Kodi mpya za miamala nadhani kuna mchezo tunachezewa

Kodi mpya za miamala nadhani kuna mchezo tunachezewa

Living Pablo

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2020
Posts
3,549
Reaction score
10,995
Mapema wiki hii kodi mpya za miamala zimetoka ambapo baadhi ya wananchi tunalalamika zinatunyonya lakin pengine nahisi kuna mchezo tunachezewa.

Ukiangalia muda ambao suala limepitishwa ni kipindi ambacho vyama vya upinzani vinadai Katiba Mpya ambapo Rais akasema wamuache kwanza apambane na uchumi kwanza lakini wao hawakusitisha mikutano yao ya kulenga katiba ibadilishwe.

Suala la kujiuliza pengine Rais SSH labda ametaka kuzima suala la katiba mpya kijanja ambapo wanaupinzani nao wameamua kuingilia suala la kodi na kuacha kidogo hilo la katiba mpya. Binafsi naamini malalamiko yakiwa mengi kodi zitarudi kama ilivyokuwa awali kwani hata bei za vifurushi walifanya hivi hivi baadae wakarudisha.

NI SUALA LA MUDA TU
 
Jamani, si tulishakubaliana Watanzania siyo wanyonge? Hebu tufanyeni sasa hiyo miamala. Sisi siyo wanyonge bhana. 😁
 
Magufuli alisema anawatetea Wanyonge kwa. Kuyabana makampuni makubwa ya madini na kushughulikia wezi, mkasema kuwaambia Watanzania Wanyonge ni kuwatusi. Leo amekuja mama demokrasia amesema sisi sio Wanyonge tulipe kodi, mnaanza kulalamika.
😅😅🤣🤣🤣🤣
 
😁😁
 
KAZI iendelee,hii ndio siasa ambayo wengi hatuielewi[emoji2958][emoji2958]
 
Back
Top Bottom