Ushindi ni kiwango cha kutandaza kandanda, hayo mengine ni mbwembwe tu. Kuna wachezaji watukutu duniani lakini makocha walienda nao hivyo hivyo kwa kutambua mchango wao. Edmundo, Romario na Baloteli ni mfano tu wa wachezaji wasio na nidhamu ndani na nje ya uwanja, yaani red card ni muda wowote! Lakini hasara ya kuwakosa kikosini ni kubwa kuliko kuwa nao, na ndio maana makocha walikuwa wanawatumia hivyo hivyo kwenye vikosi vyao. Sasa itakuwa hawa waliochelewa kufika kambini, ukizingatia siku waliyotakiwa kuripoti kambini walikuwa na mechi iliyoisha saa 2.00 usiku! Mbona kambi bado inasubiri wachezaji kibao tu, watano waliopo Kigali na Yanga, akina Samata, Msuva, Ulimwengu, Banda, Farid, Chilunda na Mandawa, wote hao wapo nje bado hawajafika, eti unawafukuza wachezaji waliomaliza mechi saa 2 usiku !