Kingine kuhusu KOBOKO,
Ni mojawapo ya nyoka wenye kumbukumbu sana na wepesi wa kulipa visasi.
Ukiona umemjeruhi alafu hukumuua.
Basi jiandae kwa revenge, wakati wowote akishatia timu.
Mf:
Kuna jamaa kule Tabora alimkuta KOBOKO jikoni kwake alkokua anawalaza kuku wake usiku.
Basi jamaa akakuta kuku 5 wamekufa.
Basi akafanya msako, akamlia ambush,akamjeruhi kwa kwanja mkiani (alimkata mkia)
Basi KOBOKO alipozidiwa akatokomea vichakani.
Jamaa akabaki na mkia wa KOBOKO.
Baada ya Muda yule koboko aliota mkia mwingine mpya
( kama kawaida yao Reptiles)
Yule koboko baada ya miezi 3, Yule koboko alirudi pale nyumbani kwa jamaa
Alienda zizini akawagonga ngombe wawili.
Kuna mbwa alkua analinda pale nyumban, nae asbuh walkuta anatoa damu machoni kalala chini hoi bin taabani.
Baada ya mda nae akafariki.
Usiku ule ule kumbe alikua keshamfata jamaa kitandan, na kumgonga mguuni.
Asbuh,
jamaa anaamshwa aone kilichowapata mbwa wake na ngombe.
Wanastuka MTU haamki, Kuangalia wanaona jeraha LA meno kwny mguu.
Na ngozi ya mwili wake ishabadilika kua blue black
PEMBENI
WANAONA GAMBA LOTE ALILOJICHUNA BLACK MAMBA MULE MULE CHUMBANI KWAKE.
Wananchi walighadhabika mno;
Msako wa wiki 2 ulifanyika kumsaka kila kona bila mafanikio.
Tulizuiwa mpaka kumwongelea, yaani ukimtaja tu unakula viboko/makofi
Msalani; ikifika usiku MTU anasindikizwa na watu 3-4 wenye silaha.
Dah,
nkikumbuka lile tukio mwili unanisisimka.
NAJIKUTA NAMWOGOPA SANA HUYU NYOKA.