Kocha Gaborone; Yanga ndio yenye presha zaidi

Kocha Gaborone; Yanga ndio yenye presha zaidi

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Kocha wa Timu ya Gaborone United ya Botswana, Sean Connor amesema kikosi chake kimejipanga kwa nidhamu, umakini na mbinu kuhakikisha kinapata matokeo dhidi ya Young Africans, akieleza kuwa wamebaini maeneo ambayo wanaweza kuyatumia kuisumbua Yanga katika mchezo huo.

Amesema Yanga ilionyesha ubora katika mchezo uliopita kwa namna ilivyofuata mpango wa mchezo na kuwa na ustahimilivu, lakini safari hii wanatarajia kuonyesha kiwango tofauti.

Kocha huyo amesisitiza kuwa wanakabiliwa na timu kubwa yenye wachezaji wenye uwezo na kujiamini, hivyo wanapaswa kudhibiti nguvu hizo huku wakitumia maeneo waliyoona yanaweza kuwapa faida.

Kuhusu presha, kocha huyo amesema Yanga ndiyo yenye presha kubwa zaidi, kwa kuwa inacheza nyumbani mbele ya mashabiki na vyombo vya habari vinavyotarajia ushindi, Ameongeza kuwa Yanga ni moja ya klabu kubwa Tanzania, lakini wao ni klabu kubwa zaidi nchini Botswana.
1789133314611.png
 
Back
Top Bottom