Kocha wa Yanga, Ramovic aingia ubaridi, asema ni mara yake ya kwanza ligi ya Mabingwa

Kocha wa Yanga, Ramovic aingia ubaridi, asema ni mara yake ya kwanza ligi ya Mabingwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kuelekea katika mechi za kimataifa katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Kocha Mkuu wa Yanga Sc, Sead Ramovic, amezungumza na waandishi wa Habari, akisema!
1732531999041.png
"Hii ni mara yangu ya kwanza kwenye ligi ya mabingwa. Ni jambo la kheri sana kwangu kushiriki mashindano haya makubwa nikiwa na timu kubwa ya Young Africans SC. Falsafa yangu kubwa ni nidhamu na kujituma. Napenda kuona wachezaji wakicheza kama timu, haijalishi unatumia mfumo gani kama wachezaji wako hawana umoja ni ngumu kupata matokeo’’

Yanga inatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika uwanja wa nyumbani wa Benjamin William Mkapa.
 
Lugha ya Mpira wewe unasema ubaridi,,kwaiyo ulitaka aseme tunaenda kumfunga Al hilal? Lugha ya kumheshimu mpinzani wako ni muhimu kwa kocha ambae ni profeshno ata kama timu yako na mbinu zako zikiwa Bora kumzidi
 
Back
Top Bottom