Kocha Zinedine Zidane ajiuzulu kuifundisha Klabu ya Real Madrid

Kocha Zinedine Zidane ajiuzulu kuifundisha Klabu ya Real Madrid

Angeendelea kubaki ningeona ajabu kwa mafanikio ya haraka aliyoipa club
 
Zizoue amesoma alama za nyakati makocha wengi wameondoka kwa kutimuliwa yeye amejihami mapema kulinda heshima kuliko kusubiri aibu ya kutimuliwa bora kuachia kwa heshima.
 
Kwa mashabiki wengi wa kandanda watashtushwa na uamuzi wa ghafla wa kuachia ngazi kwa kocha kijana wa Real Madrid Mfaransa Zinedine Zidane alioutangaza mchana wa 31/5/2018 alipokua anaongea na waandishi wa habari.

Lakini kwa upande mwingine waweza kusema ameondoka muda muafaka hasa ukizingatia rekodi aliyoiweka ya kuchukua Ubingwa wa Vilabu Ulaya (Champions League) kwa mara tatu mfululizo.

Swali; Je, wewe unahisi ni kwa nini ameamua kung'atuka?

Zidane amejiuzulu ili kumfundisha Freeman Alkaeli Mbowe mafunzo na matakwa mema ya Demokrasia katika Utawala / Uongozi.
 
Zizou labda kakimbia Pressure na pengine hakupeda kuondoka na makosa.....
Legacy yake bado iko Juu, sio unasubiri kuwa Sacked....
Nina Imani atapata sehemu nyingine punde tu....Wenger here we go!!!!!!
 
Zidane namuona kama mtu muoga hivi, anaogopa kufeli, tizama kuacha kwake kucheza mpira, aliamua kustaafu hali yaliwa badopira unamuhitaji, sasa hivi kaamua kuondoka madrid hali wanamuhitaji, wanaimani nae na ana nafasi nzuri ya kufanya vizuri, msimu huu ana nafasi ya kufanya usajili.
 
Jamaa anatisha..heshima kwako Zidane[emoji119]
IMG_20180531_150630_392.jpg
 
Zinedine Zidane aka Zizzou ameachia ngazi akiwa bado anahitajika na wachezaji na club ya Real Madrid kwa ujumla.
Ndani ya kipindi kifupi amefanikiwa kuweka rekodi ambayo haitakuja kuvunjwa hivi karibuni makombe matatu ya Uefa mfululizo sio jambo dogo hata kidogo.

Misimu mitatu,makombe tisa.
Uefa matau
La Liga moja
Ya mbuzi matano
 
Ukiambiwa kwamba kuna Watu Mwenyezi Mungu kawabariki na ' Nyota ' zao tokea wakiwa Matumboni mwa Mama zao basi mmoja wapo ni huyu ' Fundi ' Zinedine Yazid Zidane alias Zizzou.
Exactly mkuu..Kacheza soka kwa mafanikio, halafu amefundisha Real kwa mafanikio. Nyota ya bahati hii hapa duniani
 
Kwa rekodi yake ya kuchukua Ubingwa tena wa Ulaya mara tatu ( 3 ) mfululizo ' treble ' Zinedine Yazid Zidane ' Zizzou ' angeendelea kubaki Kuwa ' Manager ' wa Real Madrid ningemdharau na kumpuuza sana. Sasa hivi ajiandae tu kufundisha Timu ya Taifa ya Ufaransa pale Fainali za Kombe la Dunia zikimalizika mwezi July.
eee kabisa akachukue na world cup ili avunje nyingine
 
Kufuatia kujiuzulu ghafla kwa kocha mkuu wa Real Madrid, Klabu hiyo imeanza mchakato wa kupata kocha mpya. Wewe ukiwa kama mdau wa soka, unadhani ni kocha yupi anaweza kuvaa viatu vya Zidane pale Madrid?
 
Back
Top Bottom