Kocha wa Fountain Gate: Mimi ni shabiki wa Simba, asema mechi ya leo ni kuonana kwa Simba na Simba

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kuelekea mchezo kati ya Fountain Gate Fc dhidi ya Simba Sc, Kocha mkuu wa klabu ya Fontain Gate Fc, Robert Matano ameweka wazi kuwa yeye kwao Kenya anaitwa Simba na anakwenda kukutana na mnyama mwenzie.

"Mimi ni mpenzi wa Simba toka miaka mingi toka nacheza wakati huo marafiki zangu wanacheza Simba ila pia hata mimi kwetu Kenya naitwa Simba hivyo Simba na Simba tunakutana."

Kocha huyo raia wa Kenya amebainisha hayo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari (Press conference) kuelekea mchezo kati ya wenyeji Fountain Gate Fc dhidi ya Simba Sc utakaopigwa leo Februari 06, 2025 katika dimba la Tanzanite Kwaraa.

Drogba aliwahi kukiri mapenzi makubwa kwa arsenal ila katika washambuliaji walioiadhibu arsenal nae yumo.

Ukiwe professional unaweza kutemganisha mapenzi na kazi, hii itashindikana kwa mtu mpumbavu tu.

Mie leo nipo simba nahangaika na ugali, mixer kucheza ndondo za elfu 30, yanga wanisajili mkataba miaka mi3 mshahara milioni 3 kwa mwezi bado nijidai kuleta mapenzi kwa simba, huo ni unywanywa..
Nitakuwa na mapenzi pale tu ninapopatia pesa.
 
Hakika hili ni jambo la kawaida Kwa nchi za wenzetu
 
Kocha kasema yeye ni simba kwa maana ya umahiri kwenye life aspects anafananishwa na simba ila vyura kwa kutokuelewa kwenye mmejibu swali tofauti. Upeo mdogo
 
Mimi ni mpenzi wa Simba toka miaka mingi toka nacheza wakati huo marafiki zangu wanacheza Simba ila pia hata mimi kwetu Kenya naitwa Simba hivyo Simba na Simba tunakutana."- Robert Matano Coach Fountain Gate FC.
IMG_2671.jpeg
 
Kuelekea mchezo kati ya Fountain Gate Fc dhidi ya Simba Sc, Kocha mkuu wa klabu ya Fontain Gate Fc, Robert Matano ameweka wazi kuwa yeye kwao Kenya anaitwa Simba na anakwenda kukutana na mnyama mwenzie.

"Mimi ni mpenzi wa Simba toka miaka mingi toka nacheza wakati huo marafiki zangu wanacheza Simba ila pia hata mimi kwetu Kenya naitwa Simba hivyo Simba na Simba tunakutana."

Kocha huyo raia wa Kenya amebainisha hayo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari (Press conference) kuelekea mchezo kati ya wenyeji Fountain Gate Fc dhidi ya Simba Sc utakaopigwa leo Februari 06, 2025 katika dimba la Tanzanite Kwaraa.

Bora huyu aliyeweka wazi kuliko mexime anajificha akatupangia wachezaji wa akiba!
 
Wali wa kushiba huonekana kwenye Sahani!
 
Bora huyu aliyeweka wazi kuliko mexime anajificha akatupangia wachezaji wa akiba!
Ata fadlu na benchikha walipanga wachezaji wa akiba na wakatandikwa vile vile kwaiyo akuna maajabu Mexime aliyoyafanya kupanga kikosi cha akiba!
 
Hapa hakuna mechimmoja atakuwa anatimiza tu utaratibu
 
Bora huyu aliyeweka wazi kuliko mexime anajificha akatupangia wachezaji wa akiba!
Maxime timu yake ikifungwa na Simba analipuka kwa hasira, anamwaga povu, kejeli, lawama kwa waamuzi na TFF.
Lakini akifungwa na Yanga huwa mwenye furaha na hutoa majibu ya kimpira, tumezidiwa, wenzetu wana timu nzuri na bra bra nyingiiii
 
Muwafuatilie vizuri wapo wengi sana wa aina hiyo!
 
Back
Top Bottom