Kocha wa Simba atimuliwe

Kocha wa Simba atimuliwe

Bodi ya Simba wao ndio wataamua Sven aendelee au aondoke sisi wengine tutaendelea kuonyesha mapungufu ya kocha na wachezaji kwa ujumla wao. Kwa haraka haraka nilichokiona Simba vs Ruvu: -
1. Manula bado ana makosa yale yale kwenye kona na krosi. Kwenye goli Ruvu walilofunga alifanya kosa moja kubwa sana la kiufundi ambalo ni watu wenye kuujua mpira vizuri waliliona. Kona inataka kupigwa na mchezaji wa Ruvu halafu kipa unasukumana na mshambuluaji wa Ruvu halafu ategemee apate "motion" ya kuruka kuokoa mpira wa juu. Kwa kipa makini kwanza angemuita beki wake mbabe aje apambane na huyo mshambuliaji, pili angepiga kelele na kuwaita waamuzi ili waamuzi waweke macho yao kwake kuwa anasukumwa kama hivyo haitoshi angejiangusha (kabla kona haijapigwa) pale alipoguswa na huyo mshambuliaji hata kama hakukuwa na nguvu hiyo ya kumwangusha. Erasto na Wawa nao walikuwa wamesimama tu kama milingoti tangu wakati Manula anapambana ma mshambuliaji wa Ruvu mpaka mtu anapiga kichwa anafunga
2. Upande wa kushoto alipokuwa Kichuya na Gadiel walikuwa wanachelewesha sana mipira kwenda mbele japo Kichuya ndie aliefunga goli. Wote wawili walikuwa wanapoozesha mipira sana halafu walikuwa na "back pass" nyingi ambazo zilikuwa zinawasaidia Ruvu kujipanga upya.
3. Muzamiru na Dilunga mechi iliwakataa tangu mwanzo mwa mchezo. Ilihitajika mabadiliko ya mapema sana. Sawa kwa Dilunga walikuwepo watu wa kumbadili lakini kwa Muzamiru Fraga hakuwa benchi na Mkude ni mgonjwa.
4. Timu nzima ilikuwa inacheza vizuri kiasi mpaka nusu ya uwanja baada ya kuvuka nusu ya uwanja timu ilikuwa inakosa kasi na ubunifu kuelekea kwenye goli la Ruvu.
5. Sven ameshindwa kabisa namna nzuri ya kuwatumia Boko na Kagere ndio maana mpaka sasa ile ladha ya kuangalia fowadi ya Simba kama mwaka jana haipo tena. Kagere anatakiwa asitoke sana nje ya boksi la 18 la adui kwa dakika zote 90 kama alivyokuwa anamtumia Uchebe na wakati huohuo Boko anatakiwa azunguke kushoto na kulia kwa Kagere kuwachanganya mabeki wa timu pinzani. Kagere ni mzuri sana kwenye "second balls" na pia anawafanya mabeki wa timu pinzani wamchunge yeye hivyo kutoa nafasi kwa wachezaji wengine kufunga. Boko ni mzuri kwenye kukokota mpira kuelekea kwenye lango la adui.
6. Benchi la ufundi - hili ndio lililosababisha timu ikashindwa kupata ushindi kwani tokea mchezo unaanza kule mbele timu ilikuwa imepooza sana lakini walishindwa kufanya mabadiliko kwa wakati na kwenye benchi kulikuwa na "viberenge" Deo Kanda, Kahata na Miraji Athumani . Upande wa kushoto alipokuwa Kichuya na Gadiel nao ulikuwa mzito sana kushambulia kwa kasi lakini bado mabadiliko yalifanyika kwa kuchelewa sana.
 
mimi sitaki kuwa mnafiki,huyu kocha hamna kitu. anakosa plan B kabisa. mechi zote za Yanga,na hata hiyo ya Ruvu
Bora wewe umekuwa muwazi. Sisi watanzania tunapenda sana kuwadharau makocha wazawa na kuwatukuza wazungu hata kama uwezo wao mdogo. Lakini ni hawahawa wakina Mexime, Amri Said, Mayanga, Bares, Katwila, Rishard. n.k. ndio wanawanyoosha makocha wazungu kila siku kwenye ligi. Kwa Simba hii mpe Jamhuri, Matola au Amri Said na Yanga mpe Mexime au Adolf Rishard halafu wape mishahara na marupurupu nusu ya wanaolipwa hao makocha wazungu nina uhakika kwenye ligi ya mabingwa mwaka wa kwanza na wa pili watapata shida kidogo lakini baada ya hapo timu za Tanzania zitafanya vizuri sana. Tunataka makocha wetu wawe wazuri lakini lazima tuwaache kwanza wakanyooshwe kwa msimu mmoja au miwili mfululizo kwenye mashindano ya Afrika ndipo tutapata ubora wao.

Ndio maana mara nyingi sana nasema kwa kocha wa Simba bodi ndiyo yenye maamuzi ya mwisho lakini kwa hakika kabisa ubora wa wachezaji ilio nao Simba ndio inamfichia aibu huyu mzungu. Kwa mfano mechi ya juzi na Ruvu pamoja na ubora wa Ruvu na kucheza mpira vizuri sana kuizidi Simba Kocha alishindwa kuyaona mapungufu na kufanya mabadiliko ndani ya dakika 20 - 30 za mwanzo. Na alikosa kabisa "plan B" ya kuweza kuwadhibiti Ruvu zaidi kudra za mwenyezi Mungu ndizo ziliikoa Simba isipate kichapo. Mimi shabiki tu wa kawaida wa mpira lakini niliona mapungufu mengi yaliyohitaji mabadiliko ya wachezaji ndani ya dakika hizo 20 mpaka 30 baada ya mchezo kuanza. Na Ruvu walikosa umakini kidogo sana kwani walikuwa na uwezo wa kuimaliza ile mechi ndani ya dakika 20 za mwanzo kwa kupata angalau goli 3 za haraka haraka.
 
Haya ndio mapungufu makubwa ya kocha wetu anashindwa kuwa na plan b pale anapoona game plan imeshindikana yanga walitufunga si kwa sababu ni wazuri zaidi yetu bali kocha wao alishatusoma mapungufu yetu
 
Bora wewe umekuwa muwazi. Sisi watanzania tunapenda sana kuwadharau makocha wazawa na kuwatukuza wazungu hata kama uwezo wao mdogo. Lakini ni hawahawa wakina Mexime, Amri Said, Mayanga, Bares, Katwila, Rishard. n.k. ndio wanawanyoosha makocha wazungu kila siku kwenye ligi. Kwa Simba hii mpe Jamhuri, Matola au Amri Said na Yanga mpe Mexime au Adolf Rishard halafu wape mishahara na marupurupu nusu ya wanaolipwa hao makocha wazungu nina uhakika kwenye ligi ya mabingwa mwaka wa kwanza na wa pili watapata shida kidogo lakini baada ya hapo timu za Tanzania zitafanya vizuri sana. Tunataka makocha wetu wawe wazuri lakini lazima tuwaache kwanza wakanyooshwe kwa msimu mmoja au miwili mfululizo kwenye mashindano ya Afrika ndipo tutapata ubora wao.

Ndio maana mara nyingi sana nasema kwa kocha wa Simba bodi ndiyo yenye maamuzi ya mwisho lakini kwa hakika kabisa ubora wa wachezaji ilio nao Simba ndio inamfichia aibu huyu mzungu. Kwa mfano mechi ya juzi na Ruvu pamoja na ubora wa Ruvu na kucheza mpira vizuri sana kuizidi Simba Kocha alishindwa kuyaona mapungufu na kufanya mabadiliko ndani ya dakika 20 - 30 za mwanzo. Na alikosa kabisa "plan B" ya kuweza kuwadhibiti Ruvu zaidi kudra za mwenyezi Mungu ndizo ziliikoa Simba isipate kichapo. Mimi shabiki tu wa kawaida wa mpira lakini niliona mapungufu mengi yaliyohitaji mabadiliko ya wachezaji ndani ya dakika hizo 20 mpaka 30 baada ya mchezo kuanza. Na Ruvu walikosa umakini kidogo sana kwani walikuwa na uwezo wa kuimaliza ile mechi ndani ya dakika 20 za mwanzo kwa kupata angalau goli 3 za haraka haraka.
Simba ni timu kubwa sana kwa makocha wazawa hawa makocha wazawa wanaweza mechi za kukamiana ila sielewi kwanini kocha aliwaacha dilunga na mzamiru muda mrefu wakati ilionekana game imewakataa halafu mzamiru hawezi kucheza kiungo mkabaji kwanza badala ya kupokonya mpira yete ndio alikuwa anapokonywa wakati dilunga badala ya kulisha wafungaji yeye alikuwa anawaza kufunga matokeo yake kagere akageuka mchezeshaji hata kama nafasi hana boko alikuwa anashindwa kukaa sehemu sahihi
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa Simba ni timu kubwa lakini je kocha waliyenaye sasa hivi ana uwezo kulingana na ukubwa wa timu ya Simba? Je kocha walinaye sasa hivi anawazidi viwango kwa kiasi gani makocha wazawa? Je unafahamu kuwa makocha wazawa King Kibaden na Tito Mwaluvanda walizifanyia nini Simba na Yanga kwenye mashindano ya Afrika kipindi cha nyuma?. Tusiwadharau makocha wazawa na kutukuza wageni wakati hawa hawa wazawa wanawanyoosha hao wazungu kila week end hapo shamba la bibi. Tuwapitishe kwenye tanuru la mashindano ya Afrika kwa miaka miwili mfululizo huku tukiwapeleka kozi na kuwalipa hata nusu ya mishahara ya hao wazungu nadhani tutapata wakina "Ibenge" wetu hapa kama ilivyo Kongo. Kama kiwango cha kocha mzungu hakipishani sana na cha kocha mzawa ya nini kuingia gharama kubwa ya kumuajiri mzungu badala ya kumpa timu kocha mzawa.

Kwangu mimi binafsi ukiniambia Lechantre au Aussems nitakubali ni makocha wakubwa kwa sababu unaona timu ilikuwa inacheza kwa mfumo fulani na mbinu tofauti tofauti. Timu ikizidiwa ilikuwa inabadilisha mfumo humo humo ndani ya uwanja wakati mwingine bila hata ya kubadilisha mchezaji/wachezaji wa kwenye benchi. Any way tuiachie bodi ya Simba kwani yenyewe ndio wanajua zaidi kuhusu benchi lao la ufundi hasa ukizingatia Kaduguda ni kocha "by profession"
 
Tuna wachezaji wazuri ila hatuna kocha ,tukiacha unafki tunaweza tusifikie tulipofikia mwaka juzi champion cup,...unaona kabisa kuna vitu hana ,nadhani pia hana skills sana,alikuja na droo nyingi na magoli machache,watu wakapigwa kelele,huyu kocha mechi inayofuata na yanga hata dro ikitokea atatimuliwa
mimi sitaki kuwa mnafiki,huyu kocha hamna kitu. anakosa plan B kabisa. mechi zote za Yanga,na hata hiyo ya Ruvu
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa Simba ni timu kubwa lakini je kocha waliyenaye sasa hivi ana uwezo kulingana na ukubwa wa timu ya Simba? Je kocha walinaye sasa hivi anawazidi viwango kwa kiasi gani makocha wazawa? Je unafahamu kuwa makocha wazawa King Kibaden na Tito Mwaluvanda walizifanyia nini Simba na Yanga kwenye mashindano ya Afrika kipindi cha nyuma?. Tusiwadharau makocha wazawa na kutukuza wageni wakati hawa hawa wazawa wanawanyoosha hao wazungu kila week end hapo shamba la bibi. Tuwapitishe kwenye tanuru la mashindano ya Afrika kwa miaka miwili mfululizo huku tukiwapeleka kozi na kuwalipa hata nusu ya mishahara ya hao wazungu nadhani tutapata wakina "Ibenge" wetu hapa kama ilivyo Kongo. Kama kiwango cha kocha mzungu hakipishani sana na cha kocha mzawa ya nini kuingia gharama kubwa ya kumuajiri mzungu badala ya kumpa timu kocha mzawa.

Kwangu mimi binafsi ukiniambia Lechantre au Aussems nitakubali ni makocha wakubwa kwa sababu unaona timu ilikuwa inacheza kwa mfumo fulani na mbinu tofauti tofauti. Timu ikizidiwa ilikuwa inabadilisha mfumo humo humo ndani ya uwanja wakati mwingine bila hata ya kubadilisha mchezaji/wachezaji wa kwenye benchi. Any way tuiachie bodi ya Simba kwani yenyewe ndio wanajua zaidi kuhusu benchi lao la ufundi hasa ukizingatia Kaduguda ni kocha "by profession"
Huyu kocha amekuja Simba kutengeneza cv sio kocha wa kutegemea kufika mbali kwenye michuano mikubwa, kuhusu makocha wazawa wengi wamebweteka Kibadeni au Boniface mara nyingi wanasubiri kufundisha simba na yanga leo hii tuna makocha wengi toka Burundi ni makocha wangapi wametoka hapa kwenda kufundisha nje ya Tanzania lakini makocha hata hawa wanaochipukia hawaendi kusoma kama zamani wanasubiri vikozi vya wiki mbili tatu kwa kifupi hawana moyo wa kujiendeleza watoke nje wafundishe timu zao zikifanya vizuri wataaminiwa Boniface alipigiwa debe timu ya taifa na akapewa mshahara mzuri lakini tulipata kipigo cha aibu Algeria
 
Back
Top Bottom