Kodi kubwa zinawanyima fursa Watanzania kumiliki Simu bora na za Kisasa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Tanzania ina kiwango kikubwa cha kodi na ushuru inaotoza kwenye simu za mkononi ikilinganishwa na mataifa mengine duniani.

Viwango hivyo vinaelezwa kuwa juu kuliko mataifa mengi ya kusini mwa Jangwa la Sahara, Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika, Ulaya, Asia hata Amerika Kusini, hatua inayowadumaza Watanzania kumiliki simu janja.

Ingawa kodi na ushuru hubadilika mara kadhaa, ripoti ya Shirikisho la Kampuni za Simu Duniani (GSMA) iliyotolewa mwaka 2021 inaonyesha Tanzania inakusanya asilimia 34 ya tozo na ushuru kwenye kila simu inayouzwa kwa mteja.

Kiwango hicho ni kikubwa kuliko asilimia 21 kinachotozwa Ulaya au asilimia 18 huko Amerika ya Kusini na asilimia 26 kusini mwa Jangwa la Sahara. Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika kodi ni asilimia 24 sawa na Asia.

Taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), tozo na ushuru unaokatwa kwa kila simu inayopita bandarini ni asilimia 18 zikijumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ushuru wa maendeleo ya reli na kodi ya bandari.

Kutokana na hali hiyo, bei ya simu moja nchini hujumuisha zaidi ya theluthi moja inayoenda kwenye kodi na ushuru wa Serikali.

Simu ya Sh350,000 kwa mfano, inabidi iuzwe kwa Sh500,000, kwa hiyo mzigo wa Sh150,000 ni kodi na ushuru unakwenda kwa mteja wa simu hiyo.

Kutokana na mazingira hayo, baadhi ya wafanyabiashara wa simu janja wanasema Serikali inaweza kukwama kufanikisha malengo yake ya kufikia asilimia 80 ya wananchi kutumia intaneti ifikapo mwaka 2025 kutoka asilimia 46 ya sasa, hivyo kushauri kuurejesha msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye simu janja ambao Serikali iliutoa kwenye bajeti ya mwaka 2021/22, ikihusisha pia vishikwambi (tablets) na modemu kabla ya kuufuta mwaka 2022/23 kwa madai ya kutoona mabadiliko ya bei kwa walengwa.

Hafsa Mohamed, meneja mauzo wa duka la simu za Infinix lililopo Kariakoo anasema baada ya kuondolewa kwa kodi hiyo simu ya Sh260,000 ilishuka hadi Sh210,000, huku ya Sh1.4 milioni ikiuzwa Sh1.18 milioni.

“Nilikuwa nauza simu janja 15 hadi 20 kwa siku, ila sasa hivi ni chini, napata wateja watano. Kasi imepungua,” anasema Hafsa.

Reginald Asenga, meneja mauzo duka la simu za kampuni ya Vivo anasema simu ya Sh270,000 ilishuka mpaka Sh229,000 VAT iliposamehewa, lakini baada ya kurejeshwa inauzwa kwa bei yake halisi ya Sh270,000, hivyo akashauri zikaribishwe kampuni kubwa za simu kuja kuwekeza kwa masharti nafuu. Vivo inauza wastani wa simu 5,000 kika mwezi nchini.

“Kampuni hizi kubwa zilikuja kuwekeza nchini badala ya wananchi kufuata simu nje, itaongeza ushindani hivyo kupunguza bei kwa mtumiaji wa mwisho, kwani wengi wataweza kuzipata hapahapa kwa bei nafuu,” anasema Asenga.

Mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara, Dk Donath Olomi anasema Serikali inatakiwa kulitizama suala hilo kwa hesabu zitakazosaidia kupunguza umaskini kwa wananchi, kuongeza wigo wa mapato na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.

“Ni hesabu tu, inabidi waangalie (Serikali) kwa kutambua kwamba endapo tutaondoa kodi nyingi ili watumiaji waongezeke manufaa yatakuwa mengi kuliko uchukuaji wa kodi kabla ya kupata simu hizo. Kama mataifa ya wenzetu kodi ziko chini basi wananufaika zaidi kuliko sisi,” anasema Dk Olomi.

Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya Oktoba 2022 inaonyesha kuna jumla ya simu za 2G (viswaswadu) milioni 52.3 pamoja na simu janja milioni 17 pekee zinazotumika nchini, sawa na asilimia 27 ya mawasiliano ya 3G kwa idadi ya watu milioni 62 nchini.

Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja anasema Serikali ilianza kukusanya maoni kwenye sekta hiyo Novemba mwaka jana, katika kongamano la kuboresha sera za kodi.

“Walikuwepo maofisa wa kampuni za simu, kwa hiyo kama maoni hayo waliyatoa basi wasubiri kwenye wasilisho la bajeti kuu ya Serikali itakayosomwa Juni huenda yakawepo. Haya maoni pia tunayapokea, lakini tunashauri wafanyabiashara kujenga uaminifu wa kulipa kodi kwa hiari,” anasema Mwaipaja.

Kwa nini sasa?

Wito kusamehe VAT umetolewa siku chache baada ya kutangaza mwelekeo wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha kusomwa, ukibainisha unalenga kuhamasisha kujenga uchumi wa kidijitali kwa kuweka mazingira rafiki na wezeshi wananchi kuzitumia fursa zilizopo kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (Unicef) mwaka 2021 inaonyesha asilimia 75 ya waliohojiwa walisema kikwazo kikubwa cha kumiliki simu janja kwao ni gharama kubwa, huku asilimia 12 wakilalamikia gharama kubwa za intaneti na asilimia saba ubovu wa miundombinu ndio tatizo kwao.

Wakati mradi wa Tanzania ya kidijitali wa miaka mitano ukiendelea kutekelezwa, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabir Bakari anakiri changamoto hiyo akidai Serikali inaendelea na juhudi za kuongeza matumizi ya simu janja zinaendelea.

“Serikali kwa sasa chini ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) iko kwenye maandalizi ya kushawishi uwekezaji ili tuwe na kampuni ya ndani inayozalisha simu janja zenye gharama nafuu ili kuongeza idadi ya watumiaji wa intaneti, hazitakuwa na mambo mengi kama hizi tunazoagiza sasa,” amesema Dk Bakari.

MWANANCHI
 
Vat yetu ni Asilimia 18, ni kubwa ila sio kubwa kama ulaya.

Pia usisahau Tamaa za wafanyabiashara, wengi kwanza hawana hizo Vat na hawatoi risiti, pia wanaweka margin kubwa.

Kwa ambaye yupo Familiar na bei ya jumla anajua hili.
 
Nimeangiza simu na tablets kadhaa na sijawahi kulipishwa hiyo VAT ya 34%. Nililipa 18% kisha ikaja ule mwaka ambapo kodi iliondolewa na nikawa nalipa 3000 na kitu hivi (gharama ya kupokea mzigo posta) na mara ya mwisho nililipa 18% + gharama ya Posta.

Hiyo VAT iliyotajwa sielewi wamepata wapi, maana kisheria VAT ni 18%?
 
34% jamaa amemaanisha ni jumla ya kodi zote kwa simu (VAT+kodi ya reli + import duty nk)
 
Kodi haipigwi hivyo lakini, ndio maana zipo fixed asilimia 25% import na 18% Vat huwezi ukajumlisha na kusema ni asilimia 43% sababu utapata figure tofauti kabisa.
Ni kweli mkuu, yaani nilichomuelewa mleta mada ni kuwa hiyo 34% ameieleza kwa urahisi wa mtu asiyejua kodi kuelewa. Yaani mfano simu imefika bandarini kwa Tshs. 200,000/=
import labda 25% ya laki 2 = Tshs. 50,000
VAT = laki 2 + 50,000 = 250,000 x 18% = 45,000/=
50,000 + 45,000 = 95,000/= (kodi)
Simu itauzwa Tshs. 295,000/=

Sasa 95,000/200,000 x 100% = 47.5%

Kwa hiyo yeye amesema simu hiyo maana yake kodi imekuwa ni asilimia 47 ya bei ya manunuzi. Nafikiri ndicho alichomaanisha
 
Serikali iliondoa VAT ili wananchi wengi waweze pata simu kwa bei rahisi.

Serikali ikaja gundua bei za simu hazishuki ikaamua rejesha VAT.

Wauza simu wengi hawatoi risiti
Hii inaweza ikawa sababu ya kuwekewa kodi kubwa, sometime wafanyabiashara wanaleta wenyewe tatizo.
 
Tanzania ina kiwango kikubwa cha kodi na ushuru inaotoza kwenye simu za mkononi ikilinganishwa na mataifa mengine duniani.

Viwango hivyo vinaelezwa kuwa juu kuliko mataifa mengi ya kusini mwa Jangwa la Sahara, Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika, Ulaya, Asia hata Amerika Kusini, hatua inayowadumaza Watanzania kumiliki simu janja.

Ingawa kodi na ushuru hubadilika mara kadhaa, ripoti ya Shirikisho la Kampuni za Simu Duniani (GSMA) iliyotolewa mwaka 2021 inaonyesha Tanzania inakusanya asilimia 34 ya tozo na ushuru kwenye kila simu inayouzwa kwa mteja.

Kiwango hicho ni kikubwa kuliko asilimia 21 kinachotozwa Ulaya au asilimia 18 huko Amerika ya Kusini na asilimia 26 kusini mwa Jangwa la Sahara. Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika kodi ni asilimia 24 sawa na Asia.

Taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), tozo na ushuru unaokatwa kwa kila simu inayopita bandarini ni asilimia 18 zikijumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ushuru wa maendeleo ya reli na kodi ya bandari.

Kutokana na hali hiyo, bei ya simu moja nchini hujumuisha zaidi ya theluthi moja inayoenda kwenye kodi na ushuru wa Serikali.

Simu ya Sh350,000 kwa mfano, inabidi iuzwe kwa Sh500,000, kwa hiyo mzigo wa Sh150,000 ni kodi na ushuru unakwenda kwa mteja wa simu hiyo.

Kutokana na mazingira hayo, baadhi ya wafanyabiashara wa simu janja wanasema Serikali inaweza kukwama kufanikisha malengo yake ya kufikia asilimia 80 ya wananchi kutumia intaneti ifikapo mwaka 2025 kutoka asilimia 46 ya sasa, hivyo kushauri kuurejesha msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye simu janja ambao Serikali iliutoa kwenye bajeti ya mwaka 2021/22, ikihusisha pia vishikwambi (tablets) na modemu kabla ya kuufuta mwaka 2022/23 kwa madai ya kutoona mabadiliko ya bei kwa walengwa.

Hafsa Mohamed, meneja mauzo wa duka la simu za Infinix lililopo Kariakoo anasema baada ya kuondolewa kwa kodi hiyo simu ya Sh260,000 ilishuka hadi Sh210,000, huku ya Sh1.4 milioni ikiuzwa Sh1.18 milioni.

“Nilikuwa nauza simu janja 15 hadi 20 kwa siku, ila sasa hivi ni chini, napata wateja watano. Kasi imepungua,” anasema Hafsa.

Reginald Asenga, meneja mauzo duka la simu za kampuni ya Vivo anasema simu ya Sh270,000 ilishuka mpaka Sh229,000 VAT iliposamehewa, lakini baada ya kurejeshwa inauzwa kwa bei yake halisi ya Sh270,000, hivyo akashauri zikaribishwe kampuni kubwa za simu kuja kuwekeza kwa masharti nafuu. Vivo inauza wastani wa simu 5,000 kika mwezi nchini.

“Kampuni hizi kubwa zilikuja kuwekeza nchini badala ya wananchi kufuata simu nje, itaongeza ushindani hivyo kupunguza bei kwa mtumiaji wa mwisho, kwani wengi wataweza kuzipata hapahapa kwa bei nafuu,” anasema Asenga.

Mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara, Dk Donath Olomi anasema Serikali inatakiwa kulitizama suala hilo kwa hesabu zitakazosaidia kupunguza umaskini kwa wananchi, kuongeza wigo wa mapato na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.

“Ni hesabu tu, inabidi waangalie (Serikali) kwa kutambua kwamba endapo tutaondoa kodi nyingi ili watumiaji waongezeke manufaa yatakuwa mengi kuliko uchukuaji wa kodi kabla ya kupata simu hizo. Kama mataifa ya wenzetu kodi ziko chini basi wananufaika zaidi kuliko sisi,” anasema Dk Olomi.

Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya Oktoba 2022 inaonyesha kuna jumla ya simu za 2G (viswaswadu) milioni 52.3 pamoja na simu janja milioni 17 pekee zinazotumika nchini, sawa na asilimia 27 ya mawasiliano ya 3G kwa idadi ya watu milioni 62 nchini.

Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja anasema Serikali ilianza kukusanya maoni kwenye sekta hiyo Novemba mwaka jana, katika kongamano la kuboresha sera za kodi.

“Walikuwepo maofisa wa kampuni za simu, kwa hiyo kama maoni hayo waliyatoa basi wasubiri kwenye wasilisho la bajeti kuu ya Serikali itakayosomwa Juni huenda yakawepo. Haya maoni pia tunayapokea, lakini tunashauri wafanyabiashara kujenga uaminifu wa kulipa kodi kwa hiari,” anasema Mwaipaja.

Kwa nini sasa?

Wito kusamehe VAT umetolewa siku chache baada ya kutangaza mwelekeo wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha kusomwa, ukibainisha unalenga kuhamasisha kujenga uchumi wa kidijitali kwa kuweka mazingira rafiki na wezeshi wananchi kuzitumia fursa zilizopo kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (Unicef) mwaka 2021 inaonyesha asilimia 75 ya waliohojiwa walisema kikwazo kikubwa cha kumiliki simu janja kwao ni gharama kubwa, huku asilimia 12 wakilalamikia gharama kubwa za intaneti na asilimia saba ubovu wa miundombinu ndio tatizo kwao.

Wakati mradi wa Tanzania ya kidijitali wa miaka mitano ukiendelea kutekelezwa, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabir Bakari anakiri changamoto hiyo akidai Serikali inaendelea na juhudi za kuongeza matumizi ya simu janja zinaendelea.

“Serikali kwa sasa chini ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) iko kwenye maandalizi ya kushawishi uwekezaji ili tuwe na kampuni ya ndani inayozalisha simu janja zenye gharama nafuu ili kuongeza idadi ya watumiaji wa intaneti, hazitakuwa na mambo mengi kama hizi tunazoagiza sasa,” amesema Dk Bakari.

MWANANCHI
Tunaweza singizia vitu vingi kuhusu bei ya manunuzi ya simu. Wafanyabiashara wa simu asilimia kubwa wanatupiga kwa kisingizio cha kodi. Kuna mwaka kama sitokosea mwaka juzi serikali iliondoa VAT kwenye vishkwambi "Tablets" lakini mtaani simu hazikushuka wala nini.Ukitaka jua tunapigwa na wafanyabishara wa bidhaa hiyo nunua simu uone unakuta simu na charger pekee wakati simu inatakiwa kuwa na kitabu cha kujifunza ,ear phone na memory card.
Hata huko nje simu zinauzwa bei na kuna kodi pia wanalipia.Umezungumza la msingi sana kwenye kuwekeza simu zizalishwe ndani nami naungana na wewe kwa 100%.
Tukiacha vitu viingie bila lipisha kodi
1: Tutakuwa ni soko la nchi za wenzetu na hatimaye uchumi wetu utadorola
2: Nguvu ya kuanzisha kiwanda/viwanda au kuwekeza itakuwa hakuna.

Tukumbuke kuwa kodi ndiyo chanzo cha serikali yoyote ile ndiyo maana wenzetu hata mpira unaona kina Messi walibanwa kodi licha ya kuwa ni mchezaji mkubwa na ni nyota Duniani.
ukienda nchi kama India hata ukibainika umepokea Rushwa ,Authority yao ya Kodi wanakuwahi haraka kodi yao kabla ya Authority ya Rushwa hawajakuchukulia hatua.

Nachokiamini kuwa wafanyabiashara wachache kwa kuwa wameshajua watu nini wanahitaji ndiyo maana wanapandisha kwa kisingizio cha kodi, kumbuka the high the demand the high the price.Demand ya simu imekuwa ni kubwa na ndiyo maana angalia simu zenye bei demand yake ni kubwa kama apple,samsung halafu angalia Tecno.
 
Kweli ujinga ni mzigo. Kumiliki simu ya bei kubwa sio ujanja wala maendeleo. Ni ushamba tu wa kutafuta heshima kwa watu wenye akili ndogo.

Ungeongelea suala la serikali kuondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili watu washushe mijengo ya maana hapo ningekuelewa.
 
Kuwa na simu ya bei kubwa bila matumizi sahihi ni anasa na ukengeufu ila ukiwa na simu kubwa yenye uwezo na inakusaidia kuingiza kipato hiyo ndio inayofaa zaidi
 
Wafanyabiashara % kubwa sio wakweli kodi za simu zilipoondolewa tuliendelea kupigwa bei ya ile ile.
 
Back
Top Bottom