Mwalimu Kaze anaongoza duniani kwa kufundisha kukaba , kulinda na kuzuia kufungwa. Ukiifunga Yanga goli moja tu Kaze halali wiki nzima anastudy umeifungaje Yanga mwanya uko wapi, iliwezekanaje basi goli moja tu litamuuma mno! Ukiifunga Yanga goli mbili anaweza kupata homa!
Kifupi Cedric Kaze hataki kufungwa na anajua kulinda asifungwe. Bado Kuna shida Yanga juu ya kucheza krosi , mabeki kuruka na washambuliaji hapa ndo bado Kaze hajafanikiwa.
Wachezaji wa Yanga wameshamuelewa na Sasa kuifunga Yanga kwa mpira wa move ni ngumu sana ni kubahatisha tu.
Kaze ni mtu sahihi. Atasaidia sana Taifa Stars kujifunza kuzuia ila tu iwapo hao wageni Toka Simba sijui Geita kama watafundishika. Yanga oyeeee!