Kocha mpya wa Yanga hana sifa za kuwa Kocha Mkuu wa Ligi Kuu ya Tanzania

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
2c5394b45fd84692973b0d167a460dde.jpg

🚨 Kama Bodi ya Ligi Kuu Tanzania na idara ya ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) watasimamia vyema kanuni za Ligi Kuu msimu huu, hakuna namna Kocha mpya wa Yanga, Hamdi Miloud atalazimika kushushwa cheo na kuwa kocha msaidizi kwa daraja lake la leseni halitoshi kumfanya awe kocha Mkuu wa timu inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC na badala yake anapaswa kuwa msaidizi.
.
Yanga ilianika hadharani wasifu wake ambao ulionyesha kuwa Mualgeria huyo ana leseni daraja A iliyotolewa na Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (Uefa).
.
Kanuni ya 77 ya Ligi Kuu imefafanua sifa za kocha mojawapo ikiwa ni hadhi ya leseni inayofafanua kuwa kocha mwenye leseni kutoka nje ya Afrika anapaswa kuwa na ngazi ya Pro Diploma ambayo kwa Afrika ni sawa na Diploma daraja A.
.
3.1 “Kocha mkuu wa klabu ya Ligi Kuu kutoka nje ya bara la Afrika anatakiwa kuwa na angalau Pro Diploma au inayolingana nayo. 3.2 Kocha msaidizi wa klabu ya Ligi Kuu kutoka nje ya bara la Afrika anatakiwa kuwa na angalau A Diploma au inayolingana nayo.
.
“Kocha wa timu ya Ligi Kuu kutoka nje ya Tanzania ni lazima awe amefundisha klabu ya Ligi Kuu au timu ya Taifa katika nchi yoyote ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita,” inafafanua kanuni hiyo
.
Wakati kanuni zikimbana Miloud, kocha msaidizi Abdihamid Moalin yeye ana sifa stahiki za kuliongoza benchi la ufundi la Yanga kwa vile ana leseni daraja A inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
 
Kocha mpya aliyetangazwa na Yanga Maloud Hamdi hana vigezo vya kuwa Kocha Mkuu wa Ligi Kuu ya Tanzania bara,kwa mujibu wa kanuni,kocha mkuu anatakiwa kuwa na Diploma A ya CAF au Pro Diploma (eg UEFA Pro )kwa kocha aliyesoma nje ya CAF,Kwa mujibu wa taarifa ya Yanga,kocha wa Yanga anamiliki leseni ya UEFA A ambayo haikidhi vigezo vya Bodi ya Ligi. Hivyo Kuna uwezekano mkubwa Mkurugenzi wa Ufundi Moalini akatambuliwa kama kocha mkuu na TFF na huyu Hamdi akawa Kocha Msaidizi lakini kwenye uwanja wa mazoezi akasimama kama kocha mkuu,kama ilivyokuwa kwa Yusuf Dabo na Azam ambalo Dabo alitambulika kama kocha msaidizi
 
Attachments

  • Screenshot_20250205-102759.png
    Screenshot_20250205-102759.png
    1.3 MB · Views: 3
Kocha mpya aliyetangazwa na Yanga Maloud Hamdi hana vigezo vya kuwa Kocha Mkuu wa Ligi Kuu ya Tanzania bara,kwa mujibu wa kanuni,kocha mkuu anatakiwa kuwa na Diploma A ya CAF au UEFA Pro kwa kocha aliyesoma nje ya CAF,kocha wa Yanga anamiliki leseni ya UEFA A ambayo haikidhi vigezo vya Bodi ya Ligi. Hivyo Kuna uwezekano mkubwa Mkurugenzi wa Ufundi Moalini akatambuliwa kama kocha mkuu na TFF na huyu Hamdi akawa Kocha Msaidizi lakini kwenye uwanja wa mazoezi akasimama kama kocha mkuu,kama ilivyokuwa kwa Yusuf Dabo na Azam ambalo Dabo alitambulika kama kocha msaidizi
Wametoa side kama side wamemleta Maulid hamad.

Ila UTO.
 
alafu ebu nyie wasomi mnieleze huyu anaazaje kazi mara moja wakati vibali vyake vya kazi ni vya singida black stars?
Wala hana vibali vya Singida alikuwa anasimamia mazoezi tu.Hawezi kukaa kwenye benchi la ufundi kama kocha mkuu.
 
View attachment 3225734
🚨 Kama Bodi ya Ligi Kuu Tanzania na idara ya ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) watasimamia vyema kanuni za Ligi Kuu msimu huu, hakuna namna Kocha mpya wa Yanga, Hamdi Miloud atalazimika kushushwa cheo na kuwa kocha msaidizi kwa daraja lake la leseni halitoshi kumfanya awe kocha Mkuu wa timu inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC na badala yake anapaswa kuwa msaidizi.
.
Yanga ilianika hadharani wasifu wake ambao ulionyesha kuwa Mualgeria huyo ana leseni daraja A iliyotolewa na Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (Uefa).
.
Kanuni ya 77 ya Ligi Kuu imefafanua sifa za kocha mojawapo ikiwa ni hadhi ya leseni inayofafanua kuwa kocha mwenye leseni kutoka nje ya Afrika anapaswa kuwa na ngazi ya Pro Diploma ambayo kwa Afrika ni sawa na Diploma daraja A.
.
3.1 “Kocha mkuu wa klabu ya Ligi Kuu kutoka nje ya bara la Afrika anatakiwa kuwa na angalau Pro Diploma au inayolingana nayo. 3.2 Kocha msaidizi wa klabu ya Ligi Kuu kutoka nje ya bara la Afrika anatakiwa kuwa na angalau A Diploma au inayolingana nayo.
.
“Kocha wa timu ya Ligi Kuu kutoka nje ya Tanzania ni lazima awe amefundisha klabu ya Ligi Kuu au timu ya Taifa katika nchi yoyote ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita,” inafafanua kanuni hiyo
.
Wakati kanuni zikimbana Miloud, kocha msaidizi Abdihamid Moalin yeye ana sifa stahiki za kuliongoza benchi la ufundi la Yanga kwa vile ana leseni daraja A inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
Unajua msiwe mnadandia dandia tu vihabari kwenye mitandao bila kujiridhisha,,unasema hana sifa za kukaa kwenye benchi la yanga,,swali ni Moja tu na ulijibu imekuwaje tff wakampa leseni ya kuifundisha timu ya ligi kuu kama hana sifa stahiki?
Tff wasingempa leseni kama akidhi vigezo,,au pale singida alikuwa anaenda kuwa kocha msaidizi?
 
Wala hana vibali vya Singida alikuwa anasimamia mazoezi tu.Hawezi kukaa kwenye benchi la ufundi kama kocha mkuu.
Mbumbumbu ni mbumbumbu tu ni empty brain kweli kweli,,kama ujui kitu ni Bora ukakaa kimya kuliko kujiaibisha!
 
Back
Top Bottom