Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Ronald Koeman amejiuzulu rasmi kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi baada ya timu hiyo kutolewa kwenye Kombe la Dunia 2026 katika hatua ya 32 bora kufuatia kufungwa na Morocco kwa mikwaju ya penalti.
Koeman ametangaza uamuzi huo siku moja baada ya kipigo hicho kilichokatisha safari ya Uholanzi kwenye mashindano hayo.
Katika mchezo huo, Uholanzi ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 hadi dakika za mwisho kutokana na bao la Cody Gakpo. Hata hivyo, Morocco ilisawazisha mabao katika dakika za nyongeza kupitia Issa Diop, kabla ya kushinda kwa mikwaju ya penalti.
Koeman amesema kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa kutwaa Kombe la Dunia, lakini haikutimia. "Ndoto hiyo haikutimia. Hata hivyo, ninajivunia kila kitu ambacho soka limenipa, watu ambao nimekutana nao katika safari yangu, na nafasi ya kuifanya shauku yangu kubwa kuwa taaluma yangu,” aliandika.