Kodi na Tozo zinazowaumiza Watanzania: Tumekosea wapi ili tutubu?

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Ndugu zangu Watanzania tumekosea wapi mbona siku hadi siku mambo yanazidi kuwa tight sana mtaani huku. No pesa ukitumia ka hela kako kidogo unakutana na makato ya ajabu,ukiweka Vocha usalimie ndugu & jamaa napo tabu.

Day after day wanakuja na mbinu mpya sio kwa ajili ya kumpa ahueni Mtanzania bali wanazidi kutuongezea maumivu tu. Sitashangaa tena zikitoka takwimu za watu wasiokuwa na furaha Ulimwenguni Tanzania Tukaongoza no one is happy anymore kwa jinsi mambo yanavyoenda.

Viongozi wanaonekana kabisa hawapo kwa ajili ya wananchi bali wapo kwa ajili ya personal interests zao na sio ajabu kusikia kiongozi akijibu kwa ubabe kama hutaki nenda kaishi nchi nyingine tunaona kama kauli ndogo lakini inamaana zaidi ya 100 na zaidi. Kiongozi anayekwambia kaishi sijui wapi huko unadhani atakua na uchungu na wewe No.

Tumekua kama ng'ombe anayekamuliwa wamekamua maziwa yameisha sasa Chuchu zimeisha kutoa damu badala ya maziwa ila bado wanakamua tu.

Hakuwa mjinga mzee wetu Mkapa aliyefuta kodi ya Kichwa nakumbuka siku hiyo watu walishangilia sana na hata haikua hela nyingi almost mia 100-200 sasa assume kama mtu anayefurahia kufutwa kwa kodi ya Shs 100 leo unamkata mtu zaidi ya tsh 5000 kisa katumiwa hela.

SIKATAI KULIPA KODI NIKIWA KAMA MZALENDO ILA SIPENDI KULIPA KODI ZA DHULUMATI UKIONA KARIBIA ASILIMIA 89 YA WATU HAWA FURAHA DHIDI YA KODI/TOZO JUA HAPO UNAFANYA DHULUMA.

Tumkumbuke mtu mfupi Zakayo katika Biblia alikua mtoza/Mkusanya ushuru ila baada ya kuona hiyo kazi haina haki imejaa Dhuluma alichukua maamuzi ya kuachana nayo na kuambatana Na Bwana Yesu.

Rai yangu...Serikali rudini mezani mjadili tena tengenezeni Kodi/tozo ambazo kila Mzalendo atatoa huku akicheka/akifurahi.
 
Kodi zote ni sawa endapo wananchi watakuwa na uchumi mzuri......Ng'ombe ukimlisha unahaki ya kumkamua maziwa mengi na sio vinginevyo.
 
Je, huyu ngombe wa Sasa kalishwa vya kutosha kama kalishwa kwanini ukimkamua analia kwa uchungu?

Lazima uangalie Je umempa chakula vizuri.

Je, chuchu hazina vidonda?

Je, unauwezo wa kutoa Lita 10 unazotaka wewe?
 
Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari. Serikali ya awamu ya sita imejikita kukusanya tu. Bado hawajawa wabunifu namna ya kuchochea ukuaji. Pesa zinazokusanywa zingefaa zielekezwe kule kwenye potential ya kuleta tija tenfold.
 
Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari. Serikali ya awamu ya sita imejikita kukusanya tu. Bado hawajawa wabunifu namna ya kuchochea ukuaji. Pesa zinazokusanywa zingefaa zielekezwe kule kwenye potential ya kuleta tija tenfold.
Hapo unapokusanya ndugu umepaandaa ni sawa na kutupa mbegu shambani halafu unaenda kuvuna baada ya miezi 6 bila kupalilia au kuweka mbole.
 
Wenye mamlaka hawana takwimu zozote za hali ya uchumi wa Wananchi wao...wanachofanya ni hisia tu.

Wakiwaona kina Diamond na kina Juksi hao mitandaoni basi kwao ni takwimu tosha kuwa kila Mtu anahimili hizo tozo za miamala...na kama ndivyo sioni tena kuna haja gani kuendelea kuwa na mpango kama ule wa tasaf.

Afadhali hata hizo tozo za luku, lakini kama hizi za miamala zinawagusa mpaka Bibi na Babu zetu huko Vijijini wenye hali duni, sasa tena unataka kupunguza hata elfu tano anayotumiwa na Mjukuu au Jirani yake hivi hiyo ni kuwasaidia au kuwaongezea tu ugumu wa maisha?

Isitoshe haya makato pia yanapunguza hata wenye nia ya kutuma...kama ana elfu tano mfukoni na kamkumbuka Bibi au Babu akifikiria makato anaghairi.
 
Other side mama anaweza kuwa mtu powa swali la kujiuliza je anazungukwa na nani?
Kwani hao si anawateua yeye?

Au wamaanisha 'wanaomzunguka' hata kwenye kufanya uteuzi?.
 
Kibaya zaidi hawana ubunifu na njia ya kumkwamua mtu wa chini.

Ajira zimefutwa wala siyo issue sana kibaya zaidi hadi njia za kupokea pesa kutoka PAYPAL wamefunga.

Kuna fursa nyingi sana mtandao ila njia ya malipo ni PAYPAL. Unaacha pesa nje nje mpaka mwanaume unatoa machozi, unaomba hata ungezaliwa Kenya tu
 
Kwani hao si anawateua yeye?

Au wamaanisha 'wanaomzunguka' hata kwenye kufanya uteuzi?.
Shida ya Teuzi na Nani anamfahamu nani.
Wengi wapo kimaslahi kwanza ashibe yeye kwanza halafu ndio amkumbuke mwanachi wa kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…