Umeandika pumba na ujinga. Simba imeanza kushiriki mashindano ya CAF tangu zamani sana.Sasa jiulize kwa nini hapo zamani simba ilikuwa inashindwa kuingia hatua za makundi? Je ni uchawi ulikuwa unazidiwa na timu wanayokutana nayo knock out stage? Au je ni wachezaji walikuwa hawana viwango?We unaona alikuwa na msaada? hakuwa na plan B timu inapoelemewa. Na lile li-formation lake la striker 1 ilikuwa inaboa sana.
Kusema kweli yule 'paka' ametoa support kubwa sana. Hivi unajua hata huyo Patrick Aussems ambaye mashabiki wa Simba wanaona alikuwa 'kocha bora' naye alikuwa 'mweupe' tu asiye na msaada? Simba iliingia robo fainali kwa issue za kipaka paka,na wala si kwa uwezo wake. Ile mechi ya Simba vs Nkana ilikuwa imeshachezwa siku 2 kabla ya game halisi na viongozi wa Simba waliingia kwa Mkapa wakiwa na matokeo, NA NDIVYO ILIVYOKUWA.
Nyinyi watoto wa .com mnaosema zile issue huwa hazina msaada endeleeni kuamini hivyo. DUNIA SI KAMA UIJUAVYO.
Ngoja nikuambie Simba imefanikiwa kuingia hatua ya makundi sasa na miaka ya karibuni kutokana na kukutana na timu hasiyopishana nayo viwango knock out stage. Simba hajapishana viwango na nkana au platinum kwa hiyo yoyote kufungwa sio ajabu. Hapo zamani kabla ya 2017 timu zilizokuwa zinaunda makundi zilikuwa 8 na ndio maana ilikuwa ngumu kupenya kwa simba au yanga kutokana na kukutana na mpinzani wa kiwango cha juu knock out stage. Ilikuwa kawaida kupangiwa Esperance , al ahly, zamalek n.k .
Hata ukiangalia matokeo ya head to head kwa mechi za kwenye makundi kati ya simba dhidi ya timu zilizojuu ya viwango(al ahly, as vita) ingekuwa knock out stage simba ingekuwa imetolewa.
Tangu mwaka 2017 CAF waliongeza idadi ya timu kutoka 8 hadi 16 na hii kupelekea timu zisizopishana sana viwango kukutana knock out stage.
Ni mjinga tu atakayeamini Nkana au Platinum atafungwa na simba kwa sababu ya kulogwa na si sababu za kimchezo.