bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Ndugu zangu Watanzania tumekosea wapi mbona siku hadi siku mambo yanazidi kuwa tight sana mtaani huku. No pesa ukitumia ka hela kako kidogo unakutana na makato ya ajabu,ukiweka Vocha usalimie ndugu & jamaa napo tabu.
Day after day wanakuja na mbinu mpya sio kwa ajili ya kumpa ahueni Mtanzania bali wanazidi kutuongezea maumivu tu. Sitashangaa tena zikitoka takwimu za watu wasiokuwa na furaha Ulimwenguni Tanzania Tukaongoza no one is happy anymore kwa jinsi mambo yanavyoenda.
Viongozi wanaonekana kabisa hawapo kwa ajili ya wananchi bali wapo kwa ajili ya personal interests zao na sio ajabu kusikia kiongozi akijibu kwa ubabe kama hutaki nenda kaishi nchi nyingine tunaona kama kauli ndogo lakini inamaana zaidi ya 100 na zaidi. Kiongozi anayekwambia kaishi sijui wapi huko unadhani atakua na uchungu na wewe No.
Tumekua kama ng'ombe anayekamuliwa wamekamua maziwa yameisha sasa Chuchu zimeisha kutoa damu badala ya maziwa ila bado wanakamua tu.
Hakuwa mjinga mzee wetu Mkapa aliyefuta kodi ya Kichwa nakumbuka siku hiyo watu walishangilia sana na hata haikua hela nyingi almost mia 100-200 sasa assume kama mtu anayefurahia kufutwa kwa kodi ya Shs 100 leo unamkata mtu zaidi ya tsh 5000 kisa katumiwa hela.
SIKATAI KULIPA KODI NIKIWA KAMA MZALENDO ILA SIPENDI KULIPA KODI ZA DHULUMATI UKIONA KARIBIA ASILIMIA 89 YA WATU HAWA FURAHA DHIDI YA KODI/TOZO JUA HAPO UNAFANYA DHULUMA.
Tumkumbuke mtu mfupi Zakayo katika Biblia alikua mtoza/Mkusanya ushuru ila baada ya kuona hiyo kazi haina haki imejaa Dhuluma alichukua maamuzi ya kuachana nayo na kuambatana Na Bwana Yesu.
Rai yangu...Serikali rudini mezani mjadili tena tengenezeni Kodi/tozo ambazo kila Mzalendo atatoa huku akicheka/akifurahi.