prince dudu
Senior Member
- May 24, 2015
- 109
- 76
Hapana kifutu ni mwengine TenaHivi koboko ndio anaitwa kifutu kwa jina lingine?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana kifutu ni mwengine TenaHivi koboko ndio anaitwa kifutu kwa jina lingine?
Alimgonga mjomba wangu mpaka leo mkono ni mlemavu alitumwa jikoni kumbe jamaa alifuata joto hakuvunga alipogonga akatoka kuelekea zizi la ng'ombe akajikunyata hapo tukamuua. Nadhani huwa wanachoka sana wanapong'ata vifutu huwa hawaendi mbali.Puff adder bite View attachment 767365
Hahahah,,,eti mdomo wake upo kama jenezaBora ukutane na wasiojulikana kuliko huyu kwanza yeye good morning wala good afternoon hajui yeye ni goodbye tu
Katika ulimwengu wa nyoka huyu anaongoza
Ana mbio za kasi na akikuwa anafika mpaka 14ft kwa urefu na kuuwa yeye ni kama alshabab vile
Akiamka asubuhi anapanda mti kutafuta afungue hicho kinywa wapi
Kuna kundi la Nyati wakiwa malishoni alitokea huyu jamaa yaani kuwaonesha tu kinywa chake kilichofanana na jeneza yaani hao Nyati walitoka mbio za ajabu na wengine kupamiana hovyo na kusababisha na mpaka faru kukimbia
Najiuliza kumbe hata wanyama wanajua jeneza ni kuzimu
Mkuu nimekupata vyema,Tatizo wengi humu ni wanaume wa Dar wanaogopa hata mende
Labda niwafundishe tu kitu kimoja,
Nyoka ukitaka kumuua mpige sehemu yoyote ile hata mkiani, yaani ukishampiga tu ataanza kujibiringisha sababu ya maumivu,
Na hapo ndo unapopaswa kuendeleza mashambulizi,
Huyu KOBOKO kwetu Tunamwita KISANGA na hata Wamasai wakisikia tu hilo jina basi wataanzisha harakati za kumuwinda, wasipomuua ndani ya siku mbili au tatu basi lazima wahame,
Na hao mnaowaita KIFUTU si kwetu tunawaita MOMA hawa bwana kuwakuta ndani ya Nyumba yako ni kitu cha kawaida haswa majira ya Kiangazi, utakuta ukifungua mlango tu ili uingie ndani kama ni usiku au mchana lazima akukaribishe ndani, utasia FOOOOOO, Hapo unajua ndani kuna ugeni, ili kujua eneo alipo wee utaendelea kufuata hiyo sauti maana akihisi unamkaribia na yeye anazidi kufoka, hivyo hapo kuna mawili,
Umtimue atoke nje (kwa kuchoma Chumvi ya mawe kwenye moto) au umuue
Ila ukweli hawa KOBOKO ni hatari sana maana siku hiyo nakumbuka nilikuwa napita tuu njiani nikakutana nae na yeye alikuwa anavuka kuniona badala ya kuendelea na safari yake akasimama yaani kaziba njia kabisa hakuna kupita, nikaagiza ikabidi nimwambie dogo lete Fimbo
Kuna mwingine alikuwa anakuja kuuza dawa za nyoka ye alikuwa anakuja na KOBOKO
Katika NYOKA wote aliokuwa nao huyo ndo alikuwa hamtoi ovyo maana nakumbuka kuna siku ile kumtoa tu akaanza kutoka nduki kilichosaidia aliwahi kumdaka,huyu jamaa watu tulimnyooshea mikono, maana hatujui yule mdudu kamkamata vipi na kamtoaje sumu maana mziki wake sio wa kitoto
Kweli msomi wanguHahahah,,,eti mdomo wake upo kama jeneza
Kwa hiyo hapo umewaweka wanaume wa Dar hawawezi kitu lakini umejisahau ukawaponda tena wamasai kwa kusema wasipomuona siku ya tatu wanahama.Tatizo wengi humu ni wanaume wa Dar wanaogopa hata mende
Labda niwafundishe tu kitu kimoja,
Nyoka ukitaka kumuua mpige sehemu yoyote ile hata mkiani, yaani ukishampiga tu ataanza kujibiringisha sababu ya maumivu,
Na hapo ndo unapopaswa kuendeleza mashambulizi,
Huyu KOBOKO kwetu Tunamwita KISANGA na hata Wamasai wakisikia tu hilo jina basi wataanzisha harakati za kumuwinda, wasipomuua ndani ya siku mbili au tatu basi lazima wahame,
Na hao mnaowaita KIFUTU si kwetu tunawaita MOMA hawa bwana kuwakuta ndani ya Nyumba yako ni kitu cha kawaida haswa majira ya Kiangazi, utakuta ukifungua mlango tu ili uingie ndani kama ni usiku au mchana lazima akukaribishe ndani, utasia FOOOOOO, Hapo unajua ndani kuna ugeni, ili kujua eneo alipo wee utaendelea kufuata hiyo sauti maana akihisi unamkaribia na yeye anazidi kufoka, hivyo hapo kuna mawili,
Umtimue atoke nje (kwa kuchoma Chumvi ya mawe kwenye moto) au umuue
Ila ukweli hawa KOBOKO ni hatari sana maana siku hiyo nakumbuka nilikuwa napita tuu njiani nikakutana nae na yeye alikuwa anavuka kuniona badala ya kuendelea na safari yake akasimama yaani kaziba njia kabisa hakuna kupita, nikaagiza ikabidi nimwambie dogo lete Fimbo
Kuna mwingine alikuwa anakuja kuuza dawa za nyoka ye alikuwa anakuja na KOBOKO
Katika NYOKA wote aliokuwa nao huyo ndo alikuwa hamtoi ovyo maana nakumbuka kuna siku ile kumtoa tu akaanza kutoka nduki kilichosaidia aliwahi kumdaka,huyu jamaa watu tulimnyooshea mikono, maana hatujui yule mdudu kamkamata vipi na kamtoaje sumu maana mziki wake sio wa kitoto
Wamasai hawaami kuogopa Nyoka, ila wanahama kunusuru mifugo yake, kumbuka mifugo ndo kinachosababisha masai kuishi porini na ndio utajiri wake,Kwa hiyo hapo umewaweka wanaume wa Dar hawawezi kitu lakini umejisahau ukawaponda tena wamasai kwa kusema wasipomuona siku ya tatu wanahama.
Kwa hiyo hao wamasai ndio waliohamia Dar ama?
Nyoka hakuambii njoo tuzipige mkuu bali anakuvizia sasa hapo unatembea kichakani unategemea akuambie oyaa unataka tuliamsheee
Ooh nimekuelewa vizuriWamasai hawaami kuogopa Nyoka, ila wanahama kunusuru mifugo yake, kumbuka mifugo ndo kinachosababisha masai kuishi porini na ndio utajiri wake,
Masai yupo tayari kuua mtu ili Mifugo yake iwe salama,
Kwa hiyo sijawaponda ila nmeandika uhalisia
Huyu hayawani akisha zeeka hua ana roho mbaya sijapata kuona,Kuna kisa kimoja cha mzungu na koboko huko Botswana ninakitafuta ilinikthibitishe halafu nikilete hapa.

Samahani sijui ushaangalia kipindi cha snakes in the city ? Nat Geo ?Nyoka wengi hua wana aibu na huwa wa kwanza kuretreat unless wawe cornered, koboko hajui kuretreat, ana accuracy, speed na bado yeye ndiyo ataanzisha ugomvi.
Iwe iwavyo ninachojua hachomoki mbele ya honey badger.
Samahani sijui ushaangalia kipindi cha snakes in the city ? Nat Geo ?
Mbona yule jamaa huwa anawashika black mamba kirahisi tu hata awe aggressive au wounded ?
Mnaposema Mamba huwa yeye anaanzisha tu vita vyovyote vile napata wakati mgumu kuwaelewa
We jamaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23]Ila Koboko mwenye hasira akikubananiza, ukimuimbia ule wimbo Sina makosa wa Les Wanyika anakuacha.
Naam! mzungu anakiri mwenyewe kuwa Koboko huyo alikuwa amekomaa.I realised it was a snake - and a huge one
Jasho huwa linamtoka na yeye mwenyewe anakiri kuwa huwa anacheza na kifo.Anashika mamba wadogo mno tena kwa umakini sana
Mmmmh ... Sasa upite na chungu cha moto, akikugonga kwenye bega je?Huyu hayawani akisha zeeka hua ana roho mbaya sijapata kuona,
wakati mwingine hua anasikia raha tu jinsi anavyowapa wenzie busu la kifo.
Kwetu kolomije huwa wanakawaida ya kuning'inia juu ya mti kwenye njia wanayopita watu, ukijichanganya ukakatiza sehemu alipo basi ni lazima akupe busu la kichwa na hio ndio inakua safari yako ya kuelekea kuzimu moja kwa moja,
Ikishatokea hivyo wazee wetu hua nao hawakubali lazima tulale nae mbele kwa mbele,
Utapikwa uji halafu unawekwa kwenye chungu na kuachwa kama dakika 5 hivi ili ile layer ya juu ya uji igande isiweze kupandisha mvuke wa moto juu, baada ya hapo anachaguliwa kijana mmoja anajitwishwa chungu cha uji na kukatisha eneo hilohilo alipong'atwa mwenzetu,koboko na roho mbaya yake atagonga ndani ya chungu na hio inakua ni zamu yake na yeye kupigwa busu na uji wa moto, taratibu anajiachia wenyewe kutoka kwenye mti na kuanza kuogelea kwenye swimming pool ya uji wa moto na huo ndio unakua mwisho wake, bila yakumuua hapo anaweza akawagonga hata watu 10 eneo hilohilo.
Yaani sisi wasukuma pamoja na kua ndio kabila maarufu lenye utamaduni wa kufuga na kuchezea nyoka ktk ukanda wote wa afrika mashariki lakini kwa huyu kiumbe anaeitwa black mamba hatutaki kabisaaaa mazoea nae.