Kocha Fred Minziro akanusha kuwa na tofauti na Karia, awashangaa wazushi

Kocha Fred Minziro akanusha kuwa na tofauti na Karia, awashangaa wazushi

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Kocha wa timu ya Geita Gold, Fred Felix Minziro amewakanusha watu wote wanaosambaza video inayojaribu kuwashawishi washabiki waamini kwamba Rais wa TFF ana chuki naye na kwamba aliukwepa kwa makusudi mkono wake.

Minziro amesema Karia ni rafiki yake mkubwa na wamekuwa wakizungumza mara kwa mara mambo ya soka, hivyo haoni kama kuna tatizo lolote.

Pia soma > Rais wa TFF Karia ana tatizo gani Kocha Fred Felix Minziro? Tazama video hii

Fred felix Minziro, huyu mwamba aliichezea Yanga kwa mapenzi ya dhati kabisa, sikua najua kama bado yupo kwenye Soka kama kocha, nimtakie maisha marefu yenye afya na furaha.
 
Fred felix Minziro, huyu mwamba aliichezea Yanga kwa mapenzi ya dhati kabisa, sikua najua kama bado yupo kwenye Soka kama kocha, nimtakie maisha marefu yenye afya na furaha.
Dooh mkuu umeacha kufwatilia soka mwaka gani, inaonekana kitambo sana.

Minziro mbona ni kocha regular sana bongo kashafundisha timu nyingi sana za ligi kuu kwa nyakati tofauti tofauti hata yanga kafundisha sana.
 
Mkuu nabeba box huku kwa malkia,so kuna vingine vinanipita.
 
Minziro kaongea kwa busara kumstahi Karia ila alichofanya Karia ni ujinga wa kiwango cha lami
 
Minziro kaongea kwa busara kumstahi Karia ila alichofanya Karia ni ujinga wa kiwango cha lami
Anayepaswa kulalamika anasema hakukuwapo tatizo lolote, wasiopaswa kulalamika ndio wanalalamika
 
Anayepaswa kulalamika anasema hakukuwapo tatizo lolote, wasiopaswa kulalamika ndio wanalalamika
Hata mimi najaribu kuita watu watusaidie kushangaa.wanatoka povu balaa.wanaosahau kuwa nao ni binadam hakuna mkamilifu.
 
Sasa kwa akili ya kawaida ulitegemea Minziro aseme yeye ana bifu na boss wa Tff? Yaani kilakitu kimeonekana dhahiri bado unatafuta ushahidi upi? Kocha ametumia busara ya kawaida kabisa.
 
Karia kanenepa sana, ngoja nichukuwe fomu ya kugombea urais tiefuefu
 
Back
Top Bottom