Moshi25
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,555
- 4,118
Wanabodi
Timu yetu ilicheza vizuri sana. Tuliwamudu kabisa Algeria hadi Dkk ya 40 tukafungwa goli la bahati mbaya la faulo linalofanana kabisa na goli la kwanza Algeria walilowafunga Uganda hivi benchi la ufundi na wachezaji wetu hawakuangalia ile mechi kujifunza upigaji faulo wa Algeria ? Kwanini Manula alienda na akasita si bora angebaki golini au angeenda moja kwa moja kumsumbua yule alieurudisha mpira ndani?
Kwa maoni yangu sub za kocha Kim ndo zimetuangamiza.
Kipindi cha kwanza kinaisha tumeshafungwa kipindi cha pili kinaanza Kim bado unalinda tu kwa kuwa na wakabaji wawili Mzamiru na Novatus , unalinda nini sasa wakati ushafungwa badala ya kuanza kushambulia kwakuwa sasa huna cha kupoteza?
Nilisema kabla timu haina muanzisha mashambulizi kwenye mechi na Niger na mechi na Algeria apangwe Sureboy kuleta muunganiko sote tumeona dakika kumi zake uwanjani Algeria walitafutana!
Kim angemtoa mkabaji Mzamiru mapema sana aingie Sureboy kwenda kushambulia niliesema kuwa aanze mechi ya leo ila ujuaji umemkaa sana Kim wakati sote tunaona wanavyocheza huku vibanda umiza .
Msuva hakuwa fit hakupiga mashuti yake dkk 45 hivi benchi halikuona angetoka mapema aingie Farid mchezaji mzoefu hadi Hispania unamuwekaje benchi? Kibabage mechi ilimshinda sote tuliona angetoka mapema aingie Kibu Denis full stop ungeona kazi mashambulizi mwanzo mwisho.
Nilisema hapo kabla Novatus Dismas ni nguzo katikati asitolewe tutafungwa kwa ujuaji wa benchi wamemtoa ona sasa tumefungwa goli la pili kama nilivyotabiri!
soma hii uzi yangu
Huyu kocha Kim hatufai anawachukia wachezaji wa Yanga ambao ni moto msimu huu na kusababisha tutakosa Afcon. Au aliogopa kujaza wachezaji wa Yanga kuepuka kelele za Makolo FC?
Hivi hakuna kina Nabi wengine huko nje muwaite waje watupeleke Afcon tumechoka kuwa kichwa cha Mwendawazimu! Kubadilisha kocha ni jambo la kawaida tu TFF wasione vibaya huyu mzee Kim ameshindwa mbinu mapema tu
Mnawapa sifa kubwa Algeria ni wa kawaida sana tu na leo tuliwamudu sana wametufunga magoli mepesi sana ya bahati mbaya tu na wasingetoka kama Sureboy angeanza na kuleta muunganiko wa wachezaji wa nyuma na wa mbele.
Benchi la ufundi muwe mnachukua mawazo mengine kutoka wazoefu wa vibanda umiza kama sisi tunachowaambia kinatokea uwanjani ila ubishi bado umewajaa.
Ushauri wangu kabla ya mechi wachezaji na benchi la ufundi mkae kutazama mechi mbili za mwisho za timu tunayokutana nayo ili mjue madhaifu yao hakuna timu isiyo na uchochoro hata Real Madrid wanapigika tu ukikaa kutazama wanavyocheza na kujua pa kuwapasua.
Wanabodi mtakumbuka maneno yangu.
"mwananchi" nawasilisha
Timu yetu ilicheza vizuri sana. Tuliwamudu kabisa Algeria hadi Dkk ya 40 tukafungwa goli la bahati mbaya la faulo linalofanana kabisa na goli la kwanza Algeria walilowafunga Uganda hivi benchi la ufundi na wachezaji wetu hawakuangalia ile mechi kujifunza upigaji faulo wa Algeria ? Kwanini Manula alienda na akasita si bora angebaki golini au angeenda moja kwa moja kumsumbua yule alieurudisha mpira ndani?
Kwa maoni yangu sub za kocha Kim ndo zimetuangamiza.
Kipindi cha kwanza kinaisha tumeshafungwa kipindi cha pili kinaanza Kim bado unalinda tu kwa kuwa na wakabaji wawili Mzamiru na Novatus , unalinda nini sasa wakati ushafungwa badala ya kuanza kushambulia kwakuwa sasa huna cha kupoteza?
Nilisema kabla timu haina muanzisha mashambulizi kwenye mechi na Niger na mechi na Algeria apangwe Sureboy kuleta muunganiko sote tumeona dakika kumi zake uwanjani Algeria walitafutana!
Kim angemtoa mkabaji Mzamiru mapema sana aingie Sureboy kwenda kushambulia niliesema kuwa aanze mechi ya leo ila ujuaji umemkaa sana Kim wakati sote tunaona wanavyocheza huku vibanda umiza .
Msuva hakuwa fit hakupiga mashuti yake dkk 45 hivi benchi halikuona angetoka mapema aingie Farid mchezaji mzoefu hadi Hispania unamuwekaje benchi? Kibabage mechi ilimshinda sote tuliona angetoka mapema aingie Kibu Denis full stop ungeona kazi mashambulizi mwanzo mwisho.
Nilisema hapo kabla Novatus Dismas ni nguzo katikati asitolewe tutafungwa kwa ujuaji wa benchi wamemtoa ona sasa tumefungwa goli la pili kama nilivyotabiri!
soma hii uzi yangu
"TFF iwaandikie barua CAF kupinga kuchezeshwa mechi zetu za Afcon qualifier na waamuzi wabovu"
Benchi la ufundi lote halina ufundi wowote wa kuusoma mchezo bora watuachie timu yetu maana mechi ya pili timu imekosa mchezaji wa kupokea mipira toka nyuma na kuipeleka mbele nae ni Sureboy. Sote tumeona mara ngapi Tshabalala anapewa mpira na Mwamnyeto hana wa kumpa kupeleka mbele Tshabalala anarudisha mpira nyuma! Kina Samatta, Msuva na Feisal hakuna wa kuwalisha mipira Mzamiru hajulikani yuko wapi kupokea mipira kutoka nyuma na kupeleka mbele! Benchi la ufundi hamtufanyii haki wabongo.Job na Mwamnyeto wamepata shida sana hizi mechi mbili wamezoea kule kwao Yanga wanapasiana mpira anapewa Sureboy au Aucho ngoma inatupwa mbele Mayele au Feisal anaua! au inaenda kwa Moloko au Kibwana "wanamwaga maji" watu wanaingia nazo!Huyu kocha Kim hatufai anawachukia wachezaji wa Yanga ambao ni moto msimu huu na kusababisha tutakosa Afcon. Au aliogopa kujaza wachezaji wa Yanga kuepuka kelele za Makolo FC?