Kocha wa Simba ndio tatizo na hakika hatutofuzu, hana plan B kabisa, wachezaji wa kuamua mechi unawaweka benchi

Metronidazole 400mg

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
1,177
Reaction score
2,553
Ndio sijakosea, ni kocha anaye tabirika, Al Mary sio timu ya kutisha kivile ila wenzetu walishamsoma kocha Hana mbinu mbadala.

Hata kikosi chake kinatabirika na nitakutajia

Camara
KAPOMBE
ZIMBWE
Chamoue
Hamza
Ngoma
Kagoma
Kibu
Ahoua
Ateba
Mpanzu

Akibadilisha mchezaji hata mmoja hapo nipo paleeee mnishtue na makofi.

In short huyu kocha hamna kitu, mchezaji valentin Nouma sijawahi kuelewa kwanini hamchezeshi,

Mukwala yupo kwenye top form recently, ila anapewa dakika5 za mwisho mbele ya mchezaji ambaye ni mzigo ndani ya timu.

Niishie hapa.

NB:Nilitamani na mimi niweke ahadi nzito ya kupigwa Ban kama kocha atakuja na kikosi tofauti na nilichotaja hapo juu ila utoto huo ndio sinaga, kwa hiyo moderators wa JF Cookie Active mtulie kwanza
 
Nilitamani na mimi niweke ahadi nzito ya kupigwa Ban kama kocha atakuja na kikosi tofauti na nilichotaja hapo juu ila utoto huo ndio sinaga, kwa hiyo moderators wa JF @Cookie @Active mtulie kwanza
Unaogopa unachezea ban hao hua hawatanii
 
Kuna siku nilimuona Mzamiru Yassin kwenye benchi! Mpaka nilishangaa! Aishi Manula hata hajulikani kama ni mchezaji wa simba! Kila siku wachezaji wanaocheza ni wale wale! Siyo kombe la shirikisho la CRDB, siyo mechi za ligi kuu! Siyo kombe la luza!!

Nadhani kocha wa Yanga anastahili pongezi kwenye kuwapa nafasi wachezaji wote kucheza.
 
Hakuna siku Fadru aliponiudhi kama Tarehe 2 April 2025.

1. Kumchezesha Ahoua Kwenye No 10 Mchezo wa Ugenini na Amuache benchi Debora ambaye angekuwa na Msaada zaidi kwenye mchezo wa ugenini.

2. Kuchelewa kufanya Substitution wakati wachezaji wake wamechoka. Na kupelekea kufungwa magoli mengine.

3. Kusajili Mchezaji Mmoja Dirisha Dogo , Hii nayo ilinishangaza sana. Nikaamini jamaa uwezo wake ni Mdogo ndio maana alikuwa kocha Msaidizi huko kote alipotoka.


Fadru ni Mpumbavu sana
 
Inasikitisha sana
Kituko zaidi, ile mechi na Azam. Mpaka dk ya 70, wachezaji wake walikuwa wanaonyesha dhahiri kuwa wamechoka. Mwenzie akaingiza nguvu mpya, yeye walaaa! Goli linafungwa ile dk ya 88, ndipo akaingiza wachezaji zaidi ya mmoja, kwa wakati mmoja, ikiwa ameshachelewa!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Mwee! Mbona timu nyingi sana zina shinda ubingwa na team yao unaijua from no.1 to 11. Sema nyei quality ya nusu na final hamna bwana. Kocha mzuri tuu. Mourinho kashinda treble na inter 11 yake inajulikana kila leo na sub zake zinajulikana...ttotal 16 players ndio waliwapa ubingwa inter
Vile vile barca timu ya ukweli ya xavi iniesta pep
 
Mimi leo hata siongei kabisa na zaidi hii mechi siangalii kabisa ..Bado nayapenda maisha yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…