Kocha zahera awa mbogo asema tumecheza bila kula chakula asema anahujumiwa

Kocha zahera awa mbogo asema tumecheza bila kula chakula asema anahujumiwa

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Tumecheza mechi 3 kwa siku nane tena tunasafiri mkoa kwa mkoa wachezaji wanachoka ila kwa perfomance ya leo nimefurahi sana.

Jambo lingine lililonifurahisha wachezaji wangu wanacheza mechi bila kula.Jana tunafanya mazoezi tunapewa barua na Tff kuwa tutacheza mechi saa kumi na mbili jioni.Saa nne usiku natumiwa e mail na Tff na kutuambia mechi itachezwa saa kumi na sio saa kumi na mbili wachezaji wameshalala wanajua program yao watakula breakfast saa tano,chakula watakula saa nane watu walioenda pre match meeting ndio wananiambia coach mechi saa kumi.

Nikamuambia mkuu wa habari wapigie waambie sababu gani mechi saa kumi?

Nikapiga simu kongo kwa secretary wa chama cha soka cha Kongo nakumuuuliza hivi mnaweza kubadilisha mechi saa nne usiku mechi inachezwa kesho akanijibu coach haiwezekani na haiwezi fanyika.

Unaweza kubadilisha mechi 24HRS kabla ya mechi haiwezi pita 24 hrs kisha wakabadilisha mechi

Sisi tulipanga wachezaji watakula saa nane na wachezaji wangu walilala siwezi kuwaamsha wachezaji niwagongee amkeni haraka tunacheza saa kumi No.Nimewaacha wachezaji tumekula breakfast tukaenda kucheza mechi.
FB_IMG_15435635226865201.jpg
 
Wacha watuhujumu, ila tutafanya kweli, maana tushajua hatupendwi na tifu tifu. Tutatembeza kichapo kila atayepita mbele yetu, ndiyo wataelewa nguvu ya mwananchi ilivyo.
 
Tumecheza mechi 3 kwa siku nane tena tunasafiri mkoa kwa mkoa wachezaji wanachoka ila kwa perfomance ya leo nimefurahi sana.

Jambo lingine lililonifurahisha wachezaji wangu wanacheza mechi bila kula.Jana tunafanya mazoezi tunapewa barua na Tff kuwa tutacheza mechi saa kumi na mbili jioni.Saa nne usiku natumiwa e mail na Tff na kutuambia mechi itachezwa saa kumi na sio saa kumi na mbili wachezaji wameshalala wanajua program yao watakula breakfast saa tano,chakula watakula saa nane watu walioenda pre match meeting ndio wananiambia coach mechi saa kumi.

Nikamuambia mkuu wa habari wapigie waambie sababu gani mechi saa kumi?

Nikapiga simu kongo kwa secretary wa chama cha soka cha Kongo nakumuuuliza hivi mnaweza kubadilisha mechi saa nne usiku mechi inachezwa kesho akanijibu coach haiwezekani na haiwezi fanyika.

Unaweza kubadilisha mechi 24HRS kabla ya mechi haiwezi pita 24 hrs kisha wakabadilisha mechi

Sisi tulipanga wachezaji watakula saa nane na wachezaji wangu walilala siwezi kuwaamsha wachezaji niwagongee amkeni haraka tunacheza saa kumi No.Nimewaacha wachezaji tumekula breakfast tukaenda kucheza mechi.View attachment 951236
Kama hii habari aliyoileta Kocha Zahera ni ya kweli ni muhimu Viongozi wa TFF wakajiuzulu maana si kwa kuihujumu Yanga hivyo!!!
 
Tifua tifua hii imefail mapema sana kwakweli, walichofanikiwa nikufungia watu wanaoingilia maslahi yao
 
Hela ya kula mlikuwa nayo kweli? Manake nyie hamuaminiki, nimekumbuka maneno ya Apostle Maboya anasema Mungu haweki agano na masikini kwasababu masikini haaminiki, masikini anaweza kununulika muda wowote ule, yanga ni masikini, haiaminiki.
 
Sasa kama umejua mapema mechi saa kumi why usiwaamshe wachezaji wale chakula? May be chakula chenyewe hakikuwepo anazuga tu
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Labda Mafuguli anataka ndiyo iwe timu ya taifa hivyo maagizo kutoka juu yanaelekeza wapelekwe ki kwatakwata ili wawe kama wanajeshi!
 
zahera usanii mwingi Sana ,utafkiri mwimbaji wa taarabu
 
Back
Top Bottom