Kocha pekee aliyefika Fainali 6 za UEFA Champions League

Kocha pekee aliyefika Fainali 6 za UEFA Champions League

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Carlo.jpg
Carlo Ancelotti raia wa Italia ana rekodi kubwa ya kuwa kocha aliyefika Fainali 5 na kubeba mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League), mara 2 akiwa AC Milan na mara 2 akiwa Real Madrid

Msimu huu 2023/24 amefika Fainali akiwa na Real Madrid ambapo anatarajiwa kucheza dhidi ya Borrusia Dortmund mnamo Juni 1, 2024 kwenye Uwnja wa Wembley Jijini London

KOCHA PEKEE ALIYEFIKA FAINALI 6 ZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Rekodi za Ancelotti katika UCL
2023/24 – (Real Madrid) Fainali (Mechi Bado haijachezwa)
2022/23 – (Real Madrid) Nusu Fainali
2021/22 – (Real Madrid) BINGWA
2016/17 – (Bayern Munich) Robo Fainali
2014/15 – (Real Madrid) Nusu Fainali
2013/14 - (Real Madrid) BINGWA
2012/13 – (PSG) Robo Fainali
2010/11 – (Chelsea) Robo Fainali
2006/07 - (AC Milan) BINGWA
2005/06 – (AC MILAN) Nusu Fainali
2004/05 – (AC Milan) Fainali
2003/04 – (AC Milan) Robo Fainali
2002/03 – (AC Milan) BINGWA
1998/99 – (Juventus) Nusu Fainali
 
Kama ni kocha mzuri tumpe Nottingham forest au real huesca kama ataweza kuchukua Uefa au kikombe chochote hapo ndio nitaamini ni kocha mzuri lakini kufundisha real Madrid, ac milan kocha yeyote anaweza kufikia rekod hizo ni sawa sawa na kocha gamond apewe JKT tanzania alafu mwakan awe bingwa ni kitu ambacho hakiwezekan
 
Kama ni kocha mzuri tumpe Nottingham forest au real huesca kama ataweza kuchukua Uefa au kikombe chochote hapo ndio nitaamini ni kocha mzuri lakini kufundisha real Madrid, ac milan kocha yeyote anaweza kufikia rekod hizo ni sawa sawa na kocha gamod apewe JKT tanzania alafu mwakan awe bingwa ni kitu ambacho hakiwezekan
Everton tu ilimshinda akatimua mbio.
 
ni sahihi apewe maua yake, lakini pia tukumbuke kule Instabul kwenye fainali ya UCL 2005 aliongoza AC Milan 3-0 hadi mapumziko kama sikosei lakini hakutwaa kikombe!
 
Back
Top Bottom