Kocha wa Taifa Stars asema tumefungwa magoli machache sana

Deogratius n

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2015
Posts
1,193
Reaction score
254
Akiongea kwa ujasiri mkubwa Martin Nooij kocha mkuu wa taifa stars amesema timu yetu imefungwa magoli machache sana na timu ya taifa ya Misri.

Nakumbukua kauli yake kabla ya mechi alisema amejiandaa timu vizuri kwa kucheza pasi za haraka haraka na anamatumaini makubwa ya kupata ushindi.

Binafsi naona huyu kocha haelewi anachokifanya na ametuona sisi watanzania ni wapumbavu sana. Huyu kocha alitakiwa aondokee kulekule misri asirudi hapa tanzania.

Kitendo cha Jamal Malinzi kumpa fursa ya mwisho katika mashindano ya CHAN kitamfanya kocha huyu ajione mungu mtu.
 
Mtabadili kila aina ya makocha, tatizo si makocha tatizo ni uongozi wa TFF.

Kiongozi wa TFF Jamal Malinzi ni mbovu na wanaomsaidia wote ni wabovu, hawana ubunifu na hawana muono wa kujuwa wapi pakurekebisha, wewe fikiri kiongozi wa mpira wa karne hii anatangaza kuwa tatizo ni jezi! Khaa!

Tanzania soka linaweza kukuwa kwa haraka sana, ni ubunifu na mipango ya haraka na ya muda mrefu inayotakiwa ifanyike.

Hawa viongozi wa soka wamefikia mwisho wa fikra zao, hawawezi, hawawezi, hawawezi.

cc Bishanga
 
kwa hiyo unashauri jamal malinzi nae aachie madaraka?
 
Mtabadili kila aina ya makocha, tatizo si makocha tatizo ni uongozi wa TFF.

Kiongozi wa TFF Jamal Malinzi ni mbovu na wanaomsaidia wote ni wabovu, hawana ubunifu na hawana muono wa kujuwa wapi pakurekebisha, wewe fikiri kiongozi wa mpira wa karne hii anatangaza kuwa tatizo ni jezi! Khaa!

Tanzania soka linaweza kukuwa kwa haraka sana, ni ubunifu na mipango ya haraka na ya muda mrefu inayotakiwa ifanyike.

Hawa viongozi wa soka wamefikia mwisho wa fikra zao, hawawezi, hawawezi, hawawezi.

cc Bishanga

Naunga mkono hoja.

cc Bishanga
 
Mh.Mch.Msigwa:watu wale wale wenye akili zile zile hawawezi kuleta mabadiliko
 
Mtabadili kila aina ya makocha, tatizo si makocha tatizo ni uongozi wa TFF.

Kiongozi wa TFF Jamal Malinzi ni mbovu na wanaomsaidia wote ni wabovu, hawana ubunifu na hawana muono wa kujuwa wapi pakurekebisha, wewe fikiri kiongozi wa mpira wa karne hii anatangaza kuwa tatizo ni jezi! Khaa!

Tanzania soka linaweza kukuwa kwa haraka sana, ni ubunifu na mipango ya haraka na ya muda mrefu inayotakiwa ifanyike.

Hawa viongozi wa soka wamefikia mwisho wa fikra zao, hawawezi, hawawezi, hawawezi.

cc Bishanga

Very brilliant point my dear

Ndio maana nakupendaga

Tatizo ni malinzi...wala sio kocha...siku zote hua nasema....ni sababu ipi ilimfanya malinzi kumtimua Kim?

Kim alishakaa na timu yetu kwa zaidi ya miaka 5...alishatengeneza timu na timu ilikua ina mwelekeo...nini ilikua sababu ya kumtimua kim?
Jamal Malinzi hana hata moja alilofanikisha la kuendeleza mpira...ivi kweli mtu mzima kiongozi wa TFF unajidai eti kwa kubadili Jezi? Jezi? seriously? eti na kutoa tuzo? Tuzo za nini wakati mpira wenyewe hakuna.

Inabidi ifike mahali malinzi aondoke

Nimefurahishwa sana na wapenzi wa soka kulipiga mawe gari la stars
 
DSC03839.jpg
 
Ili timu ya taifa ifanye vizuri, mfumo wa uongozi na vipaumbele vibadilishwe. Kwa kufanya hivyo itachukua 10-15yrs hadi kufikia mafanikio.

Invest in youth kuanzia huko mashuleni na centers zingine za michezo, build conducive infrastructure na train waalimu, rasilimali fedha iwe ya kutosha....baada ya hapo work continuously 10-15yrs, haya mambo ya BRN while system ni zile zile tutabaki hivi hivi....
 
Amma aachie madaaraka amma abadilike namna ya uongozi wake haraka sana. There is always a chance for improvement.

Hapana, yule hawezi kuimprove...

Nashauri arudi Chit Chat tunyang'anyane vibinti. Kwenye fani hii hakuna atakayemlaumu. Kafuzu na Kabobea.

Mpira awaachie kina Leodgar Tenga.
 
tunasema mengi yawezekana mifumo yetu ni mibovu ila kama kocha alienda misri kutafuta ushindi basi nadhani hafai.

binafsi sijui kufundisha kupiga chenga lakini kama ningeulizwa mbinu za kwenda nazo misri ilikuwa kwenda kutafuta sare tu na sare hiyo kama ningekuwa kocha ningeitafuta kwa kupanga washambuliaji watatu na the rest mabeki.

hapo tunahakikisha ndani ya robo ya kwetu misri hawachezi mpira na tunashambulia kwa kounter attack tu.

lazima uangalie adui yako ana nguvu gani na uweke malengo yanayofikika na kupanga kumfunga misri nyumbani kwao ukaenda kubahatisha inaonyesha mipango ilikuwa ya kucheza kamali.

Akiongea kwa ujasiri mkubwa martn noij kocha mkuu wa taifa stars amesema timu yetu imefungwa magoli machache sana na timu ya taifa ya misri. Nakumbukua kauli yake kabla ya mechi alisema amejiandaa timu vizuri kwa kucheza pasi za haraka haraka na anamatumaini makubwa ya kupata ushindi. Binafsi naona huyu kocha haelewi anachokifanya na ametuona sisi watanzania ni wapumbavu sana. Huyu kocha alitakiwa aondokee kulekule misri asirudi hapa tanzania. Kitendo cha jamal malinzi kumpa fursa ya mwisho katika mashindano ya chan kitamfanya kocha huyu ajione mungu mtu.
 
Hapana, yule hawezi kuimprove...

Nashauri arudi Chit Chat tunyang'anyane vibinti. Kwenye fani hii hakuna atakayemlaumu. Kafuzu na Kabobea.

Mpira awaachie kina Leodgar Tenga.

Basi Jamal Malinzi aachie uongozi TFF kwa wanaoweza. Anawaumiza sana Watanzania.

cc Bishanga
 
Naungana na wewe ila kwakuongezea pia nadhani Vijana wetu hawahitaji Kocha wa kigeni tu bali wanahitaji kujengwa kisaikolojia pia, kuupenda mpira, kuwa na mtazamo chanya juu ya kila wanachokifanya, waelimishwe kuwa wanafanya hivyo kwa maslahi yao na ya Taifa.

Wakifundishwa na kuelezwa mambo kama haya na wakayakubali na kuyaelewa itabidi wabadilishe hata namna yao ya maisha, maisha ya starehe na U-superstar wa bongo, maisha ya kujiona kuwa wao ni zaidi ya wengine, wajitume na waamini kila mara kuwa mafanikio waliyonayo ni kidogo na wanahitaji zaidi. Huyo ndio aina ya Kocha au waalimu tunaowahitaji kwa sasa, sio mwalimu wa kufundisha upigaji chenga.
Mtabadili kila aina ya makocha, tatizo si makocha tatizo ni uongozi wa TFF.

Kiongozi wa TFF Jamal Malinzi ni mbovu na wanaomsaidia wote ni wabovu, hawana ubunifu na hawana muono wa kujuwa wapi pakurekebisha, wewe fikiri kiongozi wa mpira wa karne hii anatangaza kuwa tatizo ni jezi! Khaa!

Tanzania soka linaweza kukuwa kwa haraka sana, ni ubunifu na mipango ya haraka na ya muda mrefu inayotakiwa ifanyike.

Hawa viongozi wa soka wamefikia mwisho wa fikra zao, hawawezi, hawawezi, hawawezi.

cc Bishanga
 
Pia jambo lingine ni kuhakikisha kuwa Timu zetu zinaundwa na wachezaji wetu (nazungumzia clubs), hili la kuruhusu wachezaji wa kigeni saba au nane na kuendelea ni kuwadumaza viojana wetu, hawana cha kujifunza. Ndio maana inapokuja suala la kwenda kucheza nje ya nchi kwa mechi kama hizi hatufanyi vizuri kwa kuwa sisi tumeshalemazwa na wachezaji wa kiegni, hawa wakwetu wanakosa uzoefu.........inauma
 
Huyu Jamal Malinzi angekuwa muungwana wala asingesubiri wadau tutoe povu ndo aelewe kuwa ameshashindwa kutusaidia hivyo aachie ngazi!tumekosa hata ushindi wa sare...sasa lengo letu linaonekana ni kutofungwa magoli mengi!
 
Last edited by a moderator:
Huyu kocha sasa ameshazoea akili za kiCCM sasa
 
Pia jambo lingine ni kuhakikisha kuwa Timu zetu zinaundwa na wachezaji wetu (nazungumzia clubs), hili la kuruhusu wachezaji wa kigeni saba au nane na kuendelea ni kuwadumaza viojana wetu, hawana cha kujifunza. Ndio maana inapokuja suala la kwenda kucheza nje ya nchi kwa mechi kama hizi hatufanyi vizuri kwa kuwa sisi tumeshalemazwa na wachezaji wa kiegni, hawa wakwetu wanakosa uzoefu.........inauma

Wanaruhusu wachezaji wa kigeni wengi wakati vijana wanaomaliza copa cocacola, airtel rising star au michuano ya rollingstone wanakosa timu kubwa za kuwachukua...
Hao wachezaji saba utakuta watano wamesajiliwa kwa mbwembwe kumbe ni vimeo hatari sana...
Jamal Malinzi na wenzake wafikirie hili kwa makini sana, hatujafika levels za afrika kusini au nchi za kiarabu kwenye soka...
 
Yeah hio ndio Point yangu, kwa mfano, wako wapi wale Vijana ambao ndio walikua Mabingwa kwenye World Cup ya watoto waishio mazingira hatarishi? Wako wapi>? Wanafanya nini? Iko wapi ile hazina??

Michael Mazalla: TANZANIA YASHINDA KOMBE LA DUNIA KWA WATOTO WA MITAANI

Back
Top Bottom