Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Naomba mtuwekee picha ya Koboko na Kifutu na majina yao kwa kiingereza maana wengine mmetuacha Ubungo Mataa.
Koboko= black mamba

Kifutu= puff adder/ death adder

Si ndio imhotep?

Cc. imhotep
 
Watu wengi hujidanganya kuwa huyu nyoka huwa hana sumu,lakini sio kweli huyu nyoka Boomslang ana sumu kali lakini yenye kuua polepole.kama akikun'ata asubuhi hutosikia dalili zozote mpaka usiku ndio ukilala huamki.View attachment 767836
Mkuu Boomslang hana sumu/haui. Huyu amefanana na Green Mamba lakini ngozi yake ina madoa doa meusi mgongoni, hana sumu.
 
Huyu green bush Snake ndio hana sumu ila watu wanagongwa na Boomslang kwa sababu wanafikiria ni huyu.
 
The boomslang is a large, venomous snake in the family Colubridae
 
Black mamba anakawaida ya kutoa tahadhari pindi pindi anapotambua umemuona kwa kutoa mlio mkali na huku akiachama mdomo wake mweusi kwa ndani, ukijifanya kupambana naye ndipo hapo utaona kizaa zaa, kuna wazungu kipindi fulana huwa wanakamata Wa kila aina akiwemo huyo black mamba katika channel ya nat geo wild huwa wanawaelezea sana tabia ya huyu nyoka mpaka aone unataka kupambana naye ndio na yeye anajibu mashambulizi
 
N a unaona tahadhari wanazochukua wale wazungu wakamata nyoka wa south mara wanapogundua nyoka wanaetaka kumkamata ni black mamba?
 
Kwni mchanga ukimwagia anapata madhara gani mkuu kwamba mchanga ndo siraha inayomdhuru sana au siajaelewa kiongozi
 
Kuna warden.mmoja huko kruger aligongwa na Koboko kwenye paja hakujua kama kagongwa mpaka alipomuona koboko ndio akakimbila gali lake akaendesha kwa kasi mpaka barbara kuu akashuka akakimbila barabarani kuomba msaada alikuwa na bahati Koboko yule alikuwa mdogo sana kwa hiyo baada ya kukaa wiki hospitali ICU akapona.
 
Mkuu Boomslang hana sumu/haui. Huyu amefanana na Green Mamba lakini ngozi yake ina madoa doa meusi mgongoni, hana sumu.
Boomslang Ana sumu kali sana mkuu na yupo kwenye top ya nyoka wabaya
Wamejaa sana Botswana na kwa miaka 57 wameuwa watu 7 tu kwa takwimu zetu sijui ila huyu nyoka sio mkorofi wala havizii watu anahangaika na maisha yake tu
 
Hao jamaa ni hatari sana, lakini kuna watu wanawakamata kama kuku, hata akiingia ndani ya shimo wanachimba na kumtoa
 
Ukisoma hiyo article utagundua kua huyo mwanafunzi kama angesema mapema pengine asingepoteza maisha kwani angelipata tiba mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…