Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Kingine kuhusu KOBOKO,

Ni mojawapo ya nyoka wenye kumbukumbu sana na wepesi wa kulipa visasi.

Ukiona umemjeruhi alafu hukumuua.

Basi jiandae kwa revenge, wakati wowote akishatia timu.

Mf:
Kuna jamaa kule Tabora alimkuta KOBOKO jikoni kwake alkokua anawalaza kuku wake usiku.

Basi jamaa akakuta kuku 5 wamekufa.

Basi akafanya msako, akamlia ambush,akamjeruhi kwa kwanja mkiani (alimkata mkia)

Basi KOBOKO alipozidiwa akatokomea vichakani.

Jamaa akabaki na mkia wa KOBOKO.


Baada ya Muda yule koboko aliota mkia mwingine mpya
( kama kawaida yao Reptiles)

Yule koboko baada ya miezi 3, Yule koboko alirudi pale nyumbani kwa jamaa

Alienda zizini akawagonga ngombe wawili.

Kuna mbwa alkua analinda pale nyumban, nae asbuh walkuta anatoa damu machoni kalala chini hoi bin taabani.

Baada ya mda nae akafariki.

Usiku ule ule kumbe alikua keshamfata jamaa kitandan, na kumgonga mguuni.

Asbuh,
jamaa anaamshwa aone kilichowapata mbwa wake na ngombe.

Wanastuka MTU haamki, Kuangalia wanaona jeraha LA meno kwny mguu.

Na ngozi ya mwili wake ishabadilika kua blue black

PEMBENI
WANAONA GAMBA LOTE ALILOJICHUNA BLACK MAMBA MULE MULE CHUMBANI KWAKE.

Wananchi walighadhabika mno;

Msako wa wiki 2 ulifanyika kumsaka kila kona bila mafanikio.

Tulizuiwa mpaka kumwongelea, yaani ukimtaja tu unakula viboko/makofi

Msalani; ikifika usiku MTU anasindikizwa na watu 3-4 wenye silaha.

Dah,
nkikumbuka lile tukio mwili unanisisimka.

NAJIKUTA NAMWOGOPA SANA HUYU NYOKA.
 
Hii hatari. Tuwekee picha mkuu!
 
Nimewahi kuwaua swira kadhaa wakubwa kwa wadogo, wana purukushani lakini hawana mbio. Sikujua kama hao ni cobra kwasababu hawapanui shingo zao.

Nilimfahamu cobra pale nilipomtoa berenge akainua kichwa na kupanua shingo, akawa ananirushia mate tu huku anahema kama mbwa, mbio hana sijui ni kwababu ya ukubwa?

Nilikuwa nimetoka town nimeenda bush kwa bibi ndo siku hiyo kukutana na vita hiyo. Mama mmoja jirani analia na kutaka kulivagaa ovyo jamaa limemvamia siku nne, kila siku jioni linazama na kulala ndani halafu linakoroma kama father house. Siku hiyo wanakijiji walikuwa wanatimua mbio tu. Nilikimbizana nalo migombani, hadi kuliua ilikuwa ni kazoezi aisee, wanakijiji walijaa kutoa pongezi zao. Tangy siku hiyo huwa siwaogopi cobra.
 
Nyegere anatafuta black mamba sijui koboko na aina yeyote ya nyoka,Nyoka ndio wanamkibia..
 
Huyo nyoka ni mpole sanaa mpaka umchokoze na mara nyingi hua anatembea uck tu na hata akipita kwenye mchanga hua unakta ameacha alama iliyonyooka tofaut na nyoka wengine lazima wajikunjekunje
 
Chura kajivimbisha na anamwambia Koboko "haliwi mtu hapa"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…