mbongo_halisi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2010
- 7,074
- 5,486
huyo nyoka ni balaa, kamwe hang'ati mguuni, ila kichwani tena kisogoni ndo anapenda ili ufe haraka
Na mbwembwe zake zote koboko hana ujanja kwa bundi. Ndiyo sababu usiku hatembei.
Hivi kati ya black mamba na Greena mamba nani hatar zaidi?
Nakumbuka kipind flan nilitembelea mbuga ya mikumi sehem moja inaitwa Genesis nilipata kuoana viumbe mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyoka lakn niliambiwa Green mamba ni nyoka mpole na hana kawaida ya kung'ata hovyo ila ndio nyoka mwenye sumu kuliko nyoka wote.
Niliambiwa Green mamba huwa anaogopwa na nyoka wengne kwan hata kama akijichanganya na nyoka wengne anaweza kuwazuru wote na wakafa.
Unasemaje juu ya hili Dola Iddy

Maelezo mazuri kiasi lakini ingefaa utuambie unayatoa wapi maelezo hayo ili tujue kama yanatokana na uzoefu au siyo ili tuweze kujua thamani yake. Mie ni mmojawapo niliyechunga ng'ombe wakati wa udogo wangu na nilikutana mara nyingi na nyoka huyo. Kwa uzoefu wangu nyoka huyo ni wa aina nyingi; wengine wafupi na wengine warefu lakini wote ni machachari. Rangi yake ni ya kijivu zaidi lakini alama yake kubwa ni huo mdomo mweusi. Maelezo nilikuwa nikipata kwa wazazi wangu kabla sijafungulia ng'ombe kwenda porini yalikuwa: nikikutana na simba au koboko (huyu naye ndiye simba wa nyoka) anashambulia ng'ombe niwaache ng'ombe nirudi nyumbani niwaeleze wakubwa. Hii ilikuwa ina maana nikikutana na dharura nyingine nishughulikie kadri nitakavyoona inafaa. Na kweli nikikutana na wengine kama nyoka mweusi, cobra, pamoja na makeke yake hakunitisha; akipanua mdomo nilikuwa namtupia jiwe la manati na likimpata kwenye domo alilopanua nyoka anakuwa hoi. Black mamba yuko sehemu nyngi mno hapa Tanzania. Anapenda sehemu yenye mvua ya kadri, isizidi inchi 40 za mvua kwa mwaka au sehemu kavu yenye mito au visima vya maji. Kwa hiyo Iringa kavu ya Ilula, Ismani, Pawaga, Idodi; Dodoma, Singida, Tabora, Chunya ni halali yao. Game Park ya Ruaha wako wengi.
Black mamba ni nyoka anayehodhi eneo lake, (territorial snake) hivyo husiamamia mkia na kuchunguza mgeni nayeingia kwenye eneo lake; anaishi zaidi ya miaka 12. Pia bila shaka mnajua nyoka wote hawasikii. Macho, harufu na mtikisiko wa ardhi ndiyo kinga yao.
Nilimuona anakimbizwa na Nyegere kama vile kibaka, mtini anae, ardhini anaye, kwenye mawe anaye, mpaka akamdaka na kumtafuna kikatili !
Viumbe wengine sijui wana faida gani hapa duniani
Mtoa mada umechanganya madesa,black mamba sio koboko.hawa ni nyoka wawili tofauti,hebu jaribu kutafti tena
Nilimuona anakimbizwa na Nyegere kama vile kibaka, mtini anae, ardhini anaye, kwenye mawe anaye, mpaka akamdaka na kumtafuna kikatili !
Nyegere ni noma mkuu...tena anamla kuanzia kichwani kwenye sumu kali na ikimzidia anazimia kwa muda kisha akiamka anamalizia mzoga anasonga mbele.
Nyegere ndo kiumbe gan chief!?
Nyegere ndo kiumbe gan chief!?
Huyu hapa mkuu,hakuna mnyama porini anaemtisha kasoro tembo,na ni vile tembo ana ngozi ngumu ila nae asingemfanya chochote,Simba,Chui wote wanamgwaya na binaadam ukikutana nae kama umemchokoza anakimbilia kurarua sehemu za siri(pu*bu).hawa black mamba sijui cobra kenge gani wote anawakamata anawala kuanzia vichwani..