Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

daah kumbe ni hatar kias hicho kuna siku nikiwa dodoma napga story chin ya mti wa maembe na washkaj Huyo nyoka akawa amedondoka kwny kiatu chang kutoka mtin mm sina habar nmekuja kushtuka washkaj wameshakimbia ila na yy mwnyw alikimbilia kwny majan,ni wa kijani kama majan ya mti afu mref hv,ila washkaj walinambia huwa hang'ati

Huyo cyo black mamba
 
Koboko ni aina gani ya nyoka?nadhani ndiye nyoka hatari kuliko njoka wengine wote anaishi kwwnye vichaka vilivyotulia na misitu yenye giza.yuko kundi lipi?

koboko ni black mamba!
 
aki komaa zaidi anakuwa na ukucha kwenye mkia.
pia akikomaa zaidi magamba yake huwa yanatoa sauti akikimbia kwa sauti inakuwa kama chupa inayovunjika na pia ana uwezo wa kukaa kwenye paa la nyumba nje juu ya mlango kwa muda mrefu mpaka m2 amuone basi huyo atagongwa au itakuwa ni balaa lakini si kila mara

Kumbe huyo nyoka ndio black mamba nishawahi sikia habari zake,basi ni hatari sana.Ila huwa ninashangaa hiyo ya kuwika kama jogoo.
 
Black-Mamba-3.jpg
article-2073575-0F2AA9A000000578-547_634x383.jpg


Leo nataka tufahamishane kuhusu nyoka huyu hatari kwa sisi waswahili tunamuita KOBOKO lakini kwa lugha ya kiingereza huitwa Black Mambas

Black mamba ni moja ya nyoka hatari sana katika dunia. Nyoka hawa hupatikana katika sehemu Mashariki na Kusini mwa Afrika. Black mamba anaweza kuishi katika aina mbalimbali za mazingira: savanna, mabwawa, misitu na maeneo ya miamba.

Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu ni sehemu nzuri ya kuishi Black Mamba. Kutokana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa kilimo, makutano kati ya Black Mamba na binadamu yameongezeka zaidi.

1- Black mambas ni nyoka mwenye sifa ya urefu anaweza kufikia miguu 14 urefu na 1.58757 katika uzito.

2- Black mamba ana mwili mwembamba kufunikwa na ngozi yenye magamba kama ilivyo kwa nyoka wa jamii nyingine, Pamoja na wao kujulikana kwa kiingereza kama Black mambas lakini hawana rangi nyeusi katika ngozi na rangi ya mwili inategemea makazi yao na inaweza kuwa ya kijani, kijivu au njano.

3- Black mambas ni jina lake kwa sababu sehemu ya ndani ya vinywa vyao ni nyeusi kabisa. Black mamba kuonyesha kinywa chake cheusi wakati anakabiliwa na hatari.

4- Nyoka huyu huanza kutanua shingo yake lakini sio kama afanyavyo COBRA na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa inatoka upepo na hii ni ishara nyingine kwamba kiumbe hutayari shambulio.

Ukiona amena moja ya hizo ishara unashauri wa usifanye chochote kwasababu kwa kasi aliyonayo hutaweza kumuwai kifupi tulia mpaka hasira zishuke na ajiondokee narudia usithubutu kujifanya unafurukuta matendo yako hayatawahi tendo lake.

5- Ingawa nyoka huyu amebeba sifa ya kuwa nyoka mjeuri na mkali sana, lakini nayeye hujaribu kutoroka kabla mashambulizi lakini hushambulia kwa ukatiri sana ikibidi. Kumbuka kwa mtulivu ukikutana nae

[https://3]

6- Sasa upande wa sumu hapa ndipo patamu Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa Neuro – hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni Cardio-toxin hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake inaweza kuua.

7-Black mamba anatumia sumu kuwinda aina mbalimbali za ndege na wanyama wadogo. Na hutumia kama kitoweo chake

8- Black mamba anaishi katika mashimo ya miti na katika mashimo ya miamba. Pamoja na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, lakini hana ujanja mbele ya Nguchiro na Mbweha, na Nyegere.

9- Black mamba hutembea haraka sana akiwa juu ya ardhi. Anaweza kusafiri umbali mrefu kwa kasi ya maili hadi 12 kwa saa. Hivyo usijaribu kukimbia atakufukuza mpaka akugonge sehemu ya mwili wako.

10- Jike hutaga mayai kati ya 10 na 25 katika kiota juu ya ardhi. Joto ni muhimu kwa ajili ya incubation ya mayai. Na mayai hujitotoa baada ya miezi 3. Na vijinyoka hivyo vichanga huanza kujihudumia kwa kila kitu na huwa na sumu ile ile kama ya nyoka mkongwe hivyo usije ukadharau.

11- Black mamba anaweza kuishi hadi miaka 11 katika pori na hadi miaka 12 katika kama atafugwa.
 
Mkuu, bila utani, huyu nyoka hapendi kuishi sehemu walipo watu au wanyama wa kufugwa.

Sasa hiki kijiji chenu kinaonekana vipi? Kama vile nakiona kijiji chetu. Hapo kwetu Koboko Watoto wapo wengi ila Munu bariki hawauwi sana kama kwenu. Akishakuwa mkubwa anaanza kulia usiku "Kuwaiit, kuwaiit.....
"

Nyoka huyu kaua sana kijijini kwetu.
 
Mkuu, bila utani, huyu nyoka hapendi kuishi sehemu walipo watu au wanyama wa kufugwa.

Sasa hiki kijiji chenu kinaonekana vipi? Kama vile nakiona kijiji chetu. Hapo kwetu Koboko Watoto wapo wengi ila Munu bariki hawauwi sana kama kwenu. Akishakuwa mkubwa anaanza kulia usiku "Kuwaiit, kuwaiit.....
"

Mkuu km we ni mtu wa Sikonge basi ulizia Chabutwa , Ulyankulu na uyowa miaka ya 80.
Waliua sana hawa nyoka.

Wanakijiji wakimuona halafu wakashindwa kumuua basi Wafugaji lzm wanahame kijiji.
Siku hizi wamekuwa Wajanja kidogo.
 
Nini wafisu wa huyo mdudu?
Ana hatari gani?
 
Back
Top Bottom