Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Lakini pia sumu yake akimgonga nyegere(Honey barger) humpa hang over tu kesho yake huyu black mambas na mwezie king cobra wanaonewa sana na nyegere(honey badger),kicheche ( stripped pplecat) na mongoose nguchiro hivi vimnyama vinatafuna nyoka kama ww unavyotafuna papuchi. Easily

Honey Badger na Mongoose wanakula nyoka kama soseji vile
 
mbele ya nguchiro (mongoose) anakuwa mdogo kama piritoni.
kila mjanja ana mjanja wake.that's how nature is
ae365cb28f8b56fe3f8a668a63728f87.jpg
 

Attachments

  • 1462271153002.jpg
    1462271153002.jpg
    57.7 KB · Views: 208
Very nice analysis ingawa hujasema mazingira yapi anapenda kuishi(baridi, joto sana,misituni au katika mbuga) na je harufu au mavi ya ng'ombe yanathari kwake? Kisha naomba kufahamu kama wale nyoka wa majini nao ni aina ya koboko( black mambas)

Nyoka huyu anapatikana katika hali za hewa nyingi nusu jamgwa yupo, ikweta kwenye mvua nyingi yupo na maeneo yenye joto kama Namibia pia anapatikana. Kuhusu kinyesi cha Ng'ombe sinauhakika sana lakini kuna kesi nyingi tu za nyoka huyu kuuwa Ng'ombe wengi tu huko Shinyanga
 
Habari wanaJF,

Leo nataka tufahamishane kuhusu nyoka huyu hatari kwa sisi waswahili tunamuita KOBOKO lakini kwa lugha ya kiingereza huitwa Black Mambas

Black mamba ni moja ya nyoka hatari sana katika dunia. Nyoka hawa hupatikana katika sehemu Mashariki na Kusini mwa Afrika. Black mamba anaweza kuishi katika aina mbalimbali za mazingira: savanna, mabwawa, misitu na maeneo ya miamba. Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu ni sehemu nzuri ya kuishi Black Mamba. Kutokana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa kilimo, makutano kati ya Black Mamba na binadamu yameongezeka zaidi.


View attachment 344401

1- Black mambas ni nyoka mwenye sifa ya urefu anaweza kufikia miguu 14 urefu na 1.58757 katika uzito.

2- Black mamba ana mwili mwembamba kufunikwa na ngozi yenye magamba kama ilivyo kwa nyoka wa jamii nyingine, Pamoja na wao kujulikana kwa kiingereza kama Black mambas lakini hawana rangi nyeusi katika ngozi na rangi ya mwili inategemea makazi yao na inaweza kuwa ya kijani, kijivu au njano.

3- Black mambas ni jina lake kwa sababu sehemu ya ndani ya vinywa vyao ni nyeusi kabisa. Black mamba kuonyesha kinywa chake cheusi wakati anakabiliwa na hatari.

4- Nyoka huyu huanza kutanua shingo yake lakini sio kama afanyavyo COBRA na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa inatoka upepo na hii ni ishara nyingine kwamba kiumbe hutayari shambulio. Ukiona amena moja ya hizo ishara unashauri wa usifanye chochote kwasababu kwa kasi aliyonayo hutaweza kumuwai kifupi tulia mpaka hasira zishuke na ajiondokee narudia usithubutu kujifanya unafurukuta matendo yako hayatawahi tendo lake.

5- Ingawa nyoka huyu amebeba sifa ya kuwa nyoka mjeuri na mkali sana, lakini nayeye hujaribu kutoroka kabla mashambulizi lakini hushambulia kwa ukatiri sana ikibidi. Kumbuka kwa mtulivu ukikutana nae

6- Sasa upande wa sumu hapa ndipo patamu Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa Neuro – hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni Cardio-toxin hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake inaweza kuua.

7-Black mamba anatumia sumu kuwinda aina mbalimbali za ndege na wanyama wadogo. Na hutumia kama kitoweo chake

8- Black mamba anaishi katika mashimo ya miti na katika mashimo ya miamba. Pamoja na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, lakini hana ujanja mbele ya Nguchiro na Mbweha, na Nyegere.

9- Black mamba hutembea haraka sana akiwa juu ya ardhi. Anaweza kusafiri umbali mrefu kwa kasi ya maili hadi 12 kwa saa. Hivyo usijaribu kukimbia atakufukuza mpaka akugonge sehemu ya mwili wako.

10- Jike hutaga mayai kati ya 10 na 25 katika kiota juu ya ardhi. Joto ni muhimu kwa ajili ya incubation ya mayai. Na mayai hujitotoa baada ya miezi 3. Na vijinyoka hivyo vichanga huanza kujihudumia kwa kila kitu na huwa na sumu ile ile kama ya nyoka mkongwe hivyo usije ukadharau.

View attachment 344402

11- Black mamba anaweza kuishi hadi miaka 11 katika pori na hadi miaka 12 katika kama atafugwa.
Jina lake kwa kiingereza anaitwa cobra kuna aina zaidi ya hamsini za cobra mojawapo ni black mamba, kwa hiyo black mamba ni moja ya aina za cobra
 
Jina lake kwa kiingereza anaitwa cobra kuna aina zaidi ya hamsini za cobra mojawapo ni black mamba, kwa hiyo black mamba ni moja ya aina za cobra
Mkuu kuna king cobra na black mamba ni nyoka wa aina mbili tofauti kabisa
03cbca695446de656818d0936bd60d90.jpg
huyu ni king cobra na huyu
8ce958de675881f8fa2272bb0ab2fcfa.jpg
ni Black mamba
 
Asante kwa darasa ila Nguchiro na Nyegele ninoma sana.
 
Mkuu kuna king cobra na black mamba ni nyoka wa aina mbili tofauti kabisa
03cbca695446de656818d0936bd60d90.jpg
huyu ni king cobra na huyu
8ce958de675881f8fa2272bb0ab2fcfa.jpg
ni king cobra
King cobra na black mamba ni aina mbili kati ya zaidi ya aina hamsini za cobra
 
Kuna documentary moja ninayo mwanzo mtangazajia anasema kama ukikutana na huyu nyoka usithubutu kufanya chochote hatari sana
Hiyo documentary haisemi ukweli au hukuielewa vizuri. Nakushauri ingia sasa kwenye search engines kama Google utapata Taarifa sahihi
 
Nyoka huyu anapatikana katika hali za hewa nyingi nusu jamgwa yupo, ikweta kwenye mvua nyingi yupo na maeneo yenye joto kama Namibia pia anapatikana. Kuhusu kinyesi cha Ng'ombe sinauhakika sana lakini kuna kesi nyingi tu za nyoka huyu kuuwa Ng'ombe wengi tu huko Shinyanga
Asante kwa Tanzania ninewaona Chunya, Mpanda, Tabora na Handeni Tanga ila Handeni wengi ni Green mambas ambao hupenda sana kukaa kwenye miti hafu ni wapole inapita wako juu ya mti hata wametulia tu, kwa Mpanda wana rangi ya kijivu ni wakali balaa.
Hafu huwa wanasema kuwa Black mambas akitaga mayai huweka zone ambapo ukipita ndani ya hiyo zone lazima akushambulie je ni kweli?
 
Hahahahahhhaha Kila Mtemi ana mtemi wake kumbe, kwahio na speed zake zooote ila kwa hao jamaa hachomoi
 
Pamoja na kusimulia kwa mtiririko unaofaa, lakini wajua kuwa umeharibu sana!!!
1. Unajua kweli maana ya "KITOWEO"
2. Unaposema "kwa kiingereza anaitwa black mamba" sisi kwa kiswahili tunamwita "koboko" sasa imekuaje umeandika nnsha yako kwa kiswahili na umelionea aibu jina "KOBOKO"?


Mwisho nikuulize huyu ndiye hugonga kichwani pekee? Kama siye basi hujamsimulia aliye hatari kuwazidi wote.
 
mimi shambani kwangu kuna hao nguchiro wengi sana hua wanatembea kikundi sijui kuna hao nyoka mita hiyo mpaka naogopaga na hao nguchiro hachezi mbali du kwahiyo ni walinzi wazuri kwa nyoka kumbe safi sana
 
Pamoja na kusimulia kwa mtiririko unaofaa, lakini wajua kuwa umeharibu sana!!!
1. Unajua kweli maana ya "KITOWEO"
2. Unaposema "kwa kiingereza anaitwa black mamba" sisi kwa kiswahili tunamwita "koboko" sasa imekuaje umeandika nnsha yako kwa kiswahili na umelionea aibu jina "KOBOKO"?


Mwisho nikuulize huyu ndiye hugonga kichwani pekee? Kama siye basi hujamsimulia aliye hatari kuwazidi wote.

Kitoweo imewekwa kunogesha mkuu
 
Back
Top Bottom