

hahah mkuu nyegere ni kitu gani? Tafadhari nijuze mwenzio!
 
20151227114014_zpsobq3fuzv.jpg

Viumbe wengine sijui wana faida gani hapa duniani
 
Nakumbuka mwaka jana nilitembelea kijj flan hv wilayan manyon nkakuta maombolezo, timu ya mpira ya kijiji ilikua inasafir kwa trekta kwnda kjj jiran kushiriki michezo, koboko akadondoka kutoka kwnye mti akaangukia ndani ya trela la trekta basi aligonga wote had dereva wa trekta ndan ya mda mfup tu ikawa kilio
 
Nilimuona anakimbizwa na Nyegere kama vile kibaka, mtini anae, ardhini anaye, kwenye mawe anaye, mpaka akamdaka na kumtafuna kikatili !

Nyegere ni noma mkuu...tena anamla kuanzia kichwani kwenye sumu kali na ikimzidia anazimia kwa muda kisha akiamka anamalizia mzoga anasonga mbele.
 
Nyegere ni noma mkuu...tena anamla kuanzia kichwani kwenye sumu kali na ikimzidia anazimia kwa muda kisha akiamka anamalizia mzoga anasonga mbele.

Nyegere ndo kiumbe gan chief!?
 
Nyegere ndo kiumbe gan chief!?

Huyu hapa mkuu,hakuna mnyama porini anaemtisha kasoro tembo,na ni vile tembo ana ngozi ngumu ila nae asingemfanya chochote,Simba,Chui wote wanamgwaya na binaadam ukikutana nae kama umemchokoza anakimbilia kurarua sehemu za siri(pu*bu).hawa black mamba sijui cobra kenge gani wote anawakamata anawala kuanzia vichwani..
ceaae96d464dfafab8b175eb6f03d549.png
33a68b16725e8d3fae62831033c18570.png
 
Tusijichanganye katika jina wadau koboko na blackmamba ni kitu kimoja sema koboko ni kwa lugha yetu ya kiswahili/kibantu ila kiiengeleza/international anajulikana kama blackmamba
 
Nyegere ndo kiumbe gan chief!?

Huyu hapa mkuu,hakuna mnyama porini anaemtisha kasoro tembo,na ni vile tembo ana ngozi ngumu ila nae asingemfanya chochote,Simba,Chui wote wanamgwaya na binaadam ukikutana nae kama umemchokoza anakimbilia kurarua sehemu za siri(pu*bu).hawa black mamba sijui cobra kenge gani wote anawakamata anawala kuanzia vichwani..
ceaae96d464dfafab8b175eb6f03d549.png
33a68b16725e8d3fae62831033c18570.png
 
Zaidi middo ingia youtube search honey badger&blak mamba angalia utaamini kuna wanyama hawaogopi tatizo bali wanapenda changamoto..nyegere ni mmoja wao.
 
Last edited by a moderator:
huyu nyoka ni noma siku moja aliingia kwenye banda la mbuzi kijijini nyahuwa...ikabaki stori kwa mifugo ile
 
Huyu hapa mkuu,hakuna mnyama porini anaemtisha kasoro tembo,na ni vile tembo ana ngozi ngumu ila nae asingemfanya chochote,Simba,Chui wote wanamgwaya na binaadam ukikutana nae kama umemchokoza anakimbilia kurarua sehemu za siri(pu*bu).hawa black mamba sijui cobra kenge gani wote anawakamata anawala kuanzia vichwani..
ceaae96d464dfafab8b175eb6f03d549.png
33a68b16725e8d3fae62831033c18570.png

Ukitaka kukutana na nyegere chukua fimbo halafu uchape kwenye majivu huku unakatukana ni lazima usiku ukutane nako na kasheshe lake hapo ni balaa zaidi
 
Black mamba hata nyoka wenzio anaua ht kobra then anamla.ni nyoka ambae akiuma binadam 7 steps hupigi.na kumuuma binadam n self defence yk kukuwahi kabla hujamdhuru.hupenda kuishi mazingira comouflage yaani huwez kumwona untrained eyes.is the one of the deadliest snake in the world kills atleast 1000 mens everyyear
 
Back
Top Bottom