Habari za chinichini zilizonifiki zinasema kwamba baada ya kusemekana kuwa Kelvin Yondani, Endrew Vicent 'Dante' pamoja na Juma Abdul, kugomea mazoezi kisa kudai malikimbikizo ya mishahara yao, Bundi ameanza kutanda mitaa ya Twiga na Jangwani kwani kuna taarifa za chinichini zinadai kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Mwinyi Zahera naye ameweka mgomo wa kurudi Tanzania mpaka alipwe pesa zake.
Taarifa zinadai kuwa kocha Zahera, wakati akiifundisha Yanga kwa msimu uliomalizika, 2018-19, kuna baadhi ya gharama alikuwa akizitoa kwenye timu, kama vile kuisafirisha timu, posho za wachezaji na mambo mengine.
Chanzo Taarifa: Shaffih Dauda na Mtandao wake pia
Mmetutisha tisha hapa sijui na Harambee yenu ya KUBWA LAO huku mkasema kuwa mmekusanya karibia Bilioni 1 na Nusu hatimaye sasa ukweli wa mambo na hali Halisi ya Shida, Njaa na Umasikini unajidhihiri na Watu ( wana Yanga mnaumbuka )
Na hakyanani kwa Maandalizi ya Simba SC na kwa aina ya Kikosi Kipana na kilichosheheni Mafundi watupu wa Mpira cha Simba Sports Club kuna uwekano mkubwa kwa Msimu mpya ( Ujao ) wa Ligi Simba SC ikawa Bingwa ikiwa imebakiza Mechi 11, haitofungwa na Timu yoyote na kuna Klabu Pinzani na Simba SC isipokuwa Makini kuna uwezekano Mechi ya Kwanza wakapigwa Goli 9 na Mechi ya Pili wakapigwa hata 13 kisha wakatafutana huko katika Bwawa lao Kuu la Kuogelea Binadamu, Chura, Bata na Samaki.
Kwa aina ya Mazoezi niliyoyaona ama hakika hawa Wabrazil Watatu watakuwa wanatufanya wana Simba SC kila mara tuwe tunatapika ( tunashangilia ) tu Majukwaani kwa furaha tele kwani wanaupiga mwingi hadi wanakera na nawatabiria akina Kagere na Boko hadi Ajib kuwa watakuwa wanafunga Magoli hadi watanuna kama si Kuchukia kwa aina ya Pasi mpenyezo za hawa Wabrazili Watatu Kikosini.
Asante Mo Dewji.