Koboko (black mamba) ni nyoka mpole sana ila ukikutana nae usimpige wala kumtisha, nakuhakikishia atasepa atakuacha hata kama alikua karibu na wewe vipi; ila ukitaka uone show yake mchokoze tu, Hapo ndipo utajua kwanini akaitwa koboko.
Kuna kipindi nakumbuka enzi hizo kijijini nikiwa na uncle wangu; tulikuaga tukienda kurina asali porini usiku kwenye mapango ya mibuyu ukiingia unawakuta kibao wapo juu ya kuta za pango kwa juu, na hawana shida utatoa asali mpaka utaondoka yupo tu anakuangalia tena utakuta yupo juu kidogo tu ya kichwa; ila tu hawapendi kelele za ovyo, pia wanawika sana usiku na hupenda sana asali.
Kwaiyo ni wakawaida sana hawana Shida tatizo la waadhirika wengi wa black mamba huwakorofi wao.