Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Mama Mdogo siji KATAVI Ng'oooo Niliwahi kusikia kuna mchoma mkaa mmoja aling'atwa na huyu nyoka huko huko kwenu akafa mara moja
 
Last edited by a moderator:

Hapo kwenhye red ndio nimezidi kuogopa
 
Mambas (kama ilivyo kwa nyoka wengine) hawasikii....hawana masikio kabisa....wanategemea sana mitikisiko (vibration) kujua movements....

Black mamba sio nyoka mweusi...nadhani rangi yake ni kijivu....black inatokana na weusi mdomoni...
 

Maelezo haya yanakosa maana kama husemi jinsi ya kuwatoutisha!!!!
Walau first aid!!!!
 
Pia ana uwezo wa kusimama kwa kutumia mkia wake, anaweza kupanda mti Kwa kujinyoosha kwenda juu had kufikia tawi lililo karibu, yan inabaki sehem ndogo tu inayobeba mwili wake kabla hajafkia tawi analotaka kupanda.
 

Mkuu we ndo unamfahamu vyema huyu nyoka maana umepita mulemule.

Hapo kwenye kuwika huwa ni usiku wa manane zaidi(hii ni kwa uzoefu wangu)
 

Nawafahamu isale, wale siyo mambaz!! Isale tulikuwa tunawachezea sana enzi zetu kwenye mikungu na michongoma ya fensi. Nae akikasirika anakimbiza sana ila si mambaz
 
Mkuu we ndo unamfahamu vyema huyu nyoka maana umepita mulemule.

Hapo kwenye kuwika huwa ni usiku wa manane zaidi(hii ni kwa uzoefu wangu)

aki komaa zaidi anakuwa na ukucha kwenye mkia.
pia akikomaa zaidi magamba yake huwa yanatoa sauti akikimbia kwa sauti inakuwa kama chupa inayovunjika na pia ana uwezo wa kukaa kwenye paa la nyumba nje juu ya mlango kwa muda mrefu mpaka m2 amuone basi huyo atagongwa au itakuwa ni balaa lakini si kila mara
 

Hii inafaa Facebook huku ni 18+
 
Mama Mdogo siji KATAVI Ng'oooo Niliwahi kusikia kuna mchoma mkaa mmoja aling'atwa na huyu nyoka huko huko kwenu akafa mara moja

Usiogope njoo tu, black mamba ni mpole sana na hapendi mapambano kama utamwacha aende zake kwa amani, ila ukiamua kumkabili, ni lazima ujizatiti kwani mmoja lazima afe (wewe au nyoka), na mara kwa mara wa kufa ni mtu. Formula ya huku kwetu ni kuwa, kama mko chini ya idadi ya watu sita wenye afya timamu, na walio na fimbo na mawe, musithubutu kumchokoza, atawaua tu, angalau mkiwa wengi mwaweza kumchanganya akili akakosa malengo!!

 

daah kumbe ni hatar kias hicho kuna siku nikiwa dodoma napga story chin ya mti wa maembe na washkaj Huyo nyoka akawa amedondoka kwny kiatu chang kutoka mtin mm sina habar nmekuja kushtuka washkaj wameshakimbia ila na yy mwnyw alikimbilia kwny majan,ni wa kijani kama majan ya mti afu mref hv,ila washkaj walinambia huwa hang'ati
 

huyu sio nyoka ni SHING'WENG'WE
 
Huyu nyoka ni hatari, nimekutana naye Moro katika njia niliyoizoea wiki 2 zilizopita, nadhani aliposikia hatua zangu alitulia na kunipisha, lakini nilipomuona ilibidi nirudi na kutafuta njia nyingine. Ukubwa wake na ule weusi vilinitisha kupambana naye. Tangu siku hiyo sijapita njia hiyo.
 

inatisha kutulia tuliiii yataka ujasiri wa hali ya juu lazima upanick
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…