Kocha mpya wa Yanga Sead Ramovic ni hatari zaidi kuliko Gamond baada ya mechi tano zijazo mtamsahau Gamond

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Naomba niwe mtu wa kwanza kutofautiana na wengi wanaomponda kocha RAMOVIC.

Ni kawaida kwa kocha yeyote mpya kupoteza mechi ya kwanza japokuwa sio makocha wote.

Uchebe mwanzoni mwa pre season alikuwa anafungwa mpaka na Dodoma jiji kwenye friend match, pia Al Hilal ilimkanda kwenye CECAFA, Kocha Rachid Touasi naye alipoteza mechi yake ya kwanza dhidi ya simba.

Gamond pia alichezea kichapo cha mbwa koko kule Algeria dhidi ya CR BELOUZDAD licha ya Yanga kumiliki mpira kuliko CRB.

YANGA YA MJERUMANI INA FALSAFA GANI?

Yanga ya mjerumani falsafa yake ni soka safi pasi laki tano, pia kujilinda kwa kumiliki mpira.

Mechi ya kwanza niliiona namna ambavyo Yanga ilimiriki mpira hapakuwa na butua butua wala pasi ya kupiga mpira wa juu.

Wachezaji wengi wa Yanga walionekana kutokuwa na speed sababu falsafa ya kocha ni mpya hawajaizoea. Unaona kabisa sehemu ya kupiga counter atack mchezaji hapigi pasi ndefu ya juu badala yake anapiga pasi fupi ila mpira mpaka unapenyezwa kwa mshambuliaji (Dube) tena kwa kupenya kati kati ya box kabisa.

Beki Bacca na Job wanaonekana kutokumaster vizuri falsafa ya kocha unaona kabisa wanapiga pasi lakini ndefu mpinzani anauwahi mpira na kutaka kuishambulia Yanga.

Kibabage na Yao wanapanda sana mbele wanaacha nafasi kwenye mbavu za uwanja sababu wamezoea kusaidiwa kazi na wachezaji wenye tabia za kiungo mkabaji kama Max nzengeli.

Max Nzengeli anaonekana hafati falsafa ya kocha anapiga mashuti hovyo kama kawaida yake kocha anaamua kumtoa nje.

Sababu ya Yanga kupoteza ni moja tu, wachezaji hawajazoea falsafa ya kocha.

KWANINI RAMOVIC NI HATARI KULIKO GAMOND

Sababu ni moja tu, endapo ataanza kupata Goli na anajilinda kwa kumiliki mpira, moinzani atalazimika kufunguka na atataka kupishana na Yanga uwezekano wa kupigwa goli nyingi ni asilimia 99%

Usiombe Yanga ya Ramovic ikutangulie kukufunga utajuta. Ila ukiitangulia kuifunga utaifunga goli nyingi kama unawashambuliaji wazuri.

Msije kusema OMOYOGWANE Ahakusema enyi wachambuzi wa mitandaoni mliojaa mihemuko.

Nawasilisha
 
Maneno mingi sitaki kusikia, ninataka kuona dozi ya tano tano inarudi tena.Nabi aliwajenga wachezaji discipline sana ikawa ndiyo siri ya mafanikio yao. Gamondi aliwaharabu wachezaji wakapoteza discipline kabisa ndiyo maana unaona viwango vimeshuka kwa sababu ya kutumia nguvu nyingi sana nje ya uwanja. Ramovic anatakiwa airudishe ile discpline ya mwanzo aliyoacha Nabi
 
Side Mnyamwezi kutoka Germany 🤣🤣 Jamani mechi na Namungo lini?
 
Watu wanamshambulia kwa sababu ya mihemko
Naona mnafanya crisis management. 😅😅😅😅😅 sisi tunataka apewe misimu miwili aunde timu, ule watatu aanze kutoa ushindani. Wa nne asogee hadi nafasi ya pili ukifika watatlno ndiyo aanze kuepewa nafasi ya ubingwa.
 
Alifundisha kule south Africa tena wale walikuwa wanaongea kiingereza hawa ambao mpaka watafsiriwe ndio wataelewa falsafa yake kweli.
 
Niliona Yanga ilivyocheza. Huyu jamaa kuna bomu analisuka litakuja kuleta maafa sana pale mitaa ya Msimbazi hawataamini.

Wagermany hawana huruma.
 
Naomba niwe mtu wa kwanza kutofautiana na wengi wanaomponda kocha RAMOVIC.

Ni kawaida kwa kocha yeyote mpya kupoteza mechi ya kwanza japokuwa sio makocha wote.

Uchebe mwanzoni mwa pre season alikuwa anafungwa mpaka na Dodoma jiji kwenye friend match, pia Al Hilal ilimkanda kwenye CECAFA, Kocha Rachid Touasi naye alipoteza mechi yake ya kwanza dhidi ya simba.

Gamond pia alichezea kichapo cha mbwa koko kule Algeria dhidi ya CR BELOUZDAD licha ya Yanga kumiliki mpira kuliko CRB.

YANGA YA MJERUMANI INA FALSAFA GANI?

Yanga ya mjerumani falsafa yake ni soka safi pasi laki tano, pia kujilinda kwa kumiliki mpira.

Mechi ya kwanza niliiona namna ambavyo Yanga ilimiriki mpira hapakuwa na butua butua wala pasi ya kupiga mpira wa juu.

Wachezaji wengi wa Yanga walionekana kutokuwa na speed sababu falsafa ya kocha ni mpya hawajaizoea. Unaona kabisa sehemu ya kupiga counter atack mchezaji hapigi pasi ndefu ya juu badala yake anapiga pasi fupi ila mpira mpaka unapenyezwa kwa mshambuliaji (Dube) tena kwa kupenya kati kati ya box kabisa.

Beki Bacca na Job wanaonekana kutokumaster vizuri falsafa ya kocha unaona kabisa wanapiga pasi lakini ndefu mpinzani anauwahi mpira na kutaka kuishambulia Yanga.

Kibabage na Yao wanapanda sana mbele wanaacha nafasi kwenye mbavu za uwanja sababu wamezoea kusaidiwa kazi na wachezaji wenye tabia za kiungo mkabaji kama Max nzengeli.

Max Nzengeli anaonekana hafati falsafa ya kocha anapiga mashuti hovyo kama kawaida yake kocha anaamua kumtoa nje.

Sababu ya Yanga kupoteza ni moja tu, wachezaji hawajazoea falsafa ya kocha.

KWANINI RAMOVIC NI HATARI KULIKO GAMOND

Sababu ni moja tu, endapo ataanza kupata Goli na anajilinda kwa kumiliki mpira, moinzani atalazimika kufunguka na atataka kupishana na Yanga uwezekano wa kupigwa goli nyingi ni asilimia 99%

Usiombe Yanga ya Ramovic ikutangulie kukufunga utajuta. Ila ukiitangulia kuifunga utaifunga goli nyingi kama unawashambuliaji wazuri.

Msije kusema OMOYOGWANE Ahakusema enyi wachambuzi wa mitandaoni mliojaa mihemuko.

Nawasilisha
Bahati nzuri soka ni mchezo wa wazi!
 
BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE ALITUTAJIA MAADUI.

1. UMASIKINI
2.UJINGA.
3. MARADHI.

Akasema Hawa ni maadui wa kweli kweli katika hili Taifa.

LEO 2024 BAADA YA MIAKA 60 TUMEKUWA NA MAADUI WENGI ZAIDI.

2024 maadui wameongeseka Zaidi kuliko wale watatu wa 1961.

1.Umasikini na ufukara.
2.Ujinga na upumbavu.3.Magonwa na Maradhi
4.Mmomonyoko wa Maadili.
ushoga, usagaji Kamali, sugar mamy, sugar Dady mashangazi
5 AJIRA
5. Rushwa na Upendelo

6. USimba na u yanga.
7. Mitandao ya kijamii Tiktok, x, nk
8. Manabii wa uongo na Mashehe Uchwara.
9. Ajali nyingi mno.
10. Gharama kubwa za maisha, ujenzi holela nk

MAMBO NI MENGI SANA VIJANA WA KITANZANIA WANAWAZA MAMBO YA HOVYO SANA SIMBA NA YANGA ZINATAWALA MIKEKA NK.

OKOENI TAIFA LENU LEO.
MKIFIKA MBINGUNI MTAHOJIWA NA MUNGU MLILIFANYIA NINI TAIFA LENU NIMEMALIZA.
 
Back
Top Bottom