Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mentor wangu alikuwa ananipa somo juu ya ishu fulani ilikuwa inanitatiza akanipa mfano wa huyu jamaa kuwa alipata umaarufu kupitia mganga mmoja huko bagamoyo mwisho wa siku akakosea sharti,samahani nimelisahau
Mentor wangu alikuwa ananipa somo juu ya ishu fulani ilikuwa inanitatiza akanipa mfano wa huyu jamaa kuwa alipata umaarufu kupitia mganga mmoja huko bagamoyo mwisho wa siku akakosea sharti,samahani nimelisahau
subiri comment za clouds
Ninavyojua mimi wanamuziki wengi ha Tanzania hawawezi kusimama wenyewe.Yaani wamezoea kufanywa vibarua na vipaji vyao.
Mwinjuma Yupo sema ndio kafulia.
Mkuu hakuna aliyeua kipaji ,bali kila kitabu na zama zake,hivi wapi umesikia kwa hivi sasa muziki wa bendi au bolingobolingo unashadidiwa hapa nchini Tanzania,hebu nitajie kama kuna bendi ambayo ipo na inajazaa nyomi kwa kupiga muziki wa bendi,hao Ngwasuma tu wapo chali,Twanga wapo chali,Msondo ndio usiseme,Sikinde wapo jina sasa huyo Mwinjuma atawikia wapi,uliza akina Ally Choki wapo wapi? Muziki wa wazee nani atausikiliza siku hizi wakati robo tatu ya Watanzania ni vijana,wanaohangaika na nyimbo za Tetema ,au Nyegezi halafu wewe usema Mwinjuma ,nani anamjua Mwinjuma katika kizazi cha sasa?Kwa kifupi hata Mchinga ifufuliwe au sijui Msondo ifufuke hakuna itakayokuwa maarufu,dunia imegeuka,hata hii Bongo fleva kuna siku itakuwa zilipendwa na Domo atasahaulikaHuyu jamaa nakumbuka aliteka sana kipindi cha nyuma katika soko la mziki wa dansi Yaani kusema kweli aliweza sana kuanzia mchinga sound mpaka kwenye bendi za Manyangau twanga sijui huyu jamaa yu wapi!