Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani


Angalia hiyo video halafu jifunze kufanya utafiti kwanza kabla ya kuanza ubishi.

Hapo presenter anasema mongoose anamwonya black mamba asije kwenye himaya yake na meseji imemfikia .
angalia video nyingi utakuta mongoose Ana win
 
Khaa!! Yaani ndo Koboko mwenyewe huyu?! Mi nilidhani ni lijijoka flani hivi linatisha ile mbaya!

Oh Lord!! Yaani hivi alivyo alivyo kama ndo ningekutana nae hivi am sure ningemchukulia poa sana... wallah kama ndo angenitisha hivi halafu akaamua kusepa zake, huenda ningemtafutia bakora ili nikamtandike nayo kichwani... manake nasikia ukitaka kumuua nyoka kirahisi; basi mtandike kichwani!!

Kwahiyo wadau mnasema ningejifanya kumdindia ingekuwa ni sawa na kudandia mabasi ya BRT yanayoelekea kuzimu?!

Halafu hiyo kutomtaja jina ndo kwamba ukimtaja tu, Mwana anaweza kuwaibukia; au?!
Bora ukutane na wasiojulikana kuliko huyu kwanza yeye good morning wala good afternoon hajui yeye ni goodbye tu
Katika ulimwengu wa nyoka huyu anaongoza
Ana mbio za kasi na akikuwa anafika mpaka 14ft kwa urefu na kuuwa yeye ni kama alshabab vile
Akiamka asubuhi anapanda mti kutafuta afungue hicho kinywa wapi
Kuna kundi la Nyati wakiwa malishoni alitokea huyu jamaa yaani kuwaonesha tu kinywa chake kilichofanana na jeneza yaani hao Nyati walitoka mbio za ajabu na wengine kupamiana hovyo na kusababisha na mpaka faru kukimbia
Najiuliza kumbe hata wanyama wanajua jeneza ni kuzimu
 
Hapa kamkuta Simba kafa lakini alivyo na roho mbaya anaamua kung'ata tena sio Mara 1 bali mara 2
20180506_163806.jpeg
20180506_163701.jpeg
 
Kuna kitu ambacho nimekiona sana katika fuatilia yangu kuhusu huyu jamaa wazungu huwa kwa kiasi fulani huwa wanapotosha.nadhani kwa sababu huyu mnyama waafrika huwa wanamhusudu sana.
 
Ni balaa hicho kifaa kinaweza kuua watu mia in 5min acha tu,huku kwetu ushirombo ndo vipo,kuna siku nimekutana nacho kinavuka barabara ya vumbi,nikasimama nikarudi nyuma na corola yangu nikakipitia shaaaaaah kumbe sikukigonga kikanasa chini ya gari,bahati nzuri nilikua naenda mwendo mrefu,kufika lami nikaona kitu kimeanguka kwa nyuma dah nikashukuru sana,nikawaza ni vp ninheenda nacho home?
Aisee usije thubutu tena kujaribu kumgonga huwa wanarukia gari unaenda nae utakaposhuka anawewe.ukienda mbugani mfano serengeti unaambiwa kabisa.
 
Kuna kitu ambacho nimekiona sana katika fuatilia yangu kuhusu huyu jamaa wazungu huwa kwa kiasi fulani huwa wanapotosha.nadhani kwa sababu huyu mnyama waafrika huwa wanamhusudu sana.
Labda inawezekana maana kuna jamaa walikuwa ni wakata magogo mambas walikuwa wanaishi maeneo hayo hayo tena wengi tu ila walikuwa wanaishi kwa amani tu kila mmoja na hamsini zake
Nilikuwa nawajua hao jamaa kwa ukaribu sana na kazi zao ila walikuwa hawajali kabisa wanalala na kuamka porini ambapo wanaonana kila siku
Yaani story zinachanganya ingawa ni mkorofi
 
Duh!! Kumbe nilikuwa simfahamu hata kidogo huyu mwamba!!

Huyu jamaa ndo yule anaitwa Cobra au ni jomba wawili tofauti?!
Hapana Cobra ni Swila yule anatanua shingo na kutema mate
Ila huyu ni tofauti yeye hatemi mate ila ana sumu mbaya sana ambayo inauwa kwa dkk 30 tu kama hawajakuwahi
 
Kina mfipa 1 tabora anawaua sana na ni bwana mdogo tu, tulipokuwa wadogo niliwahi sikia story kuwa kama ukitaka muua nyoka mwanamke ashike matiti na mwanaume ashike magoti mwingine awe anampiga nyoka anakuwa hakimbii, anabiringita hapo hapo, niliwahi iona hii ukerewe nikiwa nalima na bibi na kweli nilimuua kifutu huku bibi akiwa ameshika matiti, huwa mpaka leo najiuliza wanaposhika hivyo kuna logic yoyote na inafanya kazi
Unasema kweli
Halafu na jaribio umelifanya kabisaaa
Sasa itabidi tuwe na wanawake kila tunapoenda kuwinda au shambani ukiona tu koboko shikaaaa
 
Duh!! Kumbe nilikuwa simfahamu hata kidogo huyu mwamba!!

Huyu jamaa ndo yule anaitwa Cobra au ni jomba wawili tofauti?!
Ni tofauti na Cobra ila sifa zao kama zinafanana ila huyu ni hatari sana...Cobra hawapatikani kivile nchi za Africa
 
Hiyo kitu, sumu yake Iko kama mafuta ya taa. Akikugonga , sumu inasambaa sehemu kubwa. Huyo, wenfine humwita Black Mamba. Anatofautiana kidogo sana na rattle snake.
 
Hapana Cobra ni Swila yule anatanua shingo na kutema mate
Ila huyu ni tofauti yeye hatemi mate ila ana sumu mbaya sana ambayo inauwa kwa dkk 30 tu kama hawajakuwahi
Dah!! Basi miaka yote hii nilikuwa nadhani Koboko ndo Cobra... halafu nakumbuka enzi hizo tulikuwa tunamuita Koboko Mate... kumbe tulikuwa tunalishana matango pori!
 
Dah!! Basi miaka yote hii nilikuwa nadhani Koboko ndo Cobra... halafu nakumbuka enzi hizo tulikuwa tunamuita Koboko Mate... kumbe tulikuwa tunalishana matango pori!
Hahahahaha Walahi nimecheka sana eti koboko mate
But it make sense in a way kwa sababu wote ni wabaya
 
Back
Top Bottom