Kocha wa dunia Mwinjuma kipaji ameua nani

Kocha wa dunia Mwinjuma kipaji ameua nani

Mentor wangu alikuwa ananipa somo juu ya ishu fulani ilikuwa inanitatiza akanipa mfano wa huyu jamaa kuwa alipata umaarufu kupitia mganga mmoja huko bagamoyo mwisho wa siku akakosea sharti,samahani nimelisahau

mentor wako ni mganga wa kienyeji?
 
Siafiki hizo sababu,sababu kubwa bni kuwa huo muziki wa akina Mwinjuma upo ICU na kizazi cha sasa ambacho ndio walio wengi wana aina yao ya muziki,kila kitabu na zama zake,hata isiwe majungu sijui kurogana lakini aina hiyo muziki wa akina Mwinjuma imeshakufa si hata kwenye vyombo vya habari hatusikii nani atasikiliza huo muziki wa wazee ,vijana ndio wengi na ndio wakati wa akina Domo kutamba kwa kuchezesha midomo jukwaani na kuimba tu Nyegezi au tetema wanaingiza mamilioni sasa wewe uimbe Mgumba wakati huu nani atakusikiliza na halafu muimbaji ni mzee kama Mwinjuma?

uko sahihi sana
 
Mkuu hakuna aliyeua kipaji ,bali kila kitabu na zama zake,hivi wapi umesikia kwa hivi sasa muziki wa bendi au bolingobolingo unashadidiwa hapa nchini Tanzania,hebu nitajie kama kuna bendi ambayo ipo na inajazaa nyomi kwa kupiga muziki wa bendi,hao Ngwasuma tu wapo chali,Twanga wapo chali,Msondo ndio usiseme,Sikinde wapo jina sasa huyo Mwinjuma atawikia wapi,uliza akina Ally Choki wapo wapi? Muziki wa wazee nani atausikiliza siku hizi wakati robo tatu ya Watanzania ni vijana,wanaohangaika na nyimbo za Tetema ,au Nyegezi halafu wewe usema Mwinjuma ,nani anamjua Mwinjuma katika kizazi cha sasa?Kwa kifupi hata Mchinga ifufuliwe au sijui Msondo ifufuke hakuna itakayokuwa maarufu,dunia imegeuka,hata hii Bongo fleva kuna siku itakuwa zilipendwa na Domo atasahaulika
Wewe ndo mkweli kuliko wote.
KILA ZAMA NA KITABU CHAKE!
1.Kulikuwa na zama za Mbaraka (Moro Jazz) na Salum Abdalla (Quban Malimba)
2.Ikawepo zama ya Remmy Ongala na Matimila yake.
3.Waliibuka Mlimani Park na Juwata Jazz.
4.Tusiwasahau Marijan Rajabu (Jabali la Muziki na Hemed Manet Ulaya (Chiriku)
5.Au kuna mtu amewasahau Khadija Kopa na Nassima Khamis Kidogo enzi za kilele cha mipasho ya Taarabu?
6.Ameibuka Mzee Yusuph na Issa Kijoti hadi ajali iipoondoa uhai wake na mengi yakasemwa kisha "Mfalme" naye akastaafu!!
7.Tunataka kusahau zama za Justine Kalikawe na Mr.II?
8.Walikuwepo AY na Mwana FA.
9.Kisha ni Ally Kiba na Diamond watoto wa Kigoma waluotengeneza umaarufu na fedha kwa kutumia bifu!!
KILA ZAMA NA KITABU CHAKE!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kila Masika na mbuu wake.
 
Kuna wakati mganga mmoja aliripotiwa na gazeti moja la udaku kuwa anamdai milioni 3 za kumfanya maarufu na asipomlipa hatasikika tena.wiki moja tangu niliposoma habari hiyo nikasikia double m imenunuliwa juu kwa juu tena ikiwa safarini na marehem isihaka kibene....Serengeti sound

Isiaka Kibene mmoja wapo wa wafadhili wa Msondo Ngoma alishafariki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemsikiliza mahojiano yake na watangazaji wa Efm. Jamaa anaamini sana katika ushirikina hatafuti sababu za kisayansi za kuweza kudidimia kimuziki. Inasikitisha sana.
 
Huyu limbukeni sana, alioa mtoto wa watu akaishi nae miezi 3 tu akampa talaka, kisa hawezi kuishi ki..star, yaani mshamba mara anadai halikuwa chaguo lake lilikuwa la mama ake, akili kisoda lazima ayumbe tu, eti alimkabidhi marehemu Amina chifupa mkewe amfundishe kuishi ki star lakini mkewe hakuweza kuelewa, Dar ina mambo!!!!! haahahaaa..Nipishe nipishieee njia ya kupita, sijui alipita kwenda wapi?
 
Nipo hapa naona mnanijadili kumbe mnanikumbuka bado,nafurahi kuyaona haya.....
 
Back
Top Bottom