Kuna sehemu nipo huku mkoani tabora sehemu nilikuwa nimekaa nikasikia watu wakimsimulia nyoka aina ya koboko ambaye inasemekana anapatikana tabora ,shinyanga,singida na kigoma.
Kuna mtu mmoja katika mazungumzo yake alikuwa akisema ni bora ukutane na simba au chui unaweza ukapona kuliko koboko nilipojaribu kumuuliza alisema hayupo tayali kumuongelea kiundani wala kumtajaa kwa sababu ukiwa ndani ya mkoa wa tabora au shinyanga ni marufuku kumtaja huyu nyoka jinsi alivyoniambia.
Sasa kwa wale wanaomfahamu hebu tuelezeeeni kwanini koboko anaogopeka kuliko simba au chuiii