Hatari za nyoka
1. COBRA (wanaitwa spitting cobra) wanatema sana mate yanafika hata mita kumi, mara zote wanalenga macho na wakikupata unakuwa kipofu ukichelewa kunawa haraka na maji. Wataalamu wanasema wako precise kiasi kwamba akiamua kutema ana uhakika lazima yakupate machoni, hatemi ovyo ovyo.
2. Mambas (Black&Green) wanameno makali sana kama sindano yana tundu katikati (kama sindano ya hospitali) kwa ajili ya kupump sumu, akikung'ata anapump sumu kwa kiwango cha ukubwa wa adui, kiwango anachopump kwa panya sio sawa na anachopump kwa binadamu. Kwa wakati mmoja anakuwa na sumu ya kuua watu 20 kwa mara moja. Huyu black mamba anaongoza kwa mbio akikimbia unaona kama anateleza na kicha anakiinua kidogo wakati anakimbia.
3. CHATU (python) huyu hana sumu kabisa yeye anatumi nguvu tu kumnyonga adui mpaka afe. Ana misuli ina nguvu sana akikuvingirisha ni ngumu kujinasua, wataalam wanashauri akikukamata upambane nae sana usiogope sura yake mbaya tumia nguvu sana kujinasua.
MUHIMU: Kwa haraka haraka jinsi ya kumjua nyoka asiye na sumu na mwenye sumu.
-Nyoka mwenye macho ya round na makubwa hana sumu kabisa mshike tu hawezi kukufanya chochote (ni kama toy)
-Nyoka mwenye macho yaliyochongoka (yako umbo la oval) ukimuona kimbia sana atakuua huyo.
Duniani nyoka wenye sumu ni asilimia 25 tu 75 hawana sumu kabisa.