Kocha Simba kwa heri

Kocha Simba kwa heri

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
17,296
Reaction score
18,027
SIMBA ikiwa chini ya kocha, Dylan Kerr, msimu huu imezifunga timu tatu ambazo ilishindwa kuzifunga katika misimu miwili iliyopita, lakini imebainika kuwa hata kocha huyo hana muda mrefu Msimbazi, kwani hata akishinda mechi mbili zijazo ni lazima asepe klabuni hapo.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezinasa kutoka kwa chanzo makini kilichopo Msimbazi, zinasema kuwa Kerr yupo katika harakati za kutimuliwa kutokana na kutoiva chungu kimoja na baadhi ya wanene wa klabu hiyo.

Ni kitu cha kushangaza kidogo, kwani Kerr aliyeiwezesha Simba kuzishinda Mbeya City, Stand United na Mgambo zilizokuwa zikiisumbua, anawekewa zengwe hilo.

Habari za ndani ya Simba zilieleza kuwa Kerr ataondoka punde Ligi Kuu itakapoenda mapumziko mwezi ujao, huku pia kukiwa na taarifa kuwa huenda akatimuliwa mapema zaidi. Jana Ijumaa jioni mabosi wa Simba walikutana ili kujadili suala hilo na leo Jumamosi taarifa rasmi inatarajiwa kutolewa.

"Ni kweli tutaachana na Kerr, tumeshindwana katika mambo mengi, kwanza hashauriki, anatoa mazoezi mepesi kwa timu na pia amepata ofa nyingine za maana zaidi nchini Vietnam," alisema mmoja wa mabosi wa Simba ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.

Kwa upande wake kocha Kerr alisema anafahamu kuwa kibarua chake kipo mashakani hasa baada ya kupoteza mechi dhidi ya Prisons na anasubiri uamuzi wa mabosi wake kama watamtimua au la.

"Ni kweli uamuzi nilioufanya dhidi ya Prisons ulitugharimu, niliamua kuwapumzisha wachezaji watano muhimu, nilifanya hivyo kwa kuwa walicheza vibaya katika mchezo na Mbeya City, niliangalia kama tutapata namna nyingine ya kucheza vizuri, ila nayo haikufanikiwa," alisema Kerr.

"Nasubiri nione wanaamua nini, kama nitabaki katika mechi mbili zijazo ni lazima nihakikishe tunapata ushindi, kufanya vibaya katika mechi iliyopita kunatakiwa kutujenga siyo kutubomoa.

"Kuhusu ofa nje siyo kweli, awali nilipata ofa nchini Thailand na Iran lakini nilizigomea, nilitaka kufanya kazi Simba."

Kerr ameiwezesha Simba kufikisha pointi 15 katika mechi saba, wakati msimu uliopita katika mechi kama hizo ilikusanya pointi saba tu na kuwa eneo la chini katika msimamo.

Chanzo: Mwanaspoti
 
soka la Tanzania ni gumu sana. Hata Yanga wanamvumilia Manji kwa kuwa yeye ana nunua amani ya klabu. Ukileta kelele unapingwa pesa unanyamaza . ila sidhani kama manji ameweka system ya uongozi ili mtu mwingine akija asivurunde
 
Manji kajaje sasa? Mibao inawachanganya eeh? Sasa mtatuletea hadi walimu wa cricket
 
SIMBA ikiwa chini ya kocha, Dylan Kerr, msimu huu imezifunga timu tatu ambazo ilishindwa kuzifunga katika misimu miwili iliyopita, lakini imebainika kuwa hata kocha huyo hana muda mrefu Msimbazi, kwani hata akishinda mechi mbili zijazo ni lazima asepe klabuni hapo.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezinasa kutoka kwa chanzo makini kilichopo Msimbazi, zinasema kuwa Kerr yupo katika harakati za kutimuliwa kutokana na kutoiva chungu kimoja na baadhi ya wanene wa klabu hiyo.

Ni kitu cha kushangaza kidogo, kwani Kerr aliyeiwezesha Simba kuzishinda Mbeya City, Stand United na Mgambo zilizokuwa zikiisumbua, anawekewa zengwe hilo.

Habari za ndani ya Simba zilieleza kuwa Kerr ataondoka punde Ligi Kuu itakapoenda mapumziko mwezi ujao, huku pia kukiwa na taarifa kuwa huenda akatimuliwa mapema zaidi. Jana Ijumaa jioni mabosi wa Simba walikutana ili kujadili suala hilo na leo Jumamosi taarifa rasmi inatarajiwa kutolewa.

?Ni kweli tutaachana na Kerr, tumeshindwana katika mambo mengi, kwanza hashauriki, anatoa mazoezi mepesi kwa timu na pia amepata ofa nyingine za maana zaidi nchini Vietnam,? alisema mmoja wa mabosi wa Simba ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.

Kwa upande wake kocha Kerr alisema anafahamu kuwa kibarua chake kipo mashakani hasa baada ya kupoteza mechi dhidi ya Prisons na anasubiri uamuzi wa mabosi wake kama watamtimua au la.

?Ni kweli uamuzi nilioufanya dhidi ya Prisons ulitugharimu, niliamua kuwapumzisha wachezaji watano muhimu, nilifanya hivyo kwa kuwa walicheza vibaya katika mchezo na Mbeya City, niliangalia kama tutapata namna nyingine ya kucheza vizuri, ila nayo haikufanikiwa,? alisema Kerr.

?Nasubiri nione wanaamua nini, kama nitabaki katika mechi mbili zijazo ni lazima nihakikishe tunapata ushindi, kufanya vibaya katika mechi iliyopita kunatakiwa kutujenga siyo kutubomoa.

?Kuhusu ofa nje siyo kweli, awali nilipata ofa nchini Thailand na Iran lakini nilizigomea, nilitaka kufanya kazi Simba.?

Kerr ameiwezesha Simba kufikisha pointi 15 katika mechi saba, wakati msimu uliopita katika mechi kama hizo ilikusanya pointi saba tu na kuwa eneo la chini katika msimamo.

Chanzo: Mwanaspoti

CC. sembo (Kumbuka maneno yangu).
 
Last edited by a moderator:
Nlidhani watamtimua kabla hatuja muapisha lowassa
 
Safari hii leteni kocha kutoka China
 
Nakumbuka sana Mkuu.. ila hizi habari za magazeti si za kuamini sana.. Tuwe na subira tuone kama kuna ukweli wowote.
Lakini kwa Tanzania hivyo ndiyo inavyokuwa. Kuna mzunguko mtakatifu ufuatao: 1. Mechi zinachezwa, matokeo yanapatikana. 2. Magazeti yanasema kocha hafai. 3. Fununu zinazagaa kwamba kocha anatimuliwa 4. Kocha anabadilishwa. 5. Mechi zinachezwa , mzunguko unaendelea.
Ila baina ya fununu kuzagaa na magazeti kutabiri, lolote linaweza kutangulia.
cc. Makoye Matale
 
Haha.. Upo sahihi kabisa Mkuu.. Nimeipenda hiyo cycle ulioianisha.
 
Lakini kwa Tanzania hivyo ndiyo inavyokuwa. Kuna mzunguko mtakatifu ufuatao: 1. Mechi zinachezwa, matokeo yanapatikana. 2. Magazeti yanasema kocha hafai. 3. Fununu zinazagaa kwamba kocha anatimuliwa 4. Kocha anabadilishwa. 5. Mechi zinachezwa , mzunguko unaendelea.
Ila baina ya fununu kuzagaa na magazeti kutabiri, lolote linaweza kutangulia.
cc. Makoye Matale

haha ha haaa.......
 
Back
Top Bottom