Kodi ilirahisisha Nyerere kudai Uhuru wa Tanganyika

Kodi ilirahisisha Nyerere kudai Uhuru wa Tanganyika

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Kodi ni uti wa mgongo wa uchumi wa taifa lolote, lakini kodi nyingi zisizolipika ni chanzo cha kuanguka dola lolote duniani. Ukisoma historia madola mengi yalianguka baada ya watawala kuwatoza watawaliwa kodi kubwa zisizolipika ili kugharamia mipango ya serikali au matumizi binafsi ya watawala.

Mwl. Nyerere alipata uungwaji mkubwa wa wananchi waliochoshwa na kuudhiwa na kodi za mkoloni wasizoweza kuzilipa. Kodi ya kichwa iliwafanya wanaume kuzikimbia familia zao na kwenda kujificha porini kwa kuogopa kukamatwa. Kodi iliwafanya wanaume kuziacha familia zao na kwenda kufanya vibarua kwenye mashamba ya mkonge, kahawa, chai, kakao, mpira, mifugo, nafaka na migodi ya madini iliyokuwa ikimilikiwa na wakoloni ili wapte fedha za kulipa kodi.

Nyerere aliwaambia wananchi wamuunge mkono kudai uhuru, na wakishapata uhuru atafuta kodi ya kichwa inayowasumbua. Wananchi wakafurika kwa wingi kujiunga na TANU ili kodi ifutwe, na kweli baada ya Uhuru mwl. Nyerere aliifuta kodi.

Ingawa mkoloni alikuwa akiwapatia wananchi pembejeo za kilimo, masoko ya mazao yao, majosho ya mifugo yao na ajira kwenye mashamba, ranchi za wanyama, migodi ya madini na ujenzi ili wapate urahisi wa kuilipa kodi kirahisi lakini wananchi waliichukia kodi.

Leo hii wanachi walalamika kuwa kodi ni kubwa na nyingi mmno kuweza kulipa, lakini pia hawapewi pembejeo za kilimo, hawana masoko ya uhakika kwa mazao yao, hakuna viwanda, mashamba makubwa ya kilimo na mifugo wala ajira kwa watu wengi. Je, unadhani wananchi wanaipenda kodi hii kama ilivyo?

Je, kodi hii inalipika?
 
Back
Top Bottom