Kocha Gamondi atafutiwe kocha msaidizi mzawa

Mada / mjadala unaongelea nini?
baada ya ranieli kuchukua kombe la ligi kilimkuta nini kam sio kufukuzwa?
Hatuongelei bahati tunazungumzia mipango.ile ya Leicester ni bahati.ila mpira bila pesa hautoboi.kocha ana nafasi ndogo sana katika mafanikio ya timu
 
Ukuaji wa mpira wa miguu Tanzania unaosemwa kila siku unazunguka kwenye hizi timu 2 mbili tu za Kariakoo, ushabiki na siasa za mpira ziko hapo.

Uhalisia wake ni kukosa wachezaji wazuri wa ndani, kukosa makocha, kukosa marefa.

Kwa kifupi soka letu halizalishi, kama ambavyo nchi yetu haizalishi, zaidi ya kuImport zaidi. Wachezaji wenye asili ya kibongo, walihamasika na upepo uliokuja wa kutaka matokeo bila kulima, wako kimya sasa.

Solution, mpira kama fani nyingine inahitaji kujengwa toka chini, wataalamu wapewe na nafasi za kuongoza na kuchagiza maendeleo. Siasa ziwekwe kando.
 
Meneja wa yanga walter anafanya kazi na gamondi
 
Nikiwa kama mdau na mshabiki wa soka la Tanzania, nami nimewiwa kuchangia hili kwa maendeleo endelevu ya soka la klabu ya Yanga na Taifa kwa ujumla

Nashauri klabu ya Yanga ilete kocha kijana mzawa awe kwenye jopo/benchi la ufundi la kocha wa timu ya Yanga( Dar Young African FC). Hii ni kutokana na MAFANIKIO lukuki aliyoyaleta kocha huyu toka nchini Argentina.

Naamini ujuzi, mbinu ,uzoefu na mikakati ya kocha huyu GWIJI ,si vyema kuacha ipotee pindi atakapo amua kuondoka. Hivyo nashauri klabu ya Yanga kuleta kocha/makocha vijana kwa ajili ya kujifunza UCHAWI wa kocha huyu mkongwe ili hata siku akiondoka tubaki na ujuzi wake. Mbinu hii nimeona klabu ya Simba wakiitumia kwa kuhakikisha kocha wao msaidizi ,ndugu Matola Selemaini kubaki kwenye benchi la ufundi la klabu hiiyo licha ya mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha,naamini after time t ,Kocha Matola atakuja kuwa sio HAZINA tu kwa Simba bali hata kwa Taifa..Yanga igeni hili haraka

Mwisho, nawashauri TFF na hata Wizara ya Michezo kuona namna bora zaidi ya kuchota UJUZI wa gwiji hili la soka toka nchini Argentina..tuitumie fursa hii ya yeye kuwepo nchini

Naomba kuwasilisha
Asanteni
Naunga mkono hoja
Gamondi ni profesa wa mpira Bongo
Ni vema makocha wetu wazawa wakakaa naye wajifunze .
 
Waswahili wana msemo mmoja usemao; 'Mgema akisifiwa, tembo (pombe ya mnazi) hulitia maji.'

Nadhani huu ushauri ni kama kuanza kulitia maji tembo. Kocha mkuu huchagua mwenyewe msaidizi wake, mwanzoni mwa kazi.

Ova
 
Vipi Chelsea
Ni masikini?
Ndio ujue
Pesa bila mtu wa coach vizuri ni kazi bure
baada ya ranieli kuchukua kombe la ligi kilimkuta nini kam sio kufukuzwa?
Hatuongelei bahati tunazungumzia mipango.ile ya Leicester ni bahati.ila mpira bila pesa hautoboi.kocha ana nafasi ndogo sana katika mafanikio ya timu
 
Meneja wa yanga walter anafanya kazi na gamondi
Nakuelewa ingawa huyu sidhani hata kama ni kocha kitaaluma..mameneja kwa navyofahamu mimi ni kama wakuu wa logistic.kuhakikisha mambo ya wachezaji yanaenda sawia..la kama ni kacha basi ni vizuri
 
Waswahili wana msemo mmoja usemao; 'Mgema akisifiwa, tembo (pombe ya mnazi) hulitia maji.'

Nadhani huu ushauri ni kama kuanza kulitia maji tembo. Kocha mkuu huchagua mwenyewe msaidizi wake, mwanzoni mwa kazi.

Ova
Mkuu Mdakuzi heshima kwako
Hoja yako nimeielewa, na ni kweli mara nyingi makocha wakuu hupenda kuwa na watu wao,na natambua wasaidizi wa bwana Gamondi wapo wakiongozwa na yule Msenegali..ndio nikashauri kwa masalahi mapana ya timu na nchi kwa ujumla tunaweza kufikiria hili,tukamuita Gamondi mezani HOJA zikawasilishwa kwake..sidhani kama atakataa
 
Mnataka kuleta wafitinishaji kwenye timu, mtu wa kutengeneza makundi kwenye dressing room. Acha iwe hivi hivi angalia upendo uliopo kwenye timu hakuna mchezaji anayejiona ni bora kuliko wenzake bali wote wanajiona ni wanafamilia na umoja wao ndio mafanikio ya timu.
Sahihi kabisa Gamondi anaishi na wachezaji wake kirafiki sana na upendo wa hali ya juu. Mara acheze nao hakuna matata mara waigize kutumia VAR na kutokana na hali umoja kwenye timu. Kumleta kocha wa kibongo na kuingiza kirusi kwenye timu, wabongo kwa fitina, uchawi na majungu tupo vizuri mwisho wa siku tunarudi kwenye uswahili.
 
Mkuu Mdakuzi heshima kwako
Hoja yako nimeielewa, na ni kweli mara nyingi makocha wakuu hupenda kuwa na watu wao,na natambua wasaidizi wa bwana Gamondi wapo wakiongozwa na yule Msenegali..ndio nikashauri kwa masalahi mapana ya timu na nchi kwa ujumla tunaweza kufikiria hili,tukamuita Gamondi mezani HOJA zikawasilishwa kwake..sidhani kama atakataa
Ni fikra nzuri, lakini kuleta mabaliko makubwa kwenye benchi la ufundi la timu inayofanya vizuri ni jambo gumu hasa kwa kocha.

Ndiyo nikasema, kwa hoja hii Yanga ilishachelewa, ilipaswa kuwa mwanzo wa kandarasi na kocha ndiyo hoja hiyo inaletwa kwake.

Ujue yeye kama kocha mkuu ndiye mwenye nafasi ya kupima ufanisi wa msaidizi wake, akiwa ni mzigo anamshusha tu wakati wowote.

Ova
 
Hizi timu zetu zaidi ni pesa za Mo na GSM, hawa makocha hawana la maana sana. Mpeleke Gamond Lyamungo ndio utaelewa
Unaongea kitu kisicho na uhalisia kabisa kama ishu ni pesa azam fc ndo club yenye hela na facilities bora za soka ndani ya ukanda wa africa masharik lakini uwanjani wanafanya nin cha kushangaza . Soka ni zaidi ya uwekezaji wa fedha ndugu yangu, mafanikio katika mpira yaanaanza na management bora kabisa. Nenda pale France PSG ni club taji sana na inaweza kumsajili mchezaji yoyote yule katika hii dunia lakini mpaka leo kashindwa kutawala soka la ulaya
 
Hizi timu zetu zaidi ni pesa za Mo na GSM, hawa makocha hawana la maana sana. Mpeleke Gamond Lyamungo ndio utaelewa
Lakini pesa hata Azam wanazo.

Gamondi kawasumbua Mamelodi ambao na wao pesa wanazo.
 
Back
Top Bottom