Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga SC Juma Mwambusi, amesema kwamba kitendo alichokifanya mchezaji wake Saido Ntibazonkiza kwenye mchezo dhidi ya Gwambina FC ni kutokana na furaha ya kufunga goli kwasababu hakufunga katika mechi mbili zilizopita.
"Ntibazonkiza alikuwa anafurahia kupata goli kwasababu mechi mbili zimempita alitoka bila kufunga goli". Amesema Mwambusi.
Kocha Mwambusi hivi Mchezaji anayefunga Goli huwa ananuna kama ilivyokuwa leo (jana) kwa Saido Ntibanzonkiza?
Kocha Mwambusi hivi Mchezaji anayefunga Goli (Saido Ntibanzonkiza) huwa anamfuata Kocha wake (Wewe) na Kukufokea, Kukubishia na kuelekea Vyumbani kwa Hasira?
Kocha Mwambusi hivi Mchezaji anayefunga Goli (Saido Ntibanzonkiza) kwa Furaha huwa anaanza Kujibizana hovyo na Wachezaji wenzake akina Kaseke, Nondo na Mukoko mpaka Kuwadharau?
Sikutaka Kusema kilichotokea na kama kawaida yangu Generalist huwa sipitwi na Jambo gumu pale nikitaka Ukweli wake na nashukuru mno kuwa nina Vyanzo vyangu vya uhakika huko Jangwani na Msimbazi (tena kwa wale walioko Jikoni kabisa) na nikija na Jambo hapa JamiiForums huwa silibahatishi.
UKWELI KAMILI NDANI YA YANGA
1. GSM imewagawa Wachezaji
2. Wachezaji wazawa Wanapuuzwa
3. Saido Ntibanzonkiza ana Dharau
4. Mwambusi unabagua Wachezaji
5. Wachezaji Wanarogana sana tu
6. Wachezaji wa Yanga hawapendani
7. Mishahara na Posho ni tatizo
Kesho nikiamka nitakuja na Exclusive ya kwanini Juzi Mchezaji na Kiungo mahiri wa Kinyarwanda Haruna Fadhili Hakizimana Niyonzima Yanga SC ilipocheza na Biashara United FC alipomaliza Kufuturu Tende Uwanjani akiwa amekaa pembeni ya Uwanja na Beki Bakari Nondo Mwamnyeto alipoamka alijibizana hovyo na Kit Manager wa Yanga SC huku akitukanana nae na akinyoosha kidole kwa Kocha Mwambusi.
Na nikimaliza nitakuja tena na Exclusive nyingine inayomhusu Kipa Metacha Boniface Mnata na kwanini hapangwi tena Yanga SC na Feisal Salum Fei Toto kutokupangwa kwa Maagizo kutoka Juu Uongozini na kwa GSM na Kocha Mwambusi kulazimishwa ampange Muangola Carlinho ( Kalinyo ) tu kwa sasa.
Tunajua kwanini leo ( jana ) ilikuwa iwe isiwe ni lazima mshinde kwani.
1. Mlitaka Kumuonyesha Kocha wenu mpya (asiyejua Kiingereza wala Kiswahili) Nasreddine Nabi kuwa mna Kikosi kizuri na asiogope kisha ajue kuwa ametua katika Timu bora wakati kumbe ametua katika
MATATIZO MAJUNGU LAWAMA SHIDA YANGA SPORTS CLUB ambayo kwa Historia ya huyu Kocha akidumu Yanga SC miezi Kenda (Tisa) tu ijayo Generalist nitaogelea Kifua Wazi ( Kidali Poo ) kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar.
2. Ilikuwa ni lazima leo Mshinde kwa namna yoyote ile (tena kwa idadi kubwa tu ya Magoli) ili Kuwafurahisha Mashabiki wenu na Kuwatamanisha wajitokeze kwa wingi (Nyomi Kubwa) Siku ya Jumamosi ijayo pale mtakapocheza na Azam FC ( Simba SC B ) ambayo mtafungwa na Kuvurugana zaidi.
Soka la nchini lipo 'Kiganjani' mwangu.