Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Huyu nyoka ni hatari, nimekutana naye Moro katika njia niliyoizoea wiki 2 zilizopita, nadhani aliposikia hatua zangu alitulia na kunipisha, lakini nilipomuona ilibidi nirudi na kutafuta njia nyingine. Ukubwa wake na ule weusi vilinitisha kupambana naye. Tangu siku hiyo sijapita njia hiyo.

alivyotulia nadhani anasikilizia je utaleta ukorofi na ungeamua kupambana nae peke yako usingeweza nyoka ni hatari sana
 
Kuna nyoka wapo juu ya safu za milima ya Uluguru, akihema tu ni sumu, unakufa kwa kuvuta hewa yake,
 
MAMBAS ni aina ya nyoka wakali wapatikanao ktk dunia ya leo.
Ni nyoka wenye sumu kali na wenye kasi ktk mwendo na wana sifa ya kutaga mayai (oviparous).
Kuna aina mbili za mambas :
1>GREEN MAMBAS.
2>BLACK MAMBAS.
Green mamba wanasumu aina ya NEUROTOXIC na HAEMOTOXIC.
Wanaishi miaka 12 hadi 14 (makadirio kulingana na takwimu za sayansi) wanataga mayai na kuanguliwa kwa siku 80 hadi 90.
BLACK MAMBA pia wanauwezo wa kupanda miti wakati wakitafuta chalula na wanaurefu kati ya sentimita 220 hadi 320.
Ni kati ya nyoka wenye sumu kali wapatikanao Afrika.
Wanataga mayai kati ya 12 na 18,na kuangua kati ya siku 80 hadi tisini.
Mambas ni nyoka wakali na wenye kung'ata zaidi ya mara moja kwa sababu meno yao hayang'ooki wakti wakigonga kitu.
Meno yanayong'ooka kwa nyoka yanaitwa FRONT FANGED MOVABLE na yasiyong'ooka yanaitwa FRONT FANGED FIXED.
Iwapo nyoka huwa wata kung'ata utaweza kuishi kati dakika 20.
(kama unafahamu mengine kuhusu nyoka unaweza kutuhabarisha zaidi)
maoni/ushauri: iddyallyninga@Gmail.com

Kwa kirangi ndio wanaitwa nini vile NKOBOKO au SATO.
 
Mmmmhhh aiseee hawa nyoka wanapatikana wapi hasa kwa hapa tz,makazi yao wanaopenda maana ni zaidi ya hatari,tiba ya haraka ya bite?

Vipo vingi tu vinapenda sana tumilio twa simu vimijusi tundege, kukuuma lazima uwe wenye "very close range"
Kana uwezo wa "ku-jump and vault" a bit like flying in the air

Hivi vimamba vinapenda sana kukaa kwenye miti ya mikwaju ya kizungu.

Taya za chini za nyoka zimegawanyika sehemu mbili, yaani kipande cha kushoto na cha kulia, hii inamfanya nyoka aweze kumeza kitu kikubwa zaidi ya ukubwa wa kichwa chake.

Nyoka anauwezo wa kugundua ongezeko dogo sana la joto la binadamu chini ya 0.01 kipimo cha sentigredi ndani ya mita kama kumi hivi.
 
Nawafahamu isale, wale siyo mambaz!! Isale tulikuwa tunawachezea sana enzi zetu kwenye mikungu na michongoma ya fensi. Nae akikasirika anakimbiza sana ila si mambaz
yule ni green mamba ule mweusi ni black mamba,hakuna nyoka mwingine wa kijani zaidi ya isale.
 
mkuu sina uhakika sana upole wa hao green mamba, may be green mambas wa musoma na moshi ni tofauti kidogo na hawa walioko uelekeo wa mtr, lindi na msumbiji, ninamaanisha hawa walioko huku ni wakali sana na wakubwa, wanaweza hata kukukimbiza, naomba maelekezo zaidi kutoka kwa mtoa mada
kweli inawezekana kukawa kuna utofauti,ntajaribu kulifuatilia zaidi!
 
nimwepes sana hakawii kukaa chiniya gari mkaenda nae hadi mwisho wa safari kasheshe atakae anza kushuka!
Ni kweli mkuu niliwahi ona documentary moja jamaa alitend kumkanyaga akajiingiza kwenye sehemu ya chini ya gari
kesho yake mwenye gari alipofungua boneti ya gari akangatwa.
 
yule ni green mamba ule mweusi ni black mamba,hakuna nyoka mwingine wa kijani zaidi ya isale.

Isale ni wadogo mno then wapole sana. Isale wana midomo myekundu while mambaz ni myeusi tii.

Wale isale urefu wao haufiki futi tatu, mambaz ni sita hadi tisa kutegemea na umri bro.

Isale hawezi kusimamia mkia ila ni kuning'inia kwenye miti anaweza. Mamba anasimamia mkia na anakuzidi urefu kiasi anakugonga kichwani akiwa ardhini. Upo brother??

Hujaona tofauti tu kaka??
 
mkuu usiombe kukutana nao, wapo wengi misitu ya sikonge kwenye vichuguu, ukikutana naye akiwa amesimama mbele yaki usijaribu ujanja wowote hutaweza kumwahi, labda umwombe Mungu akupe ujasiri wa kutulia tuli hadi ashushe kichwa chini ndio ujaribu ujanja mwingine otherwise WAFWA, akikuuma kichwani sijui utafunga wapi
Mkuu ujanja kwa nyoka sio huyo tu bali nyoka wote,ukitulia hakufanyi kitu sana sana atapunguza mukali na kushusha kichwa chake na kuondoka.Nyoka ana kibox karibu na ubongo wake kinaitwa ''jacobson'' hiki humsaidia pindi aonapo kitu uuelekeza ulimi wake wenye ncha mbili kuelekea kitu hicho kisha hugusisha kwenye kisanduku hicho,mara hupata taarifa kama hicho kitu kina madhara au la,sasa unapokutana na nyoka ukawaza kumdhuru anakutambua na hivyo huanza mbinu za kujihami ikiwemo hiyo ya kukurukia na kukuuma,ni vyema uwaonapo nyoka hawa usiwaze kuwadhuru ili ubakie salama.
 
Wakati flani huko Zimbabwe Black Mamba alikua amekaa barabarani , huku akiwa ameachama mdomo, mdomo ulioanzia upana kutoka upande mmoja wa barabara hadi upande wa pili , gari Land-rover 110 likiwa safarini lilipofika hapo alipo nyoka , dreva alidhani kafika kwenye Tunel (njia ya chini kwa chini)
Akailengesha gari domoni mwa nyoka !
Na ndy gari ikawa imemezwa na wasafiri wake wa 5 (watu) haijawahi patikana gari wala watu!
Mwaka wa 10 sasa!

Mkuu wewe unafaa kuwa mwanasiasa.
 
Aisee nimechek videos hao wadudu n hatari mpaka cobra wakubwa wanawagwaya...

Movie zao zinavutia Sana kuzitazama

Ni raha sana hata kenge anatumia stair hiyo hiyo mpak anamuua then anamla,ila paka sasa,,,ni mwendo wa kumpiga makofi na kumkwepa nyoka mpaka anachoka kabisa then anaburuza anakabithi watoto wake wachezee.hamli.

Nilishuhudia hii live miaka ya nyuma home nilishangaa sana nikaamini katika wanyama smart ni jamii ya paka yaan anaanza kama utani vile nyoka na ukali wake woote mfukoni.
 
Ni raha sana hata kenge anatumia stair hiyo hiyo mpak anamuua then anamla,ila paka sasa,,,ni mwendo wa kumpiga makofi na kumkwepa nyoka mpaka anachoka kabisa then anaburuza anakabithi watoto wake wachezee.hamli.

Nilishuhudia hii live miaka ya nyuma home nilishangaa sana nikaamini katika wanyama smart ni jamii ya paka yaan anaanza kama utani vile nyoka na ukali wake woote mfukoni.


Ha ha ha raha Sana mkuu

Hapa internet ya ofisi inalika kwa kuangalia hizo videos YouTube....
 
Back
Top Bottom