Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko aliwakurupusha Ngamia huko kaskazini mwa Kwenya na akakutwa anakunywa maji ambayo walikuwa wamewekewa Ngamia.
 
Ni balaa hicho kifaa kinaweza kuua watu mia in 5min acha tu,huku kwetu ushirombo ndo vipo,kuna siku nimekutana nacho kinavuka barabara ya vumbi,nikasimama nikarudi nyuma na corola yangu nikakipitia shaaaaaah kumbe sikukigonga kikanasa chini ya gari,bahati nzuri nilikua naenda mwendo mrefu,kufika lami nikaona kitu kimeanguka kwa nyuma dah nikashukuru sana,nikawaza ni vp ninheenda nacho home?
Ndio zao hizo, hapo alikuwa katulia anakusubirisha tu uweke mguu chini uone cha moto.
Bahati yako nzuri alianguka
 
Ushauri wangu ni kosa kubwa kumsogelea Koboko kwa ukaribu kama huu huyu anauwezo wa kukurukia
5640453710_ce466d8119_b.jpg
 
Angalia Video hii kwa umakini uone Koboko mdogo alivyomkosa mpanda Baiskeli, huyu nyoka ni hatari sana.
 
Chochote kifananacho na Nguchiro lazima kigongwe, kwa bahati mbaya huyu Sungura
na ujanja wake wote alikutana na mbabe wake.
Black_Mamba-1-1.jpg
 
Yeah, wewe unamjua, watu wanachanganya na black mamba sijui kobra, tofauti kabisa, huyu jamaa kwanza hana rangi nyeusi, ni mweupe fulani hivi, ana singa kichwani na akitoa mlio unaweza fikiri ni jogoo, anasafiri kama helcopta, ana shabaha, ana lenga kichwani tu, akikugonga dakika tano nyingi tuna zika, tumewaua wengi kijijini, mkigundua sehemu kuna koboko, tulikuwa tunajitwisha uji wa moto kwenye sufuria, akikuona lazima akurukie kichwani, anajizamishwa kwenye uji wa moto anakufa.
Kweli...

Kile kichwani ni kama kile cha jogoo..na anatoa sauti kama jogoo akiwika..hagongi sehemu ingine zaidi ya kichwani..na ana uwezo mkubwa wa kuruka sehemu kubwa sana
 
Koboko ana hasira sana ukikutana nae ni kutambika kikwenu au sala ya mwisho.
Usithubutu kukimbia kwani ana mbio za ajabu na kama kuna matuta ukajifanya kuyaruka yeye anatambaa juu ya matuta umenielewa
Ukiwa na gari ukamuona barabarani ataifukukuza gari na kuingia kwa chini na kujificha mpaka kwako
Hasira za kurushwa akitoka hapo ana uwezo wa kuuwa watu 25 kwa mkupuo na sumu yake huvuki dakika 30 ulimi nje.

Nawapenda nyoka lakini huyu sio rafiki kabisa very aggressive
Duuh,yani sijawahi ona nyoka anamkimbiza mtu akampata..basi huyu ni noma
 
Mnaofahamu mambo ya wanyamapori naomba mnijuze hivi ni kweli koboko huwa anawika kama jogoo?
 
Kinachomtofautisha Koboko na nyoka wengine ni umakini wake katika mauaji.
b3500adfaab54944afe658a523539d10--baby-snakes-black-mamba.jpg
 
Duuh,yani sijawahi ona nyoka anamkimbiza mtu akampata..basi huyu ni noma
Binadamu wa kawaida anaweza kukimbia maili15 kwa saa na wengine mpaka wanaojitahidi kama mimi 20 maili kwa saa
Na koboko anakimbia mile 12 kwa saa
Sasa wewe unakimbizwa na woga huo utajikwaa mara ngapi na kuamka, kuna wengine wakikimbizwa badala ya kukimbia na miguu anaongeza na mikono halafu ndio haendi popote (hapo anatambaa kwa mshtuko)
Koboko anakimbia aisee na usipande mti ana wewe
 
Back
Top Bottom