Kocha wa Simba simwelewi

Wachezaji pia wanatakiwa kuwa serious na Mechi,

Tunapoelekea Kutwaa Ubingwa inatakiwa kuweka bidii mchezoni,pamoja na malengo.

Kila anayetokea ni kuchezea Kichapo,

Sasa hii mambo ya Kufungwa na kagera ishakuwa mazoea.
Hata choko huanza kiutani utani mwsho huzowea!
 
Kwa mechi ya leo kocha hasilaumiwe wachezaji wetu wakubwa tena tegemeo la timu wanautoto mwingi jiulize chama amepata nafasi ngapi za kupasia wenzake ili wafunge hatoi huo mpira anataka kufunga yeye unaweza dhani amebet ili simba afungwe.
Njoo kwa couribly ndiyo takataka kabisa dk za mwisho zile hataki kutoa pasi kwa kagere anataka kufunga mwenyewe.
Bocco na okwi wote hawa kila mtu anataka kufunga badala ya kumpasia aliyepo nafasi nzur wao wanapiga bora mpira uende
 
Wamekutana na Katererooo, wamechanganyikiwa. Hapo bado watoto wa shule kesho kutwa, alafu kuna wale wafanyabiashara wa Musoma
Wiki mbili bila kucheza mechi hata moja ya ligi na hakuna mechi za Mataifa!! Only in Tanzania.
 
No. Mimi tangu mwanzo sikumkubali Uchebe na nilipata ahueni pale Kitambi alipokuja.
Sasa kwani kitambi katimuliwa? Wabongo wengi tunajifanya wajuaji yaani timu isifungwe tayari lawama kocha hafai ndio maana makocha hawahawa wakienda maeneo mengne afrika wanafanya vizuri tu.Huwezi shinda mechi zote then unasema hata timu ikishinda ni juhudi tu za wachezaji sasa ikifungwa kwanini usizungumzie uzembe wa wachezaji unamnanga kocha utadhani Simba ndio klabu pekee afrika kufungwa
 
Moja ya kitu alichokizungumza kocha wa TP Mazembe kuhusu timu ya Simba.
Ni kuhusu timu ya Simba kuwa na wachezaji wengi wazee.
Kwa mfano
Okwi - anamchango mkubwa kwa timu lakini uwezo wake kwa sasa Ni wakucheza kipindi kimoja cha dakika 45
Wawa- Naye umri umeenda sana niwa dakika 45
Colibaly - Ni mzee pia kuna siku anajitutumua na kuna siku mishipa inakataa.
John Boko - naye jioni tayari nafasi kumi anafunga moja.
Niyonzima- naye jioni inamnyemelea, hawezi kabisa kufunga goli.
Mkude - anajizeesha mwenyewe kwa aina ya maisha anayoishi, anajichosha na mambo ya mtaani.
Asante Kwasi - Naye kachoka
NK

Kikosi cha Simba kwa sasa kianze hivi.
Ï Aish Manula
2 Nikolaus Gyan
3 Muhamed Hussein
4 Juuko sub Bukaba, Mlipili
5 Erasto Nyoni sub Wawa
6 Kotei sub Mkude
7 Dilunga sub Mdemla
8 Chama sub Niyonzima
9 Boko first half, Okwi second
10 Kagere / sub Salamba
11 MO Rashidi sub dogo Ally

Ni mapendekezo yangu tu Kocha ndiye anayeona kuwa nani anafaa.
Ila anachelewesha Sana kufanya Sub.
 
Ilikuwa hivo hivo tulipoenda Congo kucheza na AS Vita kocha wa AS Vita alisema tuligungwa 5 kwa sababu waliona mchezo wa simba niwa pasi fupi fupi zisizo na maana.
 
Tatizo liko kwa wachezaji, Uwezo wao umeishia hapo. Tunahitaji wachezaji wa kiwango cha matokeo tunayohitaji.
 
Usimjadili kocha maana huwa anastukia tu timu imeshinda. Zote zinachezwa nje ya uwanja.
 
Kocha kapata kigugumizi kujibu.. Alivyoulizwa uchovu umesababisha kichapo. Atawajibu nini wakina Manara wakati alipewa fungu asajili wachezaji vijana January
 

Kama hili lilitokea unamlaumuje kocha kwa mfano
 
Timu ina wenyewe lakini kama shabiki wa Simba ni lazima kocha abadili aina ya upangaji timu na uchezaji ama yeye mwenyewe abadilishwe.

Safu ya Ulinzi ya Simba inacheza ovyo kabisa!
Mkuu simba mpaka hapo simba ilipofika ni juhudi za wachezaji binafsi kwa kiasi kikubwa. Kazi anayoifanya uchebe matola anaweza kuifanya kwa ufanisi zaidi. Ukitaka kugundua hilo angalia game plan yake, hana mbinu mbadala kabisa na anaamini katika mazoea. Anashindwa kabisa kuwapa nafasi kina salamba, rashid juma, mzamiru, kurefresh kikosi. Simba haina pace kwenye flanks unashindwa vipi kumtumia gyan na rashidi juma. Okwi umri umempa mkono , chama kwangu ni mchezaji wa kawaida hana discpline na mpira. Na ukiangalia kwa ukaribu utaona viungo wa simba wana makosa yale yale, yaani hakuna demand kocha anataka nini kutoka kwao sawa na mabeki wetu, ball watching defenders
 
Falsafa ipi mkuu? Hivi toka uchebe aje kuna falsafa ambayo inaweza ikaielezea simba? Unaikumbuka simba ya pierre lechantre? kupata tathmin nzuri ,Tafuta mechi 3 za simba chini ya mfaransa yule na chukua tano za uchebe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…