Tetesi: Kocha wa Gaborone United, Dimitar Pantev apewa miaka miwili Simba, kutua Dar Oktoba 4, 2025 kuziba pengo la Fadlu

Tetesi: Kocha wa Gaborone United, Dimitar Pantev apewa miaka miwili Simba, kutua Dar Oktoba 4, 2025 kuziba pengo la Fadlu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kocha mpya wa Simba SC, Dimitar Nikolaev Pantev kutoka Bulgaria, amekubali kuanza rasmi kazi yake baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili hadi Juni 2027. Simba imelipa fidia kwa klabu ya Gaborone United ya Botswana ili kumuachia kocha huyo, ambaye anatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam kesho, Oktoba 4, 2025 tayari tiketi yake imeshakatwa.

1759475850148.png
Pantev, mwenye umri wa miaka 49, atakuja na kocha msaidizi mmoja pekee, huku benchi lote la ufundi lililopo sasa likiendelea na majukumu yao hadi mikataba yao itakapomalizika Juni. Klabu imeamua kumpa nafasi Pantev kuamua nani ataendelea naye baada ya kipindi hicho, jambo linaloashiria mipango ya muda mrefu ya usimamizi wake.

Soma: Kocha wa Simba Fadlu Davids atimka, kikosi kurejea nchini bila Kocha

Katika rekodi yake, Pantev tayari ameweka historia kwa kushinda mataji ya ligi akiwa na Victoria United ya Cameroon na Gaborone United ya Botswana. Ujio wake ndani ya Simba unatarajiwa kuongeza ushindani na kuimarisha matumaini ya mashabiki kuona timu hiyo ikirejea katika ubora wake barani Afrika.

=============

1759492004757.jpeg
​
Rasmi klabu ya Gaborone imeachana na kocha wake Dimitar Nikolaev Pantev raia wa Bulgaria, kama inavyosemakana kuwa kocha huyo atajiunga na Simba Sc muda wowote kuanzia sasa.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa kocha Pantev leo asubuhi aliwaaga wachezaji pamoja na wafanyakazi wa klabu hiyo kwenye uwanja wa mazoezi tayari kwa kufungua ukurasa mpya nje ya klabu hiyo aliyojiunga nayo mnamo Januari 2025 na kuiongoza kushinda taji la Ligi Kuu Botswana msimu wa 2024/25.
​
 
Ngoja tuone itakuaje na yeye atakimbia km yule Fadlu au vipi?
 
kule kwengine kilichobaki ni taarifa kwa umma kwa makubaliano ya pande zote mbili tumeachana na aliyekuwa kocha mkuu Bw. Eminem Folz
 
Kwamba yanga kwenye timu zote africa ndio malengo ya simba? Nyie washabiki mlioletwa na wimbi la kubeti ni viazi sana
Kwaiyo unamaanisha nyie "triple mbu" mumerizika na munafurahi kufungwa na mpinzani wako wa jadi mara 6 mfululu?
au munaleta hadithi za sungura hapa ile "sizitaki mbichi hizi".
 
Wewe ni mshabiki maandazi
Pole ndugu yangu najua hiyo timu unayoshabikia inakufanya uwe na hasira, niwe shabiki maandazi, mkate, au shabiki cake, ninachofaham hakuna shabiki duniani anafurahi kupoteza mechi ya dabi,
hiyo kujifanya muna malengo ya kimataifa sana huku mukijifanya kufungwa na yanga kwenu sio tatizo hizo ni porojo tu.
 
Back
Top Bottom