Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko aliekomaa akienda kunywa maji mtoni wakati wa kiangazi viboko na mamba huwa wanampisha.
 
NAONA TUMESOMWA.

WHO yatoa tahadhari kuhusu watu kuumwa na nyoka
  • Saa 3 zilizopita
_101749704_snakesss.jpg
Haki miliki ya pichaRSPCA
Image captionMashambulizi ya nyoka yameleta madhara makubwa duniani
Nchi wanachama wa mkutano wa shirika la afya duniani wamepitisha azimio la kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele katika kulishughulikia.

Maelfu ya watu hufa kila mwaka na wengine kuwa walemavu kutokana sumu inayotokana na shambulio la nyoka.

WHO inasema athari zinazotokana na kuumwa na nyoka zimeendelea kuwa moja kati ya magonjwa ya kitropiki ambayo hayatiliwi maanani.

Kufikiwa makubaliano hayo kwa nchi wanachama wa WHO , kuna nia ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na mbinu za kuzuia, kutibu na kukabili mashambulizi ya nyoka.

Makundi ya mbalimbali ya wanaharakati wa masuala ya afya yamesifia azimio hilo na kusema kuwa hatua hiyo inafungua milango katika kupunguza vifo na ulemavu duniani kote.

Shirika la Afya duniani sasa lina jukumu la kuja na mpango wa pamoja kuimarisha programu za tiba, kuzuia na kurekebisha.

Hii itahusisha kutoa dawa za kupambana na sumu kwa bei rahisi, dawa ambazo ilikua gharama kupatikana kwenye nchi zilizo masikini hasa zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.

_101749707_nyoka.jpg
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWataalam wanasema zaidi ya watu 100,000 hufa kutokana na madhara ya kuumwa na Nyoka
Hali ya umaskini na kutokuwa na vituo vya afya vinavyokidhi mahitaji kumesababisha vifo vya maelfu ya watu huku wengine wakitafuta tiba kwa matabibu wa kienyeji ambao husababisha madhara zaidi.

Lakini mpango huu mpya utalenga kuwafundisha watoa huduma wa afya jinsi ya kushughulikia mtu aliyeumwa na nyoka na elimu ya huduma ya kwanza kwa jamii iliyo hatarini.

Kila mwaka zaidi ya watu laki moja hufa duniani kutokana na kuumwa na nyoka asilimia 20 kutoka barani Afrika.

Karibu watu nusu milioni wana ulemavu wa kutokuona, kukatwa viungo na ulemavu mwingine kutokana na mashambulizi ya nyoka.

Dondoo za huduma ya kwanza baada ya mtu kuumwa na nyoka:
  • Jaribu kukumbuka umbo na rangi ya Nyoka:
Kufahamu namna ambavyo Nyoka anavyofanana kunasaidia wakati wa matibabu baadaye, lakini usijaribu kumshika kwa kuwa utakuwa hatarini hata akaleta madhara kwa mtu mwingine.

  • Ondoka eneo la hatari
Kama uko mwenyewe mbali na msaada, jambo la kwanza ni kwenda eneo lenye usalama.Tafuta eneo ambalo utaomba msaada.Kama uko na watu wengine wacha wakubebe kama inawezekana,ili kupunguza kiasi cha sumu kutembea mwilini,wataalam wanaeleza.

  • Usifyonze sumu kutoka kwenye jeraha
Sumu huingia ndani kabisa kwenye eneo la kati ya ngozi na misuli na husambaa mara moja (ndani ya dakika moja).Hivyo haiwezekani kuondoa sumu kwa kunyonya kwani itazidisha maumivu na uharibifu zaidi pasipo na ulazima.

  • Ondoa vitu vilivyovaliwa sehemu iliyoathiriwa
Vua vitu kama pete au nguo zinazobana katika eneo ambalo madhara yametokea kama mkononi kwa sababu vinaweza kusababisha damu kutotembea vizuri.

Source:BBC
 
Kuna sehemu nipo huku mkoani Tabora sehemu nilikuwa nimekaa nikasikia watu wakimsimulia nyoka aina ya koboko ambaye inasemekana anapatikana Tabora ,Shinyanga,Singida na Kigoma.

Kuna mtu mmoja katika mazungumzo yake alikuwa akisema ni bora ukutane na simba au chui unaweza ukapona kuliko koboko. Nilipojaribu kumuuliza alisema hayupo tayari kumuongelea kiundani wala kumtaja kwasababu ukiwa ndani ya mkoa wa Tabora au Shinyanga ni marufuku kumtaja huyu nyoka jinsi alivyoniambia.

Sasa kwa wale wanaomfahamu hebu tuelezeeeni kwanini koboko anaogopeka kuliko simba au chui?

-----

Pia soma...

HABARI,
"MSELA WA MANZESE,
Swali ni zuri mimi ninachokijua kikubwa ni kwamba huyu nyoka hapendi bugudha akiwa kwenye eneo lake mfano uko kwenye mti wa mchungwa unachuma machungwa yeye akiwa upande wa pili akihisi kuna mtu analeta vurugu kwenye eneo hilo yeye huwa akimbii bali anakuja kukugonga na nyoka wengi huwa wakigonga wanakimbia yeye anabaki hapo hapo kama unaweweseka anagonga tena hata mara 30 mpaka ufe tofauti na cobra yeye akigonga hukimbia ukiwakaribu yake yeye kakuona wewe hujamuona anakimbia,Pia anaweza kusimama kimochako mbeleyako kama ukikutana nae na ukisimama naye anasimama anakuangalia ukitikisika tu au kukimbia anagonga.

AINA
Mpaka sasa ziko aina 4 za hawa mamba snake.
1.Black mamba=Wanapatikana zana Africa kusini-kati-mashariki
2.Eastern green mamba=Wanapatikana sana Nchi chache Africa-kusini-kati na magharibi
3.Jameson's mamba=Wanapatikana Nchi chache za Africa kati-mashariki-magharibi
4.WesternGreen mamba=Wanapatikana Aafrica Magharibi

SUMU
Black mamba yuko namba 5-7 kwenye orodha ya nyoka wenye sumu kutokana na tafiti kunawatu wanatofautiana ila yuko kwenye namba hizo.
Hii ni orodha ya nyoka kumi wenye sumu duniani

1.Fierce Snake or Inland Taipan
2.Eastern Brown Snake
3.Blue Krait
4.Taipan
5.Black Mamba
6.Tiger Snake
7.Philippine Cobra
8.Vipers
9.Death Adder
10.Rattlesnake

LUMUMBA
 
Huyu vipers ndo yupi
Bongo yupo kweli
 
Back
Top Bottom