Theorist Mosses
JF-Expert Member
- Jul 16, 2022
- 345
- 253
Utangulizi
Taifa letu ni miongoni kati ya nchi zinazo toza kodi kwenye biashara, uwekezaji na ajira. ikiwa na maana ya kwamba ni mpango endelevu utakao saidia kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kupitia kwenye elimu, siasa, kilimo, sayansi na teknolojia.
Kodi zinafaida na hasara, sheria zinatambua kodi kwenye upande wa faida kwamba ni kwaajiri ya kutatua changamoto za taifa letu ili kuleta maendeleo. Lakini ndani ya taifa letu kodi zimekuwa zikileta hasara kubwa na kusababisha kuporomoka kwa maendeleo na kufanya maisha kuwa magumu kwa wananchi.
Tunategemea mabadiliko kupitia kodi ambayo inasababisha hongezeko la umaskini ndani ya taifa. Kodi zinatozwa kwa wingi lakini hatuoni maendeleo na matokeo yake inamaana kodi zinazokusanywa hazifiki kwenye mamlaka husika ili zitumike kutatulia changamoto kwenye kupambana na umaskini.
Ufafanuzi
Kodi, ni tozo zinazo tozwa kwenye biashara, uwekezaji pamoja na ajira. Ni njia ya mapato iliyo pitishwa kwa muujibu wa vifungu vya sheria ya kodi ya mwaka 2004. Lengo likiwa ni kuongeza mapato ndani ya taifa ili kuchangia kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo siasa, elimu, kilimo na zinakusanywa kupitia kwa mamlaka husika ya ukusanyaji wa kodi, Tanzania revenue authority - TRA.
Tunapo zungumzia kodi namaanisha hivi, Unajua sisi kama sisi hatuwezi kutatua matatizo na changamoto kwa kila mtu mmoja mmoja, kwamba ni vyema tutatue changamoto kwa ujumla ambazo zinatuhusu kwa pamoja. Lakini sisi tunaongozwa na viongozi ambao tumewachagua ili kutuwakilisha wananchi wote kwa ujumla. Ambao ndiyo wanatuongoza kutatua changamoto za kila mtu kwa mikusanyo ya kila mwananchi ambayo hiyo mikusanyo ndiyo mapato ya kodi.
Kwahiyo kodi ni pesa zetu wenyewe wananchi na wala siyo madeni. Mategemeo ya ukusanyaji wa kodi ni kwaajiri ya kusudi moja tu, kutatulia changamoto za wananchi wote kwa ujumla ambazo zina kwamisha maendeleo. Kwahiyo kusudi la kodi siyo madeni ni kutatua changamoto za wananchi wote kwa pamoja ili kuchochea uchumi maendeleo ya taifa.
Kwa muujibu wa vifungu vya sheria vinaeleza ukusanyaji wa kodi ni kwaajiri ya utatuzi wa changamoto za ndani zinazo jumuisha wananchi wote na kusaidia kuleta maendeleo. Sasa hebu tujiulize, mbona changamoto kama vile kwenye upande wa elimu. Kuhusu ujenzi wa madarasa na madawati kuna wanafunzi mpaka leo kwenye maeneo mengi hawana madarasa inamaana wananchi wa sehemu hiyo hawalipi kodi, kama wanalipa kodi zao zinaenda wapi hadi watoto wasome chini ya mikorosho.

(pichani wanafunzi wakisomea chini ya miti)
Jinsi kodi zinavyo chochea umaskini
Unajua kwamba wananchi wengi wamekuwa wakilipa kodi kwenye mamlaka husika kwa mategemeo ya kupata maendeleo. Wananchi wana tegemea kwamba kodi walizolipa zitarudi kutatua changamoto zao, matokeo yake hizo kodi zao hazirudi kutatulia changamoto za wananchi ambapo inafikia kipindi changamoto zinazidi kuongezeka na kufanya wananchi kuwa na maisha magumu zaidi hadi kushindwa kuendelea kulipa kodi.
Lakini kumbuka serikali ilikusanya kodi ikiwa na mipango madhubuti ya kuja kutatulia changamoto za wananchi. Matokeo yake serikali aiwajibiki na wananchi inakuwa ikifanya kazi ya ukusanyaji lakini matokeo chanya ya kodi zilizo kusanywa hapo awali zilivyo tumika haijulikani. Alafu kesho yake serikali inarudi tena kukusanya kodi nyengine kwa wananchi, kwahiyo wananchi wanakuwa wanafanya tu kazi ya kulipa kodi huku matatizo yao yakizidi kuongezeka na kuwashusha kabisa kimaendeleo kwa sababu changamoto zao hazitatuliwi. hili ni tatizo na nikinyume cha sheria ya ukusanyaji wa mapato ya kodi.
Upandishaji wa kodi pia hauendani na hali halisi ya wananchi kwamba serikali inapandisha kodi na kuongeza mara dufu ukusanyaji wa mapato. Lakini kodi zinazo kusanywa mbona hazionekani zikileta maendeleo na kutatua changamoto za wananchi. Ni tatizo kwamba wananchi kodi tunalipa lakini tukisha kusanya hazirudi kutatulia changamoto zetu jambo ambalo linakwamisha maendeleo.
Wananchi wengi wanakumbwa na changamoto kwenye maeneo mbalimbali mfano ukosefu wa madaraja, madarasa, maji, chakula nk. Kumbuka hawa wanabiashara zao wengine wame jiajiri na wanatozwa kodi. Serikali inasisitiza walipe kodi kwamba zitatumika kutatulia changamoto zao ndani ya jamii, lakini inakuwa tofauti na mategemeo kwamba changamoto hazitatuliwi hupelekea kufanya maisha kuwa magumu.
Yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo kuhusu kodi, ambayo yatachangia kusaidia kwa kiasi chake kutatua migogoro ya kimaendeleo kwa wananchi kwamba nini kifanyike ili kutatua changamoto ndani ya jamii.
Mapendekezo
• Serikali iweke malengo na kutambua changamoto za wananchi kabla ya ukusanyaji wa kodi na makusanyo yote yazingatie kiwango cha mahitaji ya wananchi husika. ukusanyaji wa kodi umekuwa hauna malengo na kusababisha kodi zenye hasara. Kuwe na malengo ambayo yatakuwa muongozo kabla ya kutoza kodi ili mapato yanapo kusanywa yaende moja kwa moja kwenye utatuzi wa tatizo husika na zitumike kwa kuzingatia bajeti zilizo wekwa kwenye malengo ili changamoto zitatuliwe kwa wakati.
• Wananchi wasikusanyishwe kodi mpya ikiwa zilizo kusanywa hapo awali hazija tumika kutatulia changamoto na matatizo ya wananchi. Kodi ambazo zimekusanywa tayari na hazija tatua changamoto bado ndiyo zitumike kutatulia kwanza changamoto kwa wananchi. Kwamba wasitozwe tozo nyingine mpaka zilizo kusanywa hapo awali zitumike sehemu husika ili kupunguza kupanda kwa gharama za maisha.
• Kodi zote zikusanywe kwa kuzingatia viwango vya mapato ya wananchi. Makusanyo ya kodi hayalingani na mapato ya wananchi kwamba kodi zimekuwa kama madeni kwa wananchi, badala ya kuwa suluhisho la kutatua matatizo ndani ya jamii zimekuwa kama madeni na zimezidi uwezo wa mapato ya kila mwananchi. Serikali iweke kodi ambazo zitaendana na uwezo wa mapato ya wananchi ili wajikwamue na umaskini.
• Serikali hitoe ufafanuzi juu ya makusanyo yaliyo kusanywa ambayo hayajatumika kutatulia changamoto za wananchi. Kodi zote ambazo zimekusanywa tayari na hazija tumika katika suala la utatuzi wa matatizo ya wananchi. Serikali ifafanue kwamba kodi zilizo kusanywa kwaajiri ya wananchi zilitumika kufanyia kitu gani na kwasababu gani na kinamsaada gani kwa wananchi.
• Kodi zote zitumike kwenye maeneo ambayo yana changamoto tu ili kutatua matatizo ya wananchi husika. Kodi nyingi zimekuwa haziendi sehemu husika kwaajiri ya kutatua changamoto za wananchi. Kodi zote ziende kwenye sehemu husika moja kwa moja na kutatua changamoto za wananchi.
• Utendaji kazi wa kodi zilizo kusanywa uwe wa wazi wazi usifichwe ili kuwa hamasisha wananchi wengine kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwaajiri ya maendeleo ya taifa. Kwenye makusanyo walipa kodi wanatakiwa wajue kiwango kilicho kusanywa na kiwango kinacho kwenda kutumika kwenye utatuzi wa changamoto za wananchi kwenye nyanja zote kwahiyo usifichwe.
Hitimisho
Mabadiliko na maendeleo bila kuwaumiza na kuwanyonya wananchi maskini kupita kiasi ndiyo tunayo yahitaji. Maendeleo hayo yanaletwa na sisi wenyewe kama taifa tuangalie namna bora itakayo chochea mabadiliko kwa haki ambayo yataleta manufaa kwenye taifa la sasa na la baadae.
Upvote
3