Kocha wetu stars anataka kutupanda kichwani atimuliwe kabla mechi haijaanza!

Kocha wetu stars anataka kutupanda kichwani atimuliwe kabla mechi haijaanza!

Yale aliyosemaga RPC wa Dodoma(Muroto) kipindi Cha Mwendazake ndio mtakishuhudia leo
 
Huyu kocha ameajiriwa kuja kufundisha soka, sio kujifunza soka! Analipwa pesa nyingi sana kwa mwezi na gharama zote za malazi pamoja na usafiri ili tu aje afundishe soka! Yeye ni mtaalamu wa benchi la ufundi!

Iweje Leo anasema ameenda afcon kujifunza? Tunamlipa ili akajifunze? Au tunamlipa afundishe!? Tulitegemea yeye kutupa nguvu sisi sasa anatuondoa kwenye passion ya kushinda, aondolewe mapema inaonekana haijui kazi yake kwa sasaa.
Ndugu ,chezaji wetu mmoja tu ndio anacheza team ya maana PAOK kwanini kocha asiseme tunaenda kujifunza ,stars wanapaswa kupongezwa hatua waliyofikia ni nzuri wafanye mara tano mfululizo tutadai kombe
 
Vipi kama kauli yake ni mind games?, Unamkumbuka Mourinho na kauli zake za kudanganya makocha wenziwe.

Halafu uwe mkweli unapolinganisha uwezo wa Stars na hao wapinzani watatu.

DRC mwaka 1974 alikuwa bingwa wa afcon na akacheza kombe la dunia.

Zambia mwaka 2012 alibeba kombe la afcon mbele ya Ivory Coast ya kina Drogba na Yaya Toure.

Morocco kacheza nusu fainali ya kombe la dunia mwaka juzi.
Hahahaha ndio maana kocha kasema wnajjfunza
 
Hahahaha ndio maana kocha kasema wnajjfunza
Tuna akili mbovu kudhani kuwa tatizo ni kocha, viwango vya wachezaji wetuni vya chini sana. Hata aje Avram Grant kocha wa Zambia kwa wachezaji hawa tutapigwa tu.

Nchi hii inataka mapinduzi makubwa ya kimtazamo, huwezi kuwa na Baba Levo na Mwijaku kwenye suala linalohusu timu ya taifa halafu ukafika popote!.

Siasa zimeishi miaka mingi kwenye mpira wakati huo wenzetu wakijenga academies za soka za ukweli, wakifuata masharti yote ya mchezo.
 
Tena sio tu vya chini pia vya kawaida mno..
 
Ndugu ,chezaji wetu mmoja tu ndio anacheza team ya maana PAOK kwanini kocha asiseme tunaenda kujifunza ,stars wanapaswa kupongezwa hatua waliyofikia ni nzuri wafanye mara tano mfululizo tutadai kombe
Hiyo sio sababu ukishaitwa mchezaji wa team ya taifa cha kwanza ni morali ndio muhimu ila hawa wachezaji wetu hawa morali kabisa..
 
Back
Top Bottom