Maboss wa timu wana uwezo wa kuchambua wachezaji , timu pinzani na kitu cha msingi kabisa ni kuwadhibiti wachezaji yaani "Man-management".
Sasa ukiwa na wachezaji "multi-millionaires" kama Cristiano Ronaldo na Gareth Bale halafu hawakusikilizi wewe kama meneja na hawafuati maelekezo yaani intructions wawapo uwanjani basi ujue wewe huwezi kuwa meneja wa hiyo timu.
Kuna sababu kwanini Cristiano Ronaldo hakuweza kufunga magoli kwenye fainali na Liverpool na pia Zizzou ana tactical plan ya jinsi ya kukabiliana na timu pinzani na akazifunga, na hivyo kathibitisha kupitia ligi zote muhimu.
Hivyo basi mtu pekee ambae wachezaji wanaweza kumwita hata baba yao kwa kuwa na uwezo wa kukung'uta na kiatu ni Mzee Alex Ferguson maana yeye ukileta za kuleta atakuweka bench na atakurushia kiatu kama alivyomfanyia David Bekham huko ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo pamoja na utajiri wake Bekham.
Ukitaka kusomea sayansi ya michezo na utawala tafuta kitabu cha mzee Alex Ferguson kiitwacho Leading na kingine kiitwacho A Will to Win.
Hivyo uwezo wa maboss vijana kama Zidane wa Man Management tumeuona kwa kumtoa Ronaldo na Bale kukaa bench ili kutimiliza mpango wake wa kiufundi kuifunga Liverpool.
Lakini Uongozi nao una yake katika kufanikisha kazi ya meneja wa timu sasa mkielewana falsafa mambo poa lakini msipoelewana kama ilivyokuwa sasa kwa Zidane na uongozi wa Madrid basi imekula kwao.